Naibu Waziri Dk. Kigwangalla aagiza uboreshaji wa huduma za Afya Tunduru

  NAIBU waziri wizara ya Afya, Jinsia, Maendeleo ya Jamii, Wazee na Watoto, Dk. Hamisi Kigwangalla ametoa maagizo kwa Mkurugenzi wa Halmashauri ya Tunduru kuhakisha wanaboresha huduma za Afya katika Wilaya hiyo hasa kituo cha Afya Mkasale ambacho kimebainika kuwa na huduma mbovu huku pia kikiwa na uchakavu kwenye majengo yake hali ambayo inaweza kuhatarisha usalama na afya za watumishi …

Hospitali ya Wilaya Mkuranga Yakabidhiwa Gari la Wagonjwa na Vifaa Tiba

  NAIBU waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mh. Dk. Hamisi Kigwangalla mapema jana Mei 28.2017 amekabidhi gari maalum la kubebea wagonjwa (Ambulance) na vifaa vya Hospitali ikiwmo vitanda na Magodoro katika Hospitali ya Wilaya ya Mkuranga, Mkoani Pwani. Dk. Kigwangalla ambaye alikuwa mgeni rasmi katika tukio hilo, mbali na kukabidhi gari hilo la wagonjwa na …

Wizara ya Afya, UNDP Kuanzisha Mradi wa Kupunguza Taka

  Na Ally Daud, Maelezo – Dar es Salaam HOSPITALI za Muhimbili, Amana, Mwananyamala na Kairuki za Jijini Dar es Salaam zinatarajia kuwekwa kwenye mradi maalum wa kudhibiti taka hatarishi ikiwa ni mkakati wa Serikali wa kuboresha usafi wa mazingira katika huduma za afya nchini. Mradi huo wa kudhibiti taka hatarishi ikiwemo sindano, gloves, nyembe na bandeji unasimamiwa na Wizara …

USAID Kuendelea Kuisaidia Miradi Anuai ya Afya Tanzania

Na Rabi Hume BAADA ya kufanyika nchini kwa miaka 10, mradi wa SCMS ambao ulikuwa ukisimamiwa na John Snow Incorporated (JSI) kwa ushirikiano na Wizara ya Afya, Ustawi wa Jamii Jinsia, Wazee na Watoto, Shirika la Misaada la Watu wa Marekani (USAID) limeiahidi serikali ya Tanzania kuwa litaendelea kuisaidia katika misaada mbalimbali ya afya licha ya kumalizika kwa mradi huo. Hayo …

RC Kilimanjaro Afanya Ziara Hospitali ya Rufaa Mawenzi

Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro  Amos Makala akisalimiana na wafanyakazi wa Hospitali ya Rufaa ya Mawenzi mara baada ya kuwasili kwa ajili ya kutembelea idara mbalimbali hospitalini hapo. Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro,Amos Makala akitia saini katika kitabu cha wageni maara baada ya kuwasili katika hosptali ya Rufaa ya Mawenzi mkaoni Kilimanjaro. Mganga Mkuu wa Mkoa wa Kilimajaro Hajati, Dk. …

Watanzania Ughaibuni Watakiwa Kuwekeza Kwenye Afya Tanzania

WAZIRI wa Afya na Ustawi wa Jamii wa Tanzania, Seif Rashid na Waziri wa Afya wa Zanzibar, Rashid Seif Suleiman, Januari 25, 2015 walikutana na kuzungumza na na baadhi ya Watanzania waishio nchini Ujerumani. Mkutano huo ulifanyika katika Hoteli ya Martim mjini Berlin, ambapo mawaziri hao kwa pamoja wakiwa na Balozi wa Tanzania nchini Ujerumani, Philip Malmo walitumia fursha kuzungumza masuala mbalimbali. …