Suala la Mauaji ya Albino ni letu Sote

Balozi Henry Mdimu akiongea na waandishi wa habari katika ofisi za gazeti la Mwananchi mjini Mwanza. Kutoka kushoto ni Salome Gregory, Henry Mdimu Mgaya, Issaya Mwakilasa na Zaytun Biboze.

Balozi Henry Mdimu akiongea na waandishi wa habari katika ofisi za gazeti la Mwananchi mjini Mwanza. Kutoka kushoto ni Salome Gregory, Henry Mdimu Mgaya, Issaya Mwakilasa na Zaytun Biboze.

Balozi Henry Mdimu wa IMETOSHA Foundation atoa wito kwa vyombo vya habari na jamii nchini kulichukua suala la ukatili na mauaji kwa watu wenye ualbino kama lao ili kuiondoa nchi yetu katika aibu hii.

Aliyasema hayo alipokuwa akiongea na waandishi wa habari katika ofisi za gazeti la Mwananchi ambao ni wadhamini wa habari wa ujio wa kamati ya Imetosha katika kanda ya ziwa.

Ndugu waandishi wa habari, Mwakilishi wa Tanzania
Bloggers Network, mabibi na mabwana…..
Tuko hapa kuueleza Ulimwengu kupitia vyombo mbali mbali
vya habari juu ya harakati yetu ya IMETOSHA. Harakati hii imeanzishwa na mimi mwenyewe, Henry Mdimu,
mwanahabari mwenzenu ambaye nimeamua kwa moyo mmoja kuwa Balozi wa kujitolea wa harakati za kukomesha mauaji dhidi ya watu wenye ulemavu wa ngozi, maarufu kwa jina la Albino.

Mimi na ujumbe wangu tumekuja Mwanza kutambulisha
harakati za IMETOSHA na ikiwa sehemu ya kuandaa shughuli zitakazofanyika kanda
ya Ziwa ikiwa ni sehemu ya kupambana na mauaji na unyanyasaji wa watu wenye
ulemavu wa ngozi. Mwezi ujao ujumbe wa IMETOSHA utakuja na kuweka kambi ya
kudumu Mwanza itakayozunguka kanda ya Ziwa na kutembelea nyumba kwa nyumba
zenye wahanga wa matukio ya mauaji na kutoa elimu kwa jamii kuwa mauaji ya watu
wenye ulemavu wa ngozi hayasababishi utajiri.

Pamoja na shughuli tutakazofanya tukiwa Kanda ya Ziwa
mwezi wa tano ni pamoja na matembezi ya hisani, kutakua na mpira kati ya Simba
na Yanga ambapo IMETOSHA itavalisha wachezaji Thisrts zake ikiwa ni sehemu ya
kutangaza harakati zetu. Pia tutakua na tamasha litakaloshirikisha wasanii
mbalimbali watakaotumbuiza nyimbo mbamimbali zitakazokua na ujumbe wa kukemea
na kupinga mauaji na manyanyaso dhidi ya watu wenye ulemavu wa ngozi.

Nimeamua kufanya hivi baada ya kushuhudia ndugu zangu
wakiteseka kwa muda mrefu. Awali nilishindwa kuanzisha harakati hizi nikiamini
kuna vyombo vinavyohusika na utetezi wa watu wenye ulemavu wa ngozi. Harakati hizi zimeanza baada ya kuona kadri muda
unavyokwenda matukio yamezidi kuongezeka na hali kuwa mbaya. Nashuhudia ndugu
zangu wakinyanyaswa, wakibezwa mtaani na hata kudhihakiwa huku baadhi ya
wanaoshuhudia haya wakicheka tu.

Kwa mujibu wa takwimu zilizotolewa na vyombo vya habari
vilimkariri Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt Jakaya Kikwete
akisema kesi mbili za mauaji ya watu wenye ulemavuwa ngozi zililipotiwa kwa
mwaka 2012 na 2013. Taarifa hizo ziliongeza kuwa kati ya mwaka 2006 na 2015,
watuhumiwa 139 wameshikiliwa na kesi 35 zimeandikishwa. Watuhumiwa 73
waliachiwa huru na wengine 15 wamekutwa na makosa.
Hivyo nimeamua niweke jitihada zangu binafsi niisaidie
Serikali yangu katika kuondoa doa hili linaloichafua Nchi yetu yenye sifa ya Amani dunia nzima. Hivyo
nawaomba Watanzania wenzangu mniunge mkono tukishirikiana na Serikali ili
mauaji haya yakome. Kutokana na ushawishi nilionao kama Mwandishi, Mtangazaji
wa redio na Blogger naamini nitaleta mabadiliko makubwa katika kuhakikisha haki
ya kusihi kwa ndugu zangu inaheshimiwa na kubaki historia. Salamu zangu
ziwafikie wanyanyasaji, wauaji na wenye kufanya dhihaka kwa watu wenye ulemavu
wa ngozi kuwa IMETOSHA.

Uchunguzi wangu wa awali umebaini ukosefu wa elimu juu
ya watu wenye ulemavu wa ngozi hupelekea tatizo hili kukua na hatimaye kuuana
kwa imani za kishirikina. Hivyo basi, silaha ya Elimu ni sehemu kubwa ya harakati
hizi. Mimi pamoja na mafariki zangu wanaoniunga mkono
tutakwenda Kanda ya Ziwa kutoa Elimu kabla tatizo hili halijaenea Nchi nzima.
Swali moja tujiulize kwa nini Kanda ya Ziwa? Tutatoa Elimu kwa njia ya ushauri
nasaha, pia wanamuziki na sanaa.

Nina mpango wa kwenda kanda ya Ziwa kuhangaika na hili
mpaka nione mwisho wake. Na ni rahisi kumaliza hili tatizo kabla halijaenea
nchi nzima. Maana Walemavu wa ngozi wako nchi nzima lakini jiulize kwa nini
Kanda ya Ziwa tu?
Mimi pamoja na rafiki zangu hawa, tunatoka kuelekea huko
kutoa elimu kwa njia ya sanaa, na washauri nasaha. Pia tutakua na team ya
wanamuziki wanaoandaa nyimbo mbali mbali za kutoa mafunzo ya kutokomeza ukatili
huu.
Wasanii hao ni pamoja na Jhikoman, Kassim Mganga, Profesa
J, Ray C, Fid Q, Roma Mkatoliki na Dani Msimamo. Tutaishi na jamii hii kwa muda tukiongea nao
kwa lugha yao kwa kutumia wakalimani kwa wsifahamu Kiswahili kuwashawishi
waamini hakuna ukweli katika Imani hizo.
Naamini nguvu ya vyombo vya Habari hivyo naomba
ushirikaiano wenu katika kuhakikisha tunatokomeza mauaji ya wenzetu ili mwisho
wa siku wanunuzi wa viungo vya watu wenye ulemavu wa ngozi wafukuzwe watakaanza
kuuliza jinsi ya kufanya mauaji haya.
Harakati za IMETOSHA rasmi zimezinduliwa rasmi tarehe
3/3/2015.
Mungu atubariki.
Ahsanteni