StarTimes Waleta Chaneli Mpya Kunogesha Wateja…!

 Meneja wa Huduma kwa Wateja wa kampuni hiyo, Gaspa Ngowi akizungumza na wateja walipotembelea kitengo cha huduma kwa wateja wakati wa hafla fupi kuadhimisha wiki ya huduma kwa wateja. Katika kuadhimisha wiki hiyo StarTimes imezindua chaneli mpya tatu ambazo ni ST Bollywood Africa, ST Bollywood na FOX Life.

Meneja wa Huduma kwa Wateja wa kampuni hiyo, Gaspa Ngowi akizungumza na wateja walipotembelea kitengo cha huduma kwa wateja wakati wa hafla fupi kuadhimisha wiki ya huduma kwa wateja. Katika kuadhimisha wiki hiyo StarTimes imezindua chaneli mpya tatu ambazo ni ST Bollywood Africa, ST Bollywood na FOX Life.

 Meneja wa Ufundi wa StarTimes Tanzania, Yusuph Baracha (kushoto) akiwaelekeza wateja walipotembelea chumba cha kurushia matangazo ya chaneli mbalimbali zinazopatikana kupitia king’amuzi cha kampuni hiyo  wakati wa hafla fupi kuadhimisha wiki ya huduma kwa wateja. Katika kuadhimisha wiki hiyo StarTimes imezindua chaneli mpya tatu ambazo ni ST Bollywood Africa, ST Bollywood na FOX Life.
Na Dotto Mwaibale
 
KATIKA kuadhimisha wiki ya huduma kwa wateja inayosherehekewa duniani kote na makampuni na taasisi mbalimbali katika wiki ya kwanza ya mwezi Oktoba, StarTimes wamewaletea wateja wake chaneli mpya ambazo zitanogesha zaidi burudani.
 
Akizungumza wakati wa hafla fupi iliyofanyika katika ofisi za kampuni hiyo jijini Dar es Salaam leo, Mkurugenzi wa Uendeshaji wa StarTimes Tanzania, Carter Luoh amebainisha kuwa wanafanya jitihada za kutosha kuhakikisha mkoa yote nchini inafikiwa na huduma zake.
 
“StarTimes inajivunia kuwa kinara katika huduma za matangazo ya dijitali nchini ikiwa na wateja zaidi ya milioni moja nchi nzima. Mpaka hivi sasa tumekwishaifikia mikoa takribani 17 ambapo hivi karibuni tumezindua huduma zetu mkoani Kigoma na tukiwa mbioni kuzindua na Mtwara pia. 
 
Mbali na mikoa hiyo lengo kuu ni kuhakikisha kuwa nchi nzima inafikiwa na huduma zetu ambapo tutahakikisha tunasambaza maduka na ofisi zetu. Zote hizi ni jitihada za dhati ambazo kampuni iliahidi katika kuhakikisha kila nyumba ya mtanzania inafikiwa na huduma za matangazo ya dijitali. Hivyo basi tumekuwa tukijitahidi kukamilisha dhamira hiyo huduma na bidhaa zetu zinapatikana kwa bei nafuu ambayo hata mtanzania wa kipato cha chini anaweza kumudu.” Alisema Luoh
 
“StarTimes inajivunia kuwa na watoa huduma takribani 300 ambao wapo tayari kuwahudumia wateja muda wote kupitia nambari 0764 700 800. Mbali na watoa huduma hao pia kupitia ofisi zetu na za mawakala wetu wateja pia wanahudumiwa katika ubora ule ule katika mikoa yote tunayopatikana. Pia tunayohuduma ya baada ya mauzo ambapo tunao mafundi waliotapakaa katika mitaa mbalimbali ya jiji la Dar es Salaam kuwafuata wateja walipo. Hii yote inadhihirisha na kwa namna gani tunavyowajali wateja wetu.” Alihitimisha Mkurugenzi huyo wa Uendeshaji
 
Naye kwa upande wake Meneja wa Huduma kwa Wateja wa kampuni hiyo  Gaspa Ngowi ameongezea kuwa ndani ya mwezi huu wamewaletea wateja wao chaneli mpya ambazo ni ST Bollywood, ST Bolyywood Africa na FOX Life huku nyinginezo zikiwa njiani kuja rasmi.
 
“Wiki hii ni maalumu kwa wateja wetu hususani katika kuonyesha kuthamini mchango wao katika kuunga mkono huduma zetu. StarTimes inapenda kusherehekea wiki ya huduma kwa wateja kwa kuleta chaneli mpya katika ving’amuzi vyake ambazo ni ST Bollywood, ST Bolyywood Africa ambazo zinaonyesha filamu kali na mpya za kihindi huku kukiwa na chaguo kwa mtazamaji kuchagua lugha anayoipenda ikiwemo Kiswahili; na FOX Life ambayo yenyewe inaonyesha filamu na mfululizo wa tamthiliya za runinga.” Alisema  Ngowi
 
Meneja huyo wa Huduma kwa Wateja wa StarTimes alihitimisha kwa kusema kuwa, “Mbali  na chaneli mpya pia tumewaletea bidhaa za runinga na projekta ambazo ndani yake kuna ving’amuzi ambapo wanaweza kutazama chaneli na vipindi mbalimbali. Hivyo basi wateja wakae mkao wa kula ili kujipatia bidhaa hizi ziliunganishwa na mfumo wa dijitali moja kwa moja.”
 
Katika kusherehekea wiki hii ya huduma kwa wateja, StarTimes imeadhimisha kwa kuwakaribisha wateja kutembelea ofisi zake ili kujionea jinsi wanavyoendesha shughuli zao.
 
Wateja hao walipata pia fursa ya kutembelea kitengo cha huduma kwa wateja ambapo waliweza kuonana na kuzungumza moja kwa moja na watoa huduma hao, pamoja na chumba cha kurushia matangazo ya chaneli mbalimbali zinazopatikana ndani ya king’amuzi cha kampuni hiyo.