Balozi wa Pakistan nchini Tanzania Tajammul Altaf (kushoto) na Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Anne Makinda (kulia) wakizungumzia masuala mbalimbali kuhusu uendelezaji na uimarishaji wa ushirikiano kati ya Tanzania na Pakistan katika Nyanja za elimu, Biashara, wataalam na ubadilishanaji wa uzoefu kuhusu shughuli za Bunge leo jijini Dar es Salaam.
Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Anne Makinda akitoa ufafanuzi kwa balozi wa Pakistan nchini Tanzania, Tajammul Altaf kuhusu Zawadi ya saa aliyomuandalia balozi huyo yenye kumbukumbu ya picha za historia za maspika wa Bunge waliopita toka mwaka 1953 mpaka sasa ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya miaka 50 ya uhuru. (Picha na Aron Msigwa – MAELEZO)