Nchi ya Sudan ndiyo itakayokuwa mwenyeji wa michuano ya Kombe la Cecafa mwaka huu, baada ya Shirikisho la Soka Afrika Mashariki na Kati kutangaza.
Taifa hilo liliandaa michuano hiyo mara ya mwisho 2013.Uganda ndiyo itakayokuwa mwenyeji wa michuano ya wachezaji wasiozidi umri wa miaka 17 yaani Cecafa Under-17 na pia michuano ya ubingwa upande wa wanawake mwaka huu.
Burundi itakuwa mwenyeji wa fainali za wachezaji wa chini ya miaka 20. Cecafa pia imetangaza mpango wa miaka mitano ambao utasisitiza ukuaji wa soka ya chipukizi na wanawake pamoja na kuimarisha uwezo wa kiufundi.
Hayo yakijiri, rais wa Shirikisho la Soka la Somalia Abdiqani Said Arab ameteuliwa naibu mwenyekiti wa Cecafa.