Taekwondo Ilivyotikisha Jiji la Arusha

IMG-20160416-WA0053

Mashindano ya Taekwondo yamefanyika mwishoni mwa Jijini Arusha yakishirikisha zaidi ya vijana 60 wa Rika mbalimbali kutoka Arusha na Mkoa wa Kilimanjaro

Licha ya kuwepo idadi kubwa ya washiriki wa mashindano hayo, upande wa wasichana hali imekuwa tofauti baada ya kuonekana mchezo wa hatari kwani kati ya 60 walioshriki wawili pekee ndio walikuwa wanawake ambao ni Grace Sugilo na Zuhura Suleiman wote kutoka shule ya Sekondari ya Edmond Rice

Mkuu wa Shule hiyo Simon Kaswahili Muda wote aliwapongeza vijana wake kwa jitihada wanazofanya katika kuendeleza michezo huku akiwahamasisha kuwa Mchezo huo ni ajira tofa siku za mbele

Kwa upande wao Zuhura na Grace walisema kuwa hawataweza kuuacha Mchezo huo hata kama wengi wanaukataa wakidai ni hatari lakini kwao ni silaha kubwa ya kujilinda na magonjwa pamoja na kuufanya mwili wao kuwa katika hali ya ukakamavu.

Mkurugenzi wa ufundi wa shirikisho la Taekwondo Tanzania (TTF) Richard Kitolo alisema kuwa mashindano hayo yaliandaliwa na Klabu ya Taekwondo ya Triple A ya jijini Hapa hivyo watahakiksha wanasimamia na kuuendelrza zaidi mchezo huo sio Arusha Pekee Bali Tanzania Nzima.

Kwa upande wake Ofisa wa Michezo wa Jiji la Arusha Benson Maneno ambaye alikuwa mgeni rasmi alitoa wito kwa wakufunzi wa mchezo huo kutafuta vijana wodogo ili waweze kuunda timu ya Taekwondo ya Jiji la Arusha ambayo itaghalimiwa na Jiji.

Washindi kwa uzito wa KG 48-53 wa kwanza ni Fredrick Marandu kutoka Edmund rice sec. school wa pili Brayson Alfred- Edmund rice sec.school na wa tatu ni Fahad Karim-edmund rice

Kwa uzito wa KG 55-58 wa kwanza Athuman Omary kutoka Moshi Taekwondo klabu wa pili Ronaldo Peter-Edmund rice na watatu Athuman Jumanne-Edmund rice

Washindi wa uzito wa KG 59-62 wa kwanza Laurance Makia-Triple A Taekwondo klabu wa pili Musa Ally-Moshi Taekwondo klabu wa tatu Kelvin Shayo- Triple A Taekwondo klabu.

Kwa washindi wa uzito wa KG 63-67 wa kwanza Felix Steven- Moshi Taekwondo klabu wa pili Samson Joachim-Moshi Taekwondo klabu
Huku washindi wa KG 68-70 wa kwanza alikuwa Geofrey Daud-Triple A Taekwondo wa pili Frank –Moshi Taekwondo kalbu na watatu Daniel Manase-Jet kan do kalbu

Hivyo basi washindi wa jumla nafasi ya kwanza iliwaendea TRIPLE A Taekwondo ,ambao walipata medali za dhahabu 2,medali ya fedha 3 na medali ya shaba 4,nafasi ya pili iliwaendea shule ya Edmund Rice kwa kutwaa medali za dhahabu 2 ,Fedha 3,na shaba 4 na nafasi ya tatu iliwaendea Moshi taekwondo klabu kwa kupata medali ya dhahabu 2,fedha 3 huku wakikosa medali ya shaba.