Vurugu za Ubaguzi Afrika Kusini; Nigeria Yaondoa Mabalozi Wake

TAIFA la Nigeria limewaita mabalozi wake waishio nchini Afrika Kusini kurejee nyumbani kufuatia mashambulizi ya kibaguzi dhidi ya wenyeji yanayofanyika Afrika Kusini. Mpaka sasa watu saba wameshapoteza uhai kufuatia mashambulizi hayo, yaliyoanza wiki tatu zilizo pita. Mali zimeharibiwa vibaya na mashambulizi hayo yamezusha hofu kubwa miongoni mwa raia wa kigeni. Balozi wa Nigeria mjini Pretoria, mji wa kibiashara na kwingineko …

Rais Zuma Awatembelea Raia wa Kigeni Wanaoshambuliwa Afrika Kusini

RAIS Jacob Zuma amewatembelea watu walioathirika na ghasia hizo, mauwaji pamoja na kuibwa kwa mali zao huku akiahidi kukabiliana vilivyo na wimbi la mashambulio hayo. Bwana Zuma alifutilia mbali ziara yake nchini Indonesia, ili kukabiliana na vurumai hizo zilizoanza majuma mawili yaliyopita. Amesema kuwa ghasia hizo ni kinyume na maadili ya taifa la Afrika kusini. Maofisa zaidi wa polisi wametumwa …

Idara Yamtetea Pistorius, Yataka Afungwe Nje

IDARA ya Kurekebisha Tabia nchini Afrika Kusini imeomba mwanariadha maarufu wa nchi hiyo Oscar Pistorius anayetuhumiwa kwa mashtaka ya kumuua mpenzi, Reeva Steenkamp apewe kifungo cha nyumbani cha miaka mitatu juu ya kosa linalomkabili la kumpiga risasi na kumuua mpenzi wake huyo. Ofisa toka idara hiyo, Joel Maringa ametoa ombi hilo kwenye Mahakama mjini Pretoria kuwa hawamuadhibu tu Pistoruiis bali …

ANC Yashinda Uchaguzi Mkuu Afrika Kusini

CHAMA cha ANC kimepata ushindi mkubwa katika uchaguzi uliofanyika Jumatano ya wiki iliyopita. Tume ya uchaguzi nchini Afrika kusini imetangaza matokeo rasmi ya uchaguzi mkuu huo na kusema kuwa chama tawala cha ANC kimejipatia ushindi mkubwa wa asilimia 62. Katika hotuba yake kwa taifa Rais jacob Zuma amesema kuwa matokeo hayo ni ishara njema kwamba raia nchini humo wana imani …