BAJETI YA MWAKA 2016/17
Shabaha na Misingi ya Bajeti ya Mwaka 2016/17
29. Mheshimiwa Spika, kufuatia kukamilika kwa zoezi la
uchambuzi wa mwenendo wa viashiria vya uchumi jumla na maoteo
katika kipindi cha muda wa kati – financial programming, shabaha za
uchumi jumla katika kipindi cha mwaka 2016/17 ni kama ifuatavyo:-
(i) Pato Halisi la Taifa kukua kwa asilimia 7.2 mwaka 2016
kutoka 7.0 mwaka 2015;
(ii) Kuendelea kudhibiti mfumuko wa bei katika wigo wa
tarakimu moja kati ya asilimia 5.0 na asilimia 8.0 mwaka
2016;
(iii) Mapato ya ndani ikijumuisha mapato ya Halmashauri
kufikia asilimia 14.8 ya Pato la Taifa mwaka 2015/16, na
kuendelea kuongezeka kufikia asilimia 16.9 ya Pato la Taifa
mwaka 2016/17;
22
(iv) Mapato ya kodi kufikia asilimia 13.8 ya Pato la Taifa mwaka
2016/17 kutoka asilimia 12.6 ya Pato la Taifa mwaka
2015/16;
(v) Matumizi ya Serikali yanatarajiwa kuongezeka kutoka
asilimia 23.2 ya Pato la Taifa mwaka 2015/16 hadi asilimia
27.0 mwaka 2016/17;
(vi) Nakisi ya bajeti inakadiriwa kuwa asilimia 4.5 ya Pato la
Taifa mwaka 2016/17 kutoka makadirio ya bajeti ya
asilimia 4.2 mwaka 2015/16;
(vii) Nakisi katika urari wa malipo ya kawaida kuwa asilimia 7.9
ya Pato la Taifa mwaka 2015/16 na kupungua hadi asilimia
7.5 mwaka 2016/17; na
23
(viii) Kuwa na akiba ya fedha za kigeni kwa kiwango cha kukidhi
mahitaji ya uagizaji wa bidhaa na huduma kutoka nje kwa
kipindi kisichopungua miezi minne Juni 2017.
30. Mheshimiwa Spika, shabaha na malengo hayo yatafikiwa
kwa kutegemea misingi ya Bajeti ifuatayo:-
(i) Kuendelea kuwepo kwa amani, usalama, utulivu na utengamano
nchini, kikanda na duniani;
(ii) Utulivu wa bei za mafuta ya petroli katika soko la dunia;
(iii) Kuwepo kwa hali nzuri ya hewa nchini na katika nchi jirani;
(iv) Kuendelea kuimarika kwa viashiria vya uchumi jumla na
maendeleo ya jamii kama vile Pato la Taifa, biashara ya nje,
ujazi wa fedha, mapato, matumizi na huduma za jamii;
24
(v) Kuimarika kwa sera za fedha na za bajeti zitakazosaidia
kupunguza mfumuko wa bei na tofauti kati ya riba za amana na
za mikopo;
(vi) Kuendelea kuimarika na kutengemaa kwa uchumi wa dunia; na
(vii) Ushiriki wa sekta binafsi katika uchumi utaongezeka hususan
kwenye uwekezaji katika viwanda.
Sera za Mapato kwa mwaka 2016/17
31. Mheshimiwa Spika, Serikali ya awamu ya tano imedhamiria
kuongeza na kuimarisha ukusanyaji wa mapato ya ndani kwa
kuchukua hatua mbalimbali. Katika mwaka 2016/17, mapato ya
Serikali yanatarajiwa kuongezeka na hivyo kupunguza utegemezi wa
kibajeti kutoka kwa Washirika wa Maendeleo. Katika kufanikisha azma
hii, sera za mapato kwa mwaka 2016/17 zimejielekeza kwenye
maeneo yafuatayo:-
25
(i) Kusimamia kikamilifu matumizi ya vifaa na mifumo ya
kielektroniki katika ukusanyaji wa mapato ili kuongeza
ufanisi na kudhibiti upotevu wa mapato;
(ii) Kuendelea kupanua wigo wa walipa kodi ikiwa ni pamoja
na kurasimisha sekta isiyo rasmi ili iweze kuingia katika
mfumo wa kodi;
(iii) Kuimarisha ufuatiliaji wa mapato yanayokusanywa na
taasisi na mamlaka mbalimbali za serikali;
(iv) Kuendelea kuchukua hatua za kudhibiti na kupunguza
misamaha ya kodi isiyo na tija; na
(v) Kuendelea kuimarisha usimamizi na kufanya ukaguzi wa
mara kwa mara bandarini, kwenye viwanja vya ndege na
maeneo ya mipakani ili kuhakikisha kodi stahiki
zinakusanywa.
