Meneja Uhusiano na Mawasiliano wa Taasisi ya Maendeleo Mkoa wa Morogoro, James Mbaligwe, akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari Dar es Salaam leo asubuhi kuhusu mkataba huo walioingia na Suky Classic Boutique wa kusaidia elimu nchini
Mkutano na wanahabari ukiendelea.
Na Dotto Mwaibale
TAASISI ya Maendeleo ya Elimu Mkoa wa Morogoro (Medo), imepata udhamini wa asiliamia tano kutoka duka la nguo za kisasa la Suky Classic la Kinondoni Manyanya jijini Dar es Salaam.
Akizungumza na waandishi wa habari kwa niaba ya Mkurugenzi Mkuu wa duka hilo Dar es Salaam juzi, Mkurugenzi Msaidizi wa duka hilo, Kiki Juma alisema waliguswa na mradi huo wenye lengo la kusaidia mahitaji ya watoto hao ili wapate elimu.
“Tunapenda kuwasapoti watoto hawa waliochini ya mradi unaoendeshwa na Medo kwa kuwasaidia mahitaji muhimu kama peni. daftari, sare za shule na mahitaji mengine” alisema Juma.
Meneja Uhusiano na Mawasiliano wa Taasisi ya Maendeleo ya Elimu Mkoa wa Morogoro, James Mbuligwe alisema msaada huo umetolewa wakati muafaka ukizingatia ni msimu wa kufungua shule ambapo watoto hao waliochini ya mradi wanamahitaji mengi.
“Kwasasa taasisi yetu imezindua kampeni maalumu ya ‘Nisaidie 500 Yatosha kunipa elimu ambapo balozi wa mradi huo ni Msanii Wastara Sajuki” alisema Mbuligwe.
Alisema wasanii na watu maarufu mbalimbali wameguswa kusaidia mradi huo ambapo Linah Sanga amejitolea kuandaa chakula cha hisani baada ya mfungo wa ramadhani kwa lengo la kuchangisha fedha za kusaidia watoto walio ndani na nje ya mradi kujengewa kituo cha elimu mkoani Morogoro.
Alisema msanii Kajala Masanja, Mshereheshaji Pilipili na mshindi wa Big Brother Afrika kwa umoja wao wamejitolea kusaidia watoto hao kwa kuchangisha fedha kupitia mitandao yao ya kijamii kwa ajili ya kusaidia mradi huo. Mbuligwe alitumia fursa hiyo kuwaomba watanzania popote walipo kuusaidia mradi huo ili uweze kuwafikia watoto wengi zaidi kote nchini.