Benjamin Netanyahu Atimua Mawaziri Wawili

WAZIRI Mkuu wa Israel, Benjamin Netanyahu amewafukuza kazi mawaziri wawili ambao ni waandamizi na viongozi wa vyama katika serikali yake ya mseto jambo ambalo linatafsiriwa kuwa ameiweka nchi katika hali ya kufanyika mapema uchaguzi wa bunge. Akizungumza na waandishi wa habari kupitia televisheni, Netayahu amewashutumu mawaziri hao wawili akiwemo Waziri wa Fedha, Yair Lapid, na Waziri wa Sheria, Tzipi Livni …