Meneja Mawasiliamo wa Sumatra, David Mziray akisisitiza jambo kwenye mkutano huo na waandishi wa habari uliofanyika kwenye ukumbi wa Bandari Mkoani Tanga.
Mkurugenzi wa ulinzi na usalama wa Mamlaka ya Udhibiti wa Usafiri wa nchi kavu na majini (Sumatra) Captain Mussa Mandia, katikati akizungumza na waandishi wa habari mkoani Tanga kuzungumzia mpango maalumu wa kupambana na uchafuzi wa mazingira baharini, kushoto ni Meneja Mawasiliamo wa Sumatra, David Mziray kulia ni Mwakilishi wa Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Usafiri Baharini Zanzibar(ZMA) Suleiman Masoud.
Mwakilishi wa Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Usafiri Baharini Zanzibar(ZMA) Suleiman Masoud akizungumza katika mkutano huo.
PRO wa Mamlaka ya Bandari Mkoani Tanga (TPA) Moni Jarufu akifuatilia mkutano huo na waandishi wa habari wa mkoani Tanga
MAMLAKA ya udhibiti wa usafiri wa majini na Nchi Kavu (SUMATRA) imekusudia kuanzisha mpango mkakati maalumu wa udhibiti uchafuzi wa mazingira baharini (NMOSCRP) unaosababishwa na umwagaji wa mafuta unaofanywa bila ya kufuata taratibu za mazingira zilizowekwa na kuharibu mazingira.
Hayo yalibainishwa leo na Mkurugenzi wa Ulinzi na Usalama wa vyombo vya majini Taifa Capt Mussa Hamza wakati akizungumza na waandishi wa habari kuhusiana na maadhimisho ya siku ya wiki ya bahari dunia inayofanyika Kitaifa Mkoani Tanga kwenye viwanja vya Tangamano kesho Jumanne.
Ambapo Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Makame Mbarawa anatarajiwa kuwa mgeni rasmi kwenye maadhimisho hayo yatakayokwenda sambamba na maonyesho mbalimbali na warsha itakayofanyika Septemba 28 mwaka huu.
Alisema kuwa kutokana na kuwepo kwa biashara ya usafirishaji wa mafuta kwa njia ya bahari wame lazimika kuanzisha mpango huo ili kukabiliana na uchafuzi huo ambao unaweza kuchangia utoekaji wa viumbe vya vilivyopo.
Aidha alisema kuwa kutokana na uchavuzi huo wa mazingira uliopitiliza unachangia kwa kiasi kikubwa kuhatarisha mazilia ua samaki katika bahari na viumbe vingine vilivyomo baharini.
Alisema Tanzania imeingia katika shughuli za uchimbaji wa gesi na mafuta ambapo usafiri mkubwa wa mafuta ni kwa njia ya bahari hali ambayo inalazimika kuanzisha sheria maalumu ambayo inaweza kulinda mazingira ya bahari.
“Hakuna vyombo vinavyokuwa na uwezo wa kubeba mizigo mikubwa kama vyombo bya baharini hivyo imetulazimu kuanzisha mpango maalumu ambao tunategemea kesho kuuzindua ili kuweza kukabilia na uchavuzi wa mazingira katika bahari yetu ya Hindi,” Alisema.
Hamza alitumia fursa hiyo kueleza kuwa miongoni mwa sababu za kufanya maadhimisho hayo Kitaifa Mkoa wa Tanga ni kutokana na mkoa huo kuingia katika mradi mkubwa wa usafirishaji wa mafuta kwa njia ya bomba kutoka nchini Uganda hadi bandari ya Tanga ambapo kutakuwepo na fursa kubwa ya kuitangaza Tanga kwa wawekezaji.
Kwa upande wake Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya usafirishaji wa Majini Zanzibar (ZMA) Suleiman Masoud alisema kufanyika kwa maadhimisho hayo katika mkoa wa Tanga ni tija kwa bandari ya Tanga,kupitia maadhimisho hayo lengo ni kuitangaza bandari hiyo kwa wafanya biashara wakubwa ndani na nje ya nchi.
Alisema Tanga inaweza kuwa ni sehemu kuu ya kitovu cha biashara ya usafirishaji wa mafuta kwa njia ya bahari na hata nchi kavu ikiwa itawekewa mipango madhubuti ya kuifufyua bandari ya Tanga.
Habari kwa Hisani ya Blog ya Kijamii ya Tanga Raha