26
Misamaha ya Kodi
32. Mheshimiwa Spika, Serikali itaendelea kudhibiti utoaji wa
misamaha ya kodi kwa taasisi za kidini na wawekezaji ili kuhakikisha
inakuwa na tija kwa Taifa. Katika kutekeleza hili, Serikali itafanya
marekebisho ya sheria husika ili kuondoa matumizi mabaya ya
misamaha ya kodi. Marekebisho hayo yatawasilishwa katika muswada
wa Sheria ya Fedha wa mwaka 2016. Pamoja na mambo mengine,
marekebisho hayo yatalenga kuwataka wanufaikaji kulipa kodi kwa
bidhaa watakazoagiza na baadae kuwasilisha maombi ya kurejeshewa
kodi hiyo baada ya uhakiki kufanyika.
33. Mheshimiwa Spika, Serikali itaendelea kutangaza na kutoa
taarifa za wanufaika wa misamaha ya kodi kila robo ya mwaka ili
wadau waweze kufahamu sekta au taasisi iliyonufaika na misamaha
hiyo na maeneo ilikoelekezwa. Utaratibu huu utasaidia kudhibiti
wafanyabiashara, taasisi na makampuni yanayotumia vibaya
misamaha hiyo kwa kujinufaisha wao binafsi na watumishi wa umma
wasio waadilifu.
27
Mapato yasiyo ya Kodi
34. Mheshimiwa Spika, kuanzia mwaka 2016/17, usimamizi wa
ukusanyaji wa mapato yasiyo ya kodi ikiwa ni pamoja na kodi ya
majengo utakuwa chini ya Mamlaka ya Mapato Tanzania. Uamuzi wa
kuipatia TRA jukumu hili unatokana na uzoefu na mifumo ya
ukusanyaji wa mapato waliyonayo nchi nzima lakini pia mafanikio na
uzoefu wa nchi nyingine kama Ethiopia na Rwanda. Aidha, Serikali
itaendelea kusimamia kikamilifu matumizi ya vifaa na mifumo ya
kielektroniki katika ukusanyaji wa mapato yasiyo ya kodi ili kuongeza
ufanisi na kudhibiti upotevu wa mapato. Miongoni mwa makusanyo
yanayolengwa ni pamoja na: tozo, faini kama vile za mahakama na
usalama barabarani, ada, viingilio kwenye hifadhi za Taifa na viwanja
vya michezo pamoja na vibali vya kuvuna maliasili.
35. Mheshimiwa Spika, Serikali imekuwa na utaratibu wa
kuziruhusu baadhi ya taasisi za Serikali kutumia mfumo wa kubakiza
maduhuli – retention. Utaratibu huu umekuwa ukipunguza mapato
kwenye Mfuko Mkuu wa Serikali na kuzinufaisha taasisi chache. Hivyo,
kuanzia mwaka 2016/17, Serikali itafuta utaratibu huo. Uamuzi huu ni
28
kwa mujibu wa Sheria ya Bajeti Na. 11 ya mwaka 2015 kifungu 58 (a)
mpaka (c) ambayo inaelekeza mapato yote ya Serikali yakusanywe na
kuingizwa kwenye Mfuko Mkuu wa Serikali. Sambamba na matakwa
ya Sheria ya Bajeti, tathmini iliyofanyika kuhusu utaratibu wa
retention ilibaini kuwa:-
(i) Taasisi zinazohusika na utaratibu wa “retention” zimeacha
majukumu yao ya msingi na kuegemea zaidi kwenye
shughuli za ukusanyaji mapato. Mifano ni pamoja na
Wakala wa Misitu na Kitengo cha Usalama Barabarani cha
Jeshi la Polisi;
(ii) Baadhi ya taasisi zenye mfumo wa “retention” zinapata
fedha nyingi na kuonekana kujinufaisha zaidi wakati
Wizara, Idara na Taasisi zingine zinakabiliwa na uhaba wa
fedha. Hali hii imesababisha kuongezeka kwa maombi
kutoka taasisi nyingine kutaka kujiunga na utaratibu huu;
29
(iii) Taasisi zilizo kwenye mfumo wa “retention” bado zinalipwa
mishahara asilimia 100 kutoka kwenye mfuko mkuu wa
Serikali; na
(iv) Utaratibu huu wa “retention” umesababisha idara ambazo
awali zilikuwa zikichangia Mfuko Mkuu wa Serikali kupitia
maduhuli kutochangia na hivyo kupunguza mapato ya
Serikali.
