Waziri wa Mazingira Dk. Terezya Huvisa ambaye ni Rais wa Mawaziri wa Mazingira Barani Afrika akiipongeza Hoteli ya DoubleTree by Hilton kwa kuona umuhimu wa elimu kwa kukabidhi taa mia mbili kwa Shule za Msingi zilizopo manispaa ya Songea mkoani Ruvuma , Shule zilizopewa msaada huo ni Shule ya msingi Mletele, Mwanamonga, Liumbu na Namang’ula , Taa hizi zinazotumia Nishati ya jua pia ni rafiki wa mazingira. ” Taa hizi zitawasaidia kuepeuka kutumia vibatari na mishumaa muda wa kujisomea kwa sababu ni hatari kwani vimekuwa vikisababisha majanga ya kuungua kwa watoto wengi nchini “.
Mkuu wa wilaya ya Songea Bw. Joesph Joseph Mkirikiti alie kaa katikati na kutoka kulia kwake ni Mkurugenzi wa kanda ya Africa mashariki wa Hoteli za DoubletTree by Hilton Tanzania Bw. Judd Helman na alie kaa kushoto ni mkurugenzi wa Masoko Hoteli ya DoubleTree by Hilton Florenso Kirambata wakati wa hafula ya kukabidhi msaada wa taa zinazotumia nishati ya jua.
Mkuu wa wilaya ya Songea Bw. Joseph Joseph mkirikiti akiteta jambo na mkurugenzi wa Masoko Hoteli ya DoubleTree by Hilton Florenso Kirambata (kushoto) juu ya matumizi ya taa zinazotumia nishati ya Jua ambazo pia ni rafiki wa mazingira kwa Wanafunzi wa darasa la Saba. Kulia ni Mkurugenzi wa kanda ya Africa mashariki wa Hoteli za DoubletTree by Hilton Tanzania Bw. Judd Helman.
Toka kushoto ni Mkurugenzi wa Masoko Hoteli ya DoubleTree by Hilton Florenso Kirambata akiwa ameshikilia taa na wakatikati ni mkuu wa wilaya ya Songea Bw. Joseph Joseph mkirikiti akiwa ameshikilia taa na wa mwisho ni Mkurugenzi wa kanda ya Africa mashariki wa Hoteli ya DoubletTree by Hilton Bw. Judd helman.
Mkurugenzi wa kanda ya Africa mashariki wa Hoteli ya DoubletTree by Hilton Bw. Judd helman akimkabidhi moja ya taa inayotumia nishati ya Jua mwanafunzi wa Shule ya Msingi Liumbu iliyopo ndani ya manispaa ya Songea mkoani Ruvuma .
Wanafunzi toka katika shule nne za msingi Mletele, Mwanamonga, Liumbu na Namang’ula na wakifatilia kwa makini hutuba iliyokuwa ikitolewa kabla ya kukabidhiwa taa zinazotumia Nishati ya jua ambazo zimetolewa na Hoteli ya DoubleTree by Hilton.
Wanafunzi hao wameishukuru Hoteli hiyo na kusema taa hizo zitawasaidia kujisomea hata kipindi ambacho Umeme umekatika majumbani hivyo kuongeza uwezo wao kielimu na kupunguza matumizi ya kununua mafuta ya taa kwa ajili ya kusomea
Naye Mkurugenzi wa Masoko Hoteli ya DoubleTree by Hilton Florenso Kirambata amesema
“tumeamua kufanya kampeni hii ambayo ni endelevu tutakuwa tukigawa taa 200 za mezani zenye kutumia nishati ya jua kwa wanafunzi wa darasa la saba kwa shule tofauti kila mwezi, lengo likiwa nikuwafanya wawe na ufahamu zaidi juu ya chanzo kingine cha umeme ambacho ni rafiki wa mazingira vile vile tunaomba wahisani wengine nao wajitokeze”.
Picha na habari kwa hisani ya www.demashonews.blogspot.com