SUMATRA Yapandisha Nauli za Daladala na Mabasi Mikoani

SUMATRA Yapandisha Nauli za Daladala na Mabasi ya Mikoani

MAMLAKA ya Udhibiti Usafiri wa Nchi Kavu na Majini (SUMATRA) imepandisha viwango vya nauli za daladala na mabasi ya mikoani baada ya kukamilisha mchakato wa kuridhia viwango hivyo vipya
kiutaratibu. Akitangaza viwango hivyo jana jijini Dar es Salaam, Kaimu Mkurugenzi wa SUMATRA, A.S.K. Kilima alisema viwango hivyo vitaanza kutumika rasmi Aprili 12, 2013 maeneo yote kama ilivyoelekezwa.

Alisema kwa mujibu wa viwango hivyo vipya mwanafunzi kwenye daladala atalipa nusu ya nauli ya mtu mzima ya sh 200 kwa umbali wowote. Alisema kwa mtu mzima kwa umbali wa kawaida (mfupi) atalipa sh 400 badala ya Sh 300 ya awali. Alitolea mfano kwa njia za kuanzia kilomita kati ya 0 – 10 (Namipaka ya Jiji Kati) sasa itakuwa ni Sh 400 (Ubungo – Kivukoni).

Na kwa kilomita kati ya 11 – 15 itakuwa ni Sh 450 (Mwenge – Temeke), Kilomita kati ya 16 – 20 itakuwa Sh 500 (Tabata Chang’ombe – Kivukoni), Kilomita kati ya 21 – 25 ni Sh 600 (Pugu Kajiungeni – Kariakoo) na Kilomita kati ya 26 – 30 itakuwa Sh 750 (Kibamba – Kariakoo). Alisema mamlaka hiyo imeandaa majedwali kwa njia zote za Dar es Salaam kuonesha nauli hizo ili kuondoa usumbufu na pia viwango hivyo vipya vitapatikana kwenye tovuti ya SUMATRA www.sumatra.or.tz.

“Viwango hivi vipya vimefikiwa baada ya kufuata taratibu za kisheria na za kiutendaji ambazo SUMATRA kama msimamizi na mdhibiti wa sekta ya usafiri wa barabara inapaswa kuzifuata kabla ya kuridhia viwango hivyo. Viwango vipya vya naulivitaanza kutumika kuanzia tarehe 12 Aprili, 2013,” alisema Kilima akizungumza na vyombo vya habari.

Aidha alisema SUMATRA ina jukumu lakujenga na kulinda mazingira mazuri na ya kuvutia kwa watoa huduma ili huduma yausafiri inayotolewa inakuwa katika kiwango na gharama zinazoendana na hudumazenyewe. Aliongeza kuwa katika kipindi cha mwaka wa fedha wa 2011/2012, SUMATRA ilipokea maombi kutoka kwa wamiliki wa vyombo vya usafiri wa barabara yakiwemo makampuni ya usafirishaji abiria.

Wakati maombi ya wamiliki wa Daladala yalilenga katika kuongeza viwango vya naulikwa 149% ya viwango vya sasa, wamiliki wa mabasi ya masafa marefu waliombanyongeza kati ya 35% na 48.5%. Kwa mujibu wa Kifungu Na 18 cha Sheria ya SUMATRA, 2001, SUMATRAiliwashirikisha wadau mbalimbali katika kujadili na kupata maoni yao kuhusu maombi yawamiliki ya kuongeza viwango vya nauli kabla ya kufanya maamuzi ya mwisho.

Aidha Mamlaka iliridhia viwango vipya kwa mujibu wa kifungu cha 16 Cha Sheria yaSUMATRA ambacho kinaipa Mamlaka kufanya mapitio ya nauli mara kwa mara kwakuzingatia gharama za kutoa huduma, maslahi ya watoa huduma, faida, maslahi yawatumia huduma ya kulipa nauli yenye uwiano na gharama za huduma inayotolewa.

Kwa kuzingatia hoja za waombaji, maoni ya wadau, uchambuzi wa menejimenti, haja yakupunguza gharama zisizo za lazima za uendeshaji na udhibiti wa vitendo vya uvunjajiwa Sheria na taratibu za uendeshaji shughuli za usafirishaji, Mamlaka ya SUMATRAiliamua kuongeza viwango vya juu vya nauli za Daladala kwa wastani wa 24.46%.