36. Mheshimiwa Spika, kutokana na sababu hizo, kuanzia sasa
mapato yote yatakusanywa na kuwasilishwa kwenye Mfuko Mkuu wa
Serikali na kila fungu litapewa fedha kulingana na bajeti yake. Wizara
ya Fedha na Mipango kwa upande wake itahakikisha kwamba fedha
kutoka Mfuko Mkuu zinagawiwa kwa Mafungu mbalimbali bila
kuchelewa kulingana na mapato yaliyokusanywa.
30
Sera za Matumizi kwa Mwaka 2016/17
37. Mheshimiwa Spika, katika mwaka 2016/17, Serikali
itaendelea kusimamia nidhamu ya matumizi ya fedha za umma kwa
kuzingatia sheria, kanuni na taratibu pamoja na miongozo mbalimbali.
Lengo kuu ni kupunguza matumizi yasiyo ya lazima, kuziba mianya ya
uvujaji wa fedha za umma na kuelekeza kiasi kikubwa cha fedha
kwenye miradi ya maendeleo. Katika kutimiza azma hii, Serikali
itachukua hatua mbalimbali kama ifuatavyo:-
(i) Kuwianisha matumizi na mapato halisi yatakayopatikana
kwa kila mwezi ili kuepuka malimbikizo ya madai. Maafisa
Masuuli wanaagizwa kuzingatia maelekezo ikiwemo kuingia
miadi baada ya kupokea mgao wa fedha (exchequer) na
siyo kabla;
(ii) Kuhakikisa malipo kwa wazabuni na watoa huduma
yanafanyika kwa kuwasilisha Hati za Ununuzi – LPOs
zitokanazo na IFMS;
31
(iii) Kuwasilisha Bungeni marekebisho ya Sheria ya Ununuzi wa
Umma ili kuziba mianya ya upotevu wa fedha katika
ununuzi wa umma na kuhakikisha ununuzi unawiana na
thamani ya fedha itakayotumika;
(iv) Kudhibiti matumizi ya taasisi za Serikali yasiyo na tija na
kufanya tathmini ya gharama za uendeshaji ili kuchukua
hatua stahiki kwa maendeleo ya nchi;
(v) Kuendelea na zoezi la kuunganisha Halmashauri zote nchini
kwenye mfumo wa malipo ya kibenki ili kuongeza udhibiti
wa matumizi ya fedha za umma na kuhakikisha kwamba
malipo yanafika kwa wakati;
(vi) Kuhakikisha kuwa mashirika ya umma yaliyoundwa kwa
lengo la kujiendesha kibiashara yanajiendesha kwa faida
bila kutegemea ruzuku ya Serikali; na
32
(vii) Kuimarisha ufuatiliaji na tathmini ya matumizi ya fedha za
umma hususan katika miradi ya maendeleo.
