SuperSport Kuonesha Mechi Mzunguko wa Pili

Boniface Wambura Ofisa Habari, TFF

MIZUNGUKO wa pili ya Ligi Kuu ya Vodacom unaanza Januari 26 mwaka huu huku kukiwa na maombi ya televisheni ya SuperSport kuonesha mechi za Super Week kama ilivyokuwa katika mzunguko wa kwanza.

Ofisa Habari wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), Boniface Wambura katika taarifa aliyoitoa itoa leo kwa vyombo vya habari alisema raundi tano za awali katika ratiba ya mzunguko wa pili zinabaki kama zilivyo wakati nyingine zilizobaki zitatolewa baada ya kuingiza mechi za Super Week.

Wakati huo huo, mzunguko wa pili wa Ligi Daraja la Kwanza unatarajia kuanza Januari 26 mwaka huu. Ratiba ya ligi hiyo na tarehe rasmi ya kuanza itatangazwa baada ya kupitiwa na Kamati ya Ligi ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) inayotarajiwa kukutana mwishoni mwa wiki.