Kwa usafiri wa reli pia umepanda ambapo daraja la kwanza Dar es Salaam hadi Morogoro, nauli mpya na ya zamani katika mabano ni Sh21,100, (Sh16,852), Dar hadi Dodoma Sh34,700, (Sh27,788), Dar es Salaam-Tabora Sh54,800, (Sh43,859). Dar es Salaam-Isaka Sh62,100, (Sh49,662), Dar- Shinyanga Sh65,300 (Sh52,229) Dar –Mwanza Sh74,800 (Sh 59,818), Dar- Kigoma Sh75,700, (Sh60,599).

Daraja la pili, Dar es Salaam-Morogoro Sh16,600, (Sh13,280), Dar es Salaam-Dodoma Sh26,400 (Sh 21,092), Dar es Salaam-Tabora Sh40,500 (Sh 32,364), Dar es Salaam-Isaka Sh45,800, (Sh36,605), Dar es Salaam-Shinyanga Sh48,000 (Sh38,390), Dar es Salaam- Mwanza Sh54,700 (Sh43,747), Dar es Salaam-Kigoma Sh55,400 (Sh44,305).

Daraja la tatu, dar es Salaam-Morogoro Sh8,800 (Sh6,138), Dar es Salaam-Dodoma Sh13,500 (Sh9,374), Dar es Salaam-Tabora 20,400 (Sh14,173), Dar es Salaam-Isaka Sh22,800 (Sh15,847), Dar es Salaam –Shinyanga Sh24,000 (Sh16,628), Dar es Salaam-Mwanza Sh27,200 (Sh18,860), Dar es Salaam- Kigoma Sh27,500 (Sh19,084).

Aidha kwa mabasi ya masafa marefu, viwango vimeongezwa kwa 20.3% kwa mabasi yakawaida, 16.9% kwa mabasi ya daraja la kati na 13.2% kwa mabasi ya daraja la juu. Mchanganuo wa viwango vipya vya nauli ni kama ifuatavyo: Nauli za Mabasi ya Masafa Marefu Daraja la Basi Nauli yazamani kwa km-abiria Nauli mpya kwa km-abiria Mfano wa kiwango kipya cha nauli kwa baadhi ya njia Basi la Kawaida kwa njia ya lami Sh 30.67Sh 36.89 DSM–Mbeya Km 833Sh 30,700 Basi la Kawaida kwa njia ya vumbi Sh 37.72 Sh 46.11S/wanga-Kigoma Km 551 Sh 25,400 Basi la hadhi yakati (SemiLuxury Sh 45.53Sh 53.22 DSM–Mwanza Km 1,154 Sh 61,400 Basi la hadhi ya juu (Luxury) Sh 51.64Sh 58.47 DSM–Arusha Km 616 Sh 36,000.

Ili kuhakikisha kuwa kuna uwiano kati ya viwango vipya vya nauli na ubora wa huduma ya usafiri, Mamlaka imetoa maagizo kwa wamiliki wa mabasi ya masafa marefu kuboresha maeneo yanayo husiana na huduma ya usafiri kama; Wamiliki wa mabasi kutokutumia wapiga debe katika kuuza tiketi zasafari, kuhakikisha wanafuata Kanuni za SUMATRA za Udhibiti wa Tozo na Nauli (SUMATRA Tarrif Regulations) ambazozinahimiiza kuwepo kwa kumbukumbu sahihi za mahesabu ili kurahisisha mapitio ya viwango vya nauli.

Kutoza nauli kwa mujibu wa daraja la basi lenye sifa kamili la daraja husika kama ilivyoainishwa katika Kanuni za Usalama na Ubora Aidha kwa mabasi ya mjini, Mamlaka imetoa maelekezo yafuatayo: Kuhakiksha kuwa abiria wote wanapatiwa tiketi, Kudhibiti vitendo vya ukiukwaji wa Sheria ikiwemo kutokamilisha safari maarufa kama kukata ruti, kubadili njia na unyanyasaji wa aina yoteyotekwa abiria.