Spika Makinda azindua ripoti ya UN kuhusu haki za watoto

Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Anne Makinda akizindua ripoti ya dunia ya umoja wa mataifa kuhusu Haki za watoto nchini, idadi ya watu na masuala ya vijana akiwa ameungana na baadhi ya vijana kutoka mikoa mbalimbali nchini jana jijini Dar es Salaam.

Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Anne Makinda akimpongeza kijana Mohamed Kessy kutoka Mbeya mara baada ya kijana huyo kuwasilisha matamko mbalimbali ya watoto yakiwemo uboreshaji wa elimu, utoaji wa huduma za afya ya uzazi kwa jamii, elimu ya maambukizi ya VVU na Ukimwi, Masuala ya ulinzi na ukatili dhidi ya watoto pamoja na sheria zinazolinda na kutetea haki za watoto jana jijini Dar es Salaam.

Mwakilishi mkazi wa UNICEF nchini Tanzania, Dorothy Rozga akitoa ujumbe maalum wa shirika hilo jana jijini Dar es Salaam wakati wa uzinduzi wa ripoti ya dunia ya umoja wa mataifa kuhusu Haki, idadi ya watu na masuala ya vijana jana jijini Dar es Salaam.


Mwakilishi mkazi wa Umoja wa Mataifa nchini Tanzania Alberic Kacou akitoa ujumbe wa umoja wa mataifa kuhusu masuala mbalimbali yakiwemo ongezeko la idadi ya watu, masual ya wanawake na watoto jana wakati wa uzinduzi wa ripoti ya dunia ya umoja wa mataifa kuhusu Haki, idadi ya watu na masuala ya vijana leo jijini Dar es Salaam. (Picha zote na Aron Msigwa –MAELEZO)