Taarifa za Uchaguzi Mpira wa Miguu Vyama vya KAREFA, TASMA, RUREFA

Tanzania Football Federation Logo

Mchakato wa uchaguzi wa KAREFA umefutwa kutokana na wagombea watano kati ya nane vyeti vyao vya elimu ya sekondari kuwa na utata. Mchakato wa uchaguzi huo utaanza upya Novemba 21 mwaka huu.

Mchakato wa uchaguzi wa Chama cha Wataalamu wa Tiba ya Michezo Tanzania (TASMA) utaanza upya Novemba 26 mwaka huu baada ya mchakto wa sasa kupata wagombea kwenye nafasi mbili tu za Kamati ya Utendaji ya chama hicho.

Mchakato wa uchaguzi wa RUREFA utaanza Novemba 26 mwaka huu na Kamati ya Uchaguzi ya RUREFA itapewa maelekezo ya usimamiaji wa uchaguzi huo baada ya mchakato wa awali kuwa umefutwa kutokana na kufanyika bila kuzingatia kanuni za uchaguzi.

Wakati huo huo; Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) litakuwa na mkutano na Waandishi wa Habari utakaofanyika Novemba 22 mwaka huu. Mkutano huo utafanyika saa 6 kamili mchana kwenye ukumbi wa mikutano wa TFF.