Steven Galinoma afariki dunia!

Marehemu, Steven Galinoma

ALIYEKUWA Mbuge wa Jimbo la Kalenga, Steven Galinoma amefariki dunia leo mapema. Taarifa zaidi zinasema kuwa Galinoma amefariki dunia leo asubuhi mjini Iringa ndani ya gari akipelekwa hospitalini kutokea Kalenga ambako alikokuwa anaishi.

Marehemu Galinoma katika enzi za uhai wake amewahi kushika nafasi anuai, mbali na kuwa mtumishi wa Serikali. Aliwahi kuwa Katibu Mkuu Idara ya Ulinzi na Jeshi la kujenga taifa, Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa mbuga za wanyamapori, Mwenyekiti wa Bodi ya Mashirika ya Umma (SCOPO) na Katibu wa Tume ya Uchunguzi wa Viongozi.

Nafasi nyingine ni pamoja na kuwa Mbunge wa Jimbo la Kalenga, Iringa. Marehemu Galinoma alikuwa anaugua kwa muda mrefu na amewahi kupelekwa nchini India kwa matibabu ambapo alichukua muda wa wiki 6 kabla ya kupata nafuu kwa kiasi fulani na baadaye kuzidiwa tena.

Marehemu ameacha wajukuu kadhaa na watoto, miongoni mwa watoto wake ni wanamuziki Innocent na Buti Jiwe aka Enry Galinoma.
Taaritibu za mazishi zitatolewa hapo baadaye.
Mungu amlaze mahala pema peponi.

-The Ngoma Africa Band, www.ngoma-africa.com