Daktari Mwingine Aambukizwa Ebola

DAKTARI, Olivette Buck ambaye alikuwa ni miongoni mwa madaktari wanaowatibu wagonjwa wa Ebola nchini Sierra Leone ameguduliwa kuambukizwa ugonjwa huo baada ya kufanyiwa vipimo. Dk. Olivette Buck anakuwa ni daktari wa nne kukumbwa na ugonjwa huo kutoka nchi za Afrika Magharibi. Madaktari wengine watatu walioshikwa na ugonjwa huo tayari wamefariki dunia. Akizungumzia tukio hilo Waziri wa Afya wa Sierra Leone, …