Stars ya Tanzania Yala Kichapo Nyumbani, Yapigwa 4-2 na Ivory Coast

Kwa sasa ni mapumziko katika mechi ya kufuzu kucheza kombe la dunia mwakani nchini Brazil ambapo Ivory Coast wanaongoza kwa mabao matatu wakati Stars wakiwa na mabao mawili (Picha na GPL).

LICHA ya Taifa Stars ya Tanzania kupata goli la mapema zaidi katika mchezo wao wa mechi ya kufuzu kucheza kombe la dunia mwakani nchini Brazil na timu ya Taifa ya Ivory Coast leo jijini Dar es Salaam imejikuta ikipata dhahama baada ya kufungwa magoli 4-2.

Stars ndio walioadha kwa kuonesha walikuwa na uchu na mchezo huo kwani dakika chache tu baada ya kuanza kwa mchezo walijipatia bao la mapema. Kupatikana kwa bao hilo la mapema kuliwafanya Ivory Coast kuja juu na kusawazisha bao hilo kabla ya kuongeza lingine na lingine tena.

Hadi mwisho wa mchezo Ivory Coast 4 na Stars 2. Mabao ya Stars yamefungwa na Amri Kiemba pamoja na Thomas Ulimwengu.