KWA wakazi wa Kitongoji cha Kona Nne, Kijiji cha Ugembe II, Kata ya Mwakashanhala wilayani Nzega katika Mkoa wa Tabora, takriban kilometa 90 kutoka Nzega mjini, saa 3:00 ni usiku mkubwa na wengi wamelala baada ya shughuli za ujenzi wa taifa. Majira kama hayo, usiku wa Jumatatu, Juni 15, 2015 haukuwa na tofauti kubwa, isipokuwa giza lililotanda kutokana na mbalamwezi kuwa gizani. …
UNESCO Yaahidi Kupambana na Unyanyasaji wa Albino Tanzania
Kiongozi wa ofisi na mwakilishi wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) nchini, Zulmira Rodrigues (kulia) akisalimiana na Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, Magesa Mulongo (kushoto) alipomtembelea ofisini kwake jijini Mwanza akiwa ameambatana na Mbunge wa Viti Maalum CCM, anayetetea maslahi ya watu wenye albinism, Mh. Al-Shaymaa Kwegyir (wa pili kulia) pamoja na Semeni Kingaru …