TFF Yataja Kiingilio Mpambano Yanga na AZAM FC

MCHEZO wa Ngao ya Hisani ambao ni sehemu ya ufunguzi wa pazi la Ligi Kuu ya Vodacom (VPL) nchini kati ya Azam FC dhidi ya Yanga SC utachezwa siku ya jumamosi katika uwanja wa Taifa jijini Dar es salam, ambapo kiingilio cha chini kitakua ni shilingi elfu saba. Fuata link chini kwa taarifa kamili Mchezo wa Ngao ya Hisani ambao …

Kumekucha Kombe la Kagame, Azam FC Yaanza Vizuri

MICHUANO ya Kombe la Kagame inayoendelea kutimua vumbi katika viwanja viwili vya Taifa na Karume vilivyopo jijini Dar es salaam, itaendelea kesho kwa michezo miwili itayopigwa katika dimba la Uwanja wa Taifa. Katika michezo iliyochezwa leo, Malakia ya Sudani Kusini iliibuka na ushindi wa mabao 2- 1 dhidi ya Adama City ya Ethiopia, LLB ya Burundi ikitoka sare ya bila …

Coastal Union Yajipanga Kuiangamiza Azam FC

Na Mwandishi Wetu, Tanga TIMU ya Coastal Union imewasili jijini Tanga ikiwa na mikakati mizito ya kuhakikisha inawanyamazisha wapinzani wao Azam FC ikiwa ni muendelezo wa Michuano ya Ligi kuu soka Tanzania bara mchezo unaotarajiwa kucheza kwenye uwanja wa CCM Mkwakwani wikiendi ijayo. Akizungumza na waandishi wa habari, Ofisa Habari wa Coastal Union, Oscar Assenga amesema kuwa sasa nguvu zao …

AZAM FC Wampelekea Rais Kikwete Kombe…!

Na dev.kisakuzi.com, Dar es Salaam TIMU ya Mpira wa Miguu ya Azam FC ambao ni mabingwa wapya wa Ligi Kuu ya Mpira wa Miguu Tanzania Bara, jana jijini Dar es Salaam ilimpelekea kombe la Ubingwa huo Rais wa Tanzania, Jakaya Kikwete. Azam inayomilikiwa na kampuni maarufu na tajiri Afrika Mashariki ya mfanyabiashara, Said Salim Bakhresa (SSB) inayotengeneza bidhaa mbalimbali nchini …

Azam FC Kukabidhiwa Kombe Kesho, Yanga na Simba Patashika…!

MICHUANO ya Ligi Kuu ya Vodacom (VPL) kuwania ubingwa wa Tanzania Bara inafikia tamati kesho (Aprili 19 mwaka huu) kwa timu zote 14 kuwa viwanjani, huku mabingwa wapya Azam wakikabidhiwa kombe lao Uwanja wa Azam Complex, Dar es Salaam katika mechi yao dhidi ya JKT Ruvu.   Mechi zote saba zitachezwa kuanzia saa 10 kamili jioni ambapo Yanga na Simba …