Wateja wakinunua ving’amuzi vya StarTimes kwa bei ya shilingi 22,000/- vilivyounganishwa na ofa ya kifurushi cha Mambo chenye chaneli za Sports Focus na World Football ili kujionea michuano ya Copa America moja kwa moja. Copa America imeanza Juni 4 mpaka Juni 26 mwaka huu ambapo inachezeka nchini Marekani na kushirikisha mataifa 16 ya Marekani ya Kusini na Kaskazini na kuonekana kupitia chaneli za Sports Focus na Worl Football.
Hapa wakipiga mpira.
Wateja wa StarTimes wakiwa na zawadi zao walizojishindia baada ya kununua ving’amuzi ili kujionea michuano ya kombe la Copa America. Copa America imeanza Juni 4 mpaka Juni 26 mwaka huu ambapo inachezeka nchini Marekani na kushirikisha mataifa 16 ya Marekani ya Kusini na Kaskazini na kuonekana kupitia chaneli za Sports Focus na Worl Football.
Na Dotto Mwaibale
MASHABIKI wa soka nchini kote wameanza kufurahia mechi za michuano ya kombe la Copa America ambayo inaonekana moja kwa moja kupitia ving’amuzi vya StarTimes kwenye chaneli zake za michezo za Sports Focus na World Football kuanzia Juni 4 mpaka Juni 26 mwaka huu inayopigwa nchini Marekani.
Akizungumza katika uzinduzi wa kuanza rasmi kwa michuanoo hiyo katika viwanja vya Posta, Kijitonyama jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki hii Meneja wa Mauzo wa StarTimes Tanzania, Bw. David Kisaka amebainisha kuwa Copa America imekwishaanza na tayari timu za Marekani na Colombi zimekwisha fungua pazia.
“Leo ninayo furaha kubwa kuwafahamisha wateja wetu na watanzania wapenda soka kwamba michuano ya Copa America inaonekana moja kwa moja kwenye ving’amuzi vyao vya StarTimes. Mechi zote za kombe hili 32 zitakazozikutanisha timu kutoka mataifa 16 kwenye viwanja 10 tofauti nchini Marekani zitaonekana kupitia chaneli zetu za michezo za Sports Focus na World Football. Anachotakiwa mteja ni kujiunga na malipo ya mwisho wa mwezi ya kuanzia shilingi 12,000/- na kuendelea na wasio na ving’amuzi vyetu watembelee viwanjani hapa au maduka, mawakala na ofisi zetu ili kununua kwa bei nafuu kabisa ya shilingi 22,000/- tu ikiwa na ofa ya kifurushi cha Mambo kwa mwezi mmoja.” Alisema Bw. Kisaka
Meneja huyo wa Mauzo alifafanua zaidi kuwa kutokana na tofauti ya muda baina yetu na nchi ya Marekani ambako michuano hiyo inafanyikia kwa mara ya kwanza tangu kuanza kwake miaka 100 iliyopita mechi hizo zitakuwa zikirudiwa kupitia chaneli hizo hizo kuanzia saa saba mchana.
“Kuna tofauti kubwa kati ya muda na hivyo kusababisha mechi nyingi kuanza usiku au alfajiri, mechi za mapema kabisa kwa muda wa kwetu zinaanza saa sita ya usiku. Kwa kulitambua hilo mechi hizo zitakuwa zikirudiwa mchana ili kila mtu aweze kushuhudia ni kitu gani kinaendelea. Na mpaka sasa tayari wenyeji Marekani wamekwisha fungua pazia kwa mechi yao ya kwanza ambayo wamepoteza kwa kufungwa magoli 2 – 0 dhidi ya Colombia. Msisimko ni mkubwa wa michuano hii kwani wachezaji nyota wote wa dunia kutoka bara la Amerika ya Kusini watakuwa uwanjani kuhakikisha kombe linarudi nyumbani. Wachezaji kama Lionel Messi, Luis Suarez, Kun Aguero, Gonzalo Higuan, Angel Di Maria, Edinson Cavani, James Rodriguez, Countinho na wengineo wengi.”
Bw. Kisaka alimalizia kwa kusema kuwa, “Ninapenda kuchukua fursa hii kuwasihi watanzania kulipia ving’amuzi vyao na kujiunga nasi. Falsafa ya StarTimes Tanzania ni kutaka kila mtanzania afurahie matangazo ya dijitali akiwa nyumbani kwake kwa bei nafuu na ndio maana gharama zetu ni nafuu. Dhamira yetu ni kuwapatia wateja huduma bora zenye uhakika. Tunafahamu watanzania wanapenda michezo hususani soka na tunajitahidi kila siku kuwaletea michezo mizuri zaidi kama safari hii Copa America, awali tumeonyesha ligi za Bundesliga na Seriea A pamoja na kombe la vilabu bingwa duniani (ICC). Hivyo basi tunawaomba wateja wetu waichangamkie hii fursa kwa kufurahia kile wakipendacho na StarTimes.”
Michuano ya Copa America ilianza mnamo mwaka 1916 na mwaka huu inatimiza miaka 100 tangu kuanzishwa kwake. Kwa mafanikio hayo waandaaji wameamua shamrashamra zake kufanyika nje ya ardhi ya bara la Amerika Kusini, yaani Marekani. Timu ya taifa ya Uruguay ndiyo inashikilia rekodi ya kutwaa ubingwa huo mara nyingi zaidi, mara 15 ikifuatiwa na Argentina mara 14 ambapo mara mwisho walichukua mwaka 1993, na kushika nafasi ya pili mara tatu mfululizo, safari hii tena wakiongozwa na mchezaji wao bora wa dunia mara tano, Lioneli Messi mastaa kibao, wanapewa nafasi kubwa zaidi ya kuibuka mabingwa.
Bingwa mtetezi wa michuano hiyo ni timu ya taifa ya Chile ambayo inaongozwa na nyota kama Alexis Sanchez (Arsenal), Arturo Vidal (Bayern Munich) na kipa Claudio Bravo (Barcelona) ambapo walichukua ubingwa mwaka jana kwa mikwaju ya penati dhidi ya Argentina.