Super D Kufanya Ziara Kuhamasisha Ngumi Tanga

Super D Kufanya Ziara Kuhamasisha Ngumi Tanga

ZIARA hiyo yenye lengo la kuhamasisha mchezo wa ngumi kwa vijana na kuwapa mbinu mpya baadhi ya makocha wa mikoa husika ili mchezo wa ngumi uweze kusonga mbele ingawa mchezo huo unapendwa na wenga na kukwepwa na wadhamini ndicho kitu kinachokifanya mchezo wa masumbwi uonekane umeshuka hadhi yake wakati bado upo juu.

Akizungumzia safari hiyo Super D amesema safari hiyo ni ya manufaa sana kwa watu wa mikoani kwani bado mikoa mingi atatembelea kutoa elimu ya mchezo huo na kuhamasisha vijana wengi wajiunge na mchezo huo kwani yaweza kuwa ni ajira yao. 

Super D ambaye ni kocha wa kwanza kutoa mafunzo yake kwa njia ya DVD zilizochanganywa na clips mbalimbali. CD hizo zilizotengenezwa kwa umakini wa ali ya juu ambazo ni chachu kwa ajili ya kuvutia wapenzi na mashabiki mbalimbali kujua mchezo wa masumbi

DVD hizo kwa sasa zinapatikana katika makutano ya barabara ya Uhuru na Msimbazi au unaweza kuzipata jengo la Azam lililopo mtaa wa Msimbazi karibu na kituo cha Polisi Post Gerezani wasiliana na kocha kwa simu 0713406938 ili uweze kupata dvd hizo kwa ajili ya kujifunza zaidi mchezo huo.

DVD zina mabondia wakari wanaotamba Duniani kama vile Manny Paquaio, Floyd Maywether, Roy Jones, Miguel Cotto, Linox Lewis, David Haye, Mohamed Ali na wengine wengi. Super D aliongeza kuwa mikoa mingine atakayotembelea ni abora, Singida, Dodoma, Morogoro, Iringa, Mbeya na Songea.

ambapo amewaomba baadhi ya makocha, wadau wa mchezo huo wa mikoa husika ambao ajawai kuonana mikoa iliyotajwa kuwasiliana nae ili wabadilishane ujuzi kwani kuna wengine awana mawasiliano nao waweza kumpigia kwa 0713 406938 ili kupeana ufundi na ujuzi zaidi wa mchezo wa masumbwi ili usonge mbele zaidi.