RAIS wa Ufaransa Nicholas Sarkozy na Chansela wa Ujerumani Angela Merkel wametoa mapendekezo mapya kukabiliana na mgogoro wa kiuchumi unaokabili mataifa yanayotumia sarafu ya Euro.
Viongozi hao wanataka mfumo mpya kusimamia uchumi wa ulaya
Baada ya kukutana mjini Paris, viongozi hao walitoa wito wa kile walichokitaja kuwa usimamizi mpya wa kiuchumi na kuyataka mataifa yanayotumia sarafu hiyo kusawazisha bajeti zao.
Viongozi hao wanasema mgogoro wa kiuchumi unaoendela bara ulaya ni ishara ya jinsi ilivyo vigumu kwa nchi kutumia sarafu ikiwa hawana mikakati maalum ya kusimamia matumizi ya pesa za serikali.
Pendekezo lililotolewa na viongozi hao ni njia moja tu ya kufikia mpango huo.
Rais Sarkozy na Bi Merkel wamependekeza kubuniwa kwa mfumo huo mpya wa utawala utakao simamia msauala ya uchumi bara ulaya utasimamiwa na viongozi wa nchi wanachama wa umoja wa ulaya na watakuwa wakikutana mara mbili kwa mwaka.
Hata hivyo viongozi hao hawajaweka bayana viongozi hao watakuwa na mamlaka yapi.
Rais Sarkozy na Chansela Merkel pia wametaka sheria mpya zibuniwe ifikiapo mwaka ujao ambapo zitalazimu nchi wanachama kuwa na makadirio ya bajeti zao ambayo yataambatana.
Viongozi hao pia wametangaza kuwa watatoa mfano ambapo nchi zao- Ufaransa na Ujerumani- watakuwa na mfumo mmoja wa kulipisha kodi kwa wafanyibiashara wao.
Wadadisi wanasema mapendekezo haya ni njia moja ya kusuluhisha mgorogoro wa kiuchumi unaoshuhudiwa bara ulaya, lakini kwa sasa hakuna kubwa yanaweza kufanya kudhiti tatizo lililopo.
Soko la hisa bara ulaya lingeimarika ikiwa viongozi hao wangetangaza kutolewa kwa pesa za kusaidia nchi zingine kulipia madeni yao lakini hatua hiyo haijatangazwa.
-BBC