Oscar Pistorius Ahukumiwa Kwenda Jela Miaka 5

MWANARIADHA nyota wa nchi ya Afrika Kusini Oscar Pistorius amehukumiwa kwenda jela miaka 5 baada ya kupatikana na hatia ya kumuua mpenziwe Reeva Steenkamp bila kukusudia. Hukumu hiyo imetolewa baada ya mwanariadha huyo mlemavu kuthibitika kuwa alifanya mauaji hayo bila ya kukusudia. Jaji Thokozile Masipa akitoa hukumu hiyo alianza kwa kueleza kuwa itakuwa ni vigumu na changamoto kwake kutoa hukumu …