MAPIGANO yaliyodumu kwa zaidi ya miezi minane nchini Sudan Kusini yameliacha eneo hilo likikabiliwa na njaa baada ya wakulima kushindwa kuendesha shughuli za kilimo yakikimbia mapigano. Umoja wa Mataifa, UN umesema takriban watu milioni nne wako katika hatari kubwa ya kukosa chakula baada ya wakulima kushindwa kuzalisha msimu huu.
Mvua zinazoendelea kushesha pia zimekwamisha zoezi la usambazaji wa misaada nchini Sudan Kusini. Mvua hizo pia zimeharibu barabara na kufanya juhudi za usambazaji misaada kuwa ngumu zaidi. Wataalam wameonya kuwa baa la njaa huenda likaikumba Sudan Kusini mwishoni mwa mwaka 2014, hii ni kutokana na idadi kubwa ya watu wakiwa tayari wanakabiliwa na ukosefu mkubwa wa chakula.
-BBC