Bondia ‘Dula Mbabe’ Kuzipiga Vunja Jungu

BONDIA machachari wa ngumi za kulipwa nchini Abdallah Paziwapazi a.k.a ‘Kiroba’ au kama anavyojulikana na wengi ‘Dula Mbabe’ anatarajiwa kupanda ulingoni Juni 29, 2014 katika Ukumbi wa CCM Mwinjuma, Mwananyamala jijini Dar es Salaam kuzipiga na Hamis Juma ambaye ameonekana mbadala wa bondia Maneno Osward. Mpambano huo ambao utakuwa wa vunja jungu yaani wa kukaribisha mwezi mtukufu wa ramadhani, utaambatana na …