Suluhu kwa Wagonjwa wa Figo, Mfumo wa Mkojo Yapatikana

Dk. Sanjay Maitra

Dk. Sanjay Maitra


SULUHU kunufaika na kile ambacho wachambuzi huona kama nafasi adimu katika sekta ya afya. Hii ni kwasababu nchi inatarajia kupokea wataalamu wawili kutoka taasisi mashuhuri ya matibabu duniani. Kwa kushirikiana na madaktari kutoka hosipitali ya Hindu Mandal. Madaktari kutoka hospitali ya Apollo watahudumia na kutoa ushauri kwa wagonjwa wa figo na mfumo wa mkojo siku ya Oktoba 10 na Oktoba 11 katika Hospitali ya Hindu Mandal Dar es Salaam.

Watanzania wengi wenye maradhi hayo hushindwa kupata matibabu hapa nchini na badala yake husafiri nje ya nchi kwa ushauri na matibabu. Lakini kwa sasa wanaweza kupata huduma hiyo hapa Tanzania katika hosipital ya Hindu Mandal. Madaktari hao wawili kutoka hosipital inayoongoza katika kutoa huduma bora duniani ya Apollo wanatarajia kutoa huduma iliyo na ubora uleule hapa nchini Tanzania.

Watanzania watapata fursa ya kuonana na madaktari kati ya saa 3 kamili asubuhi mpaka saa 8 kamili mchana siku ya Ijumaa na Jumamosi kuanzia saa 10 kamili jioni mpaka saa 1 na nusu usiku kwa gharama ya shilling 45,000 tu kwa kila mgonjwa kwa ajili ya kumuona dokta.

Ujio wa Dk. Sanjay Maitra na Dk. Rajagopal katika hosipital ya Hindu Mandal ni sehemu ya nia ya dhati ya hospitali ya Apollo ya kutoa huduma bora za matibabu kwa wote na kujenga uhusiano mzuri na nchi ya Tanzania ambao ulianza zaidi ya miaka kumi iliyopita. Madaktari hawa wakiwa Tanzania watakuwa kuwawafuatilia wagonjwa mbalimbali, kupitia upya kesi za magonjwa yao na kutoa ushauri juu ya matibabu kama taarifa za matibabu zinavyoeleza.

Hatua hii ni sehemu mpango mkakati wa hospital za Apollo wa kutokomeza magonjwa kama haya nchini Tanzania. Hatua hii imechukuliwa kutokana na utafiti uliofanyika hivi karibuni.

Kulingana utafiti uliofanywa na Shirika la Afya Duniani (WHO)  mwaka 2011 vifo vitokanavyo na ugonjwa wa figo nchini Tanzania vimefikia 4533 sawa na 1.03 asilimia ya vifo vyote. Takwimu hizi zimeiweka Tanzania katika nafasi ya 54 duniani.

Ugonjwa wa figo umeripotiwa kuwa katika asilimia 14 miongoni mwa watu wazima katika hospitali kulingana ujumla idadi ya watu. Chanzo cha kifo kwa wagonjwa hao ni kushindwa kwa figo na mishipa ya  moyo au matatizo yanayojitokeza kutokana na ugonjwa huo. Katika utafiti mwingine uliofanyika hivi karibunina Shirika la Afya Duniani WHO mwaka 2012 nchini Tanzania.

Wagonjwa 100 waligundulika kuwa na magonjwa sugu ya figo kutoka jumla ya wagonjwa 1,476 waliokuwa na magonjwa mbalimbali, asilimia 61 walikuwa wanaume ambapo kati yao asilimia 91 walikuwa katika ugonjwa sugu wa figo katika hatua ya nne na tano.

Dk. Sanjay Maitra ni mtaalamu wa magonjwa ya figo. Anatarajia kuhudumia Watanzania wenye matatizo hayo katika kuwepo kwake nchini Tanzania. Amefanikiwa katika upandikizaji wa figo kwa watu zaidi ya 500 uliofanyika chini ya usimamizi wake. Hivyo basi ana uzoefu mkubwa sana katika masuala ya figo.

Mtaalamu wa mfumo wa mkojo  na viungo vya uzazi kwa wanaume,  Dk. Rajagopal atakuwa akihudumia wagonjwa wenye matatizo yanayohusiana na hayo kwa kulenga zaidi katika upasuaji na matibabu. Wagonjwa wanaohitaji Matibabu au ushauri  juu ya jiwe katika figo, uhadubini, kufeli kwa kibofu cha mkojo, matatizo ya mfumo wa mkojo, upandikizaji wa figo, utasa, ukosefu wa nguvu za kiume, maambukizi ya kawaida au matatizo mengine yanayohusiana na mfumo wa mkojo na viungo vya uzazi kwa wanaume wanashauriwa  kutokosa fursa hii iliyopo  mbele yao.

Katika kiliniki hiyo ya siku 2, wagonjwa watapimwa ili  kugundua hali yao na kushauriwa kama  wanaweza kupata dawa na tiba ndani ya nchi ambayo itasaidia kuponya maradhi yao. Kwa upande mwingine, kulingana na ukali wa hali ya mgonjwa, watakuwa wanashauriwa kutafuta matibabu zaidi ikibidi kwenda nje ya nchi kwa ajili ya matibabu ya maradhi ya figo kutokana na ukosefu wa kituo cha matibabu ya figo nchini Tanzania.

Gharama ya kusafirisha wagonjwa wa hali hii nje ya nchi si tu ghali kwa serikali bali hata kwa wagonjwa wenyewe hukosa fedha za kutosha kuwawezesha kupata tiba bora nje ya nchi. Hivyo kliniki hii ya siku mbili kupitia madokta hawa ni baraka kwa wagonjwa wanaosumbuliwa na figo na magonjwa yanayohusiana na mfumo wa mkojo  ambao hawawezi kumudu kusafiri nje ya nchi kwa matibabu zaidi.

Bw. Radhey Mohan, Makamu Rais wa Shirika la kimataifa la Maendeleo ya Biashara ndiye anayewezesha kliniki hiyo katika hospitali Hindu Mandal.

Kuhusu hospitali za apollo
Hospitali ya Apollo ilifunguliwa mnamo mwaka 1983, na kutoka kipindi hicho imekuwa ikiendeshwa kwa kauli mbiu isemayo “Dhamira yetu ni kuleta huduma ya kisasa karibu kabisa na walengwa. Tunajitolea kutoa huduma bora na mafanikio katika elimu na  utafiti kwa ajili ya jamii  ya kibinadamu”.

Katika miaka 30 tokea kuanzishwa kwake, hospitali ya Apollo imeandika historia kubwa kupata kuonekana nchini India. Ni moja ya kampuni kubwa ya Afya katika bara la Asia, na pia imeleta mapinduzi makubwa katika sekta ya afya nchini india. Katika safari yake, imeweza kuboresha maisha ya watu wapatao milioni 39 kutoka nchi 120.

Inatoa huduma maalum 52 na vitanda vya upasuaji 710
Imefanya upasuaji wa moyo wenye kufikia idadi ya watu 152,000 na panuzi 125, 000 za mishipa myembamba. Imefanya upasuaji wa wa viungo unaopita kiasi cha idadi ya watu 10,000, upasuaji wa uvimbe wa ubongo, uti wa mgongo na zaidi. Novalis TX, PET MRI na Upasuaji unaotumia mashine za kiroboti.