Spurs Yashinda Nne Mtungi, Leicester City Wahaha

1

Klabu ya soka ya Tottenham wakicheza ugenini katika dimba la Brittania wameibuka na ushindi wa kishindo wa mabao 4-0 dhidi ya Stoke City.

Mshambuliaji mahiri wa kikosi cha Spurs Harry Kane alianza kuzifumania nyavu katika dakika ya tisa ya mchezo, kisha kiungo Delle Ali akaongeza bao la pili katika dakika ya 67 kipindi cha pili.

2
Katika dakika ya 71 Harry kane tena akawatungua Stoke City kabla ya Dele Ali kuhitimisha ushindi huo kwa bao la nne katika dakika ya 82.

Kwa ushindi huo Spurs wanafikisha alama 68 wakiwa wamecheza michezo 34, hivyo kupunguza pengo dhidi ya Vinara Leicester City kufikia alama 5,huku wakiwa wanalingana michezo waliyocheza.

msmo