Maeneo ya Vipaumbele
38. Mheshimiwa Spika, kama nilivyoeleza kwenye hotuba yangu
ya Hali ya Uchumi, Mpango wa Maendeleo wa Taifa wa mwaka
2016/17 una maeneo makuu manne (4) ya vipaumbele:- (i) Viwanda
vya Kukuza Uchumi na Ujenzi wa Msingi wa Uchumi wa Viwanda; (ii)
Kufungamanisha Maendeleo ya Uchumi na Rasilimali Watu; (iii)
Mazingira Wezeshi kwa Uendeshaji Biashara na Uwekezaji; na (iv)
Usimamizi wa Utekelezaji wa Mpango. Ili kufikia malengo hayo,
mikakati itakayotumika ni pamoja na: kuhamasisha wawekezaji na
sekta binafsi kuwekeza katika viwanda na maeneo mbalimbali nchini
hususan kupitia mfumo wa ubia baina ya serikali na sekta binafsi
(PPP); kuondoa vikwazo kwa kuimarisha mazingira ya uwekezaji na
kufanya biashara; na kuimarisha usimamizi, ufuatiliaji na tathmini ya
utekelezaji wa Mpango.
33
Kuongeza Uzalishaji Viwandani
39. Mheshimiwa Spika, kama nilivyoeleza hapo awali, kauli mbiu
ya Bajeti ya mwaka 2016/17 ni “kuongeza uzalishaji viwandani ili
kupanua fursa za ajira”. Katika kufikia azma hii, Serikali imelenga
kutekeleza mikakati mbalimbali itakayochochea uwekezaji katika
viwanda. Miongoni mwa mikakati hiyo ni pamoja na: kufanya uthamini
wa ardhi na mali na kulipa fidia kwa maeneo maalum ya uwekezaji
yaliyotengwa nchini; kugharamia tafiti za viwanda kupitia taasisi za
TIRDO, TEMDO, CAMARTEC na COSTECH; kuendeleza miundombinu
ya viwanda vidogo kupitia SIDO; kuanzisha kongane za viwanda
(industrial clusters); na kuwezesha upatikanaji wa teknolojia rahisi na
nafuu kwa ajili ya viwanda. Katika mwaka 2016/17, Serikali imetenga
fedha za maendeleo kiasi cha shilingi bilioni 50.9 katika fungu 44 na
fungu 46 ambazo pamoja na mambo mengine zitagharamia
utekelezaji wa maeneo niliyoainisha hapo juu.
40. Mheshimiwa Spika, kama alivyoelekeza Mhe. Rais wakati wa
hotuba ya ufunguzi wa Bunge lako Tukufu, Serikali itahakikisha
viwanda vilivyopo vinafanya kazi. Katika mwaka 2016/17, Serikali
34
itakamilisha tathmini ya viwanda vilivyobinafsishwa ili kuweka mikakati
ya namna bora ya kuviendeleza. Baadhi ya viwanda hivyo ni viwanda
vya nguo, viwanda vya mazao ya mifugo, viwanda vya kusindika
mazao yakiwemo mazao ya mpira, korosho, tumbaku, miwa na
mpunga. Katika kutekeleza jukumu hilo, fedha za maendeleo
zimetengwa katika Mafungu mbalimbali kwa ajili ya kuendeleza
mashamba; na kuimarisha uzalishaji wa mazao ya kilimo, na ya
mifugo. Pamoja na kuvutia uwekezaji wa sekta binafsi katika viwanda,
Serikali itachukua hatua stahiki dhidi ya wawekezaji waliokiuka
masharti ya mikataba ya mauzo ya viwanda walivyobinafsishiwa.
41. Mheshimiwa Spika, katika kuboresha mazingira ya
uwekezaji wa viwanda, Serikali imetenga fedha za kuboresha
miundombinu ya uwekezaji hususan ya umeme, maji, barabara,
bandari na reli. Aidha, Serikali imedhamiria kuondoa urasimu usio wa
lazima na kuharakisha utoaji wa maamuzi ili kuvutia uwekezaji wa
sekta binafsi katika viwanda. Vilevile, zipo hatua mahsusi za kodi
zinazopendekezwa katika Bajeti hii ambazo zina lengo la kushawishi
na kuhimiza uwekezaji wa sekta binafsi katika viwanda. Serikali pia
35
itaimarisha upatikanaji wa mikopo ya uendelezaji wa viwanda kupitia
Benki ya Rasilimali pamoja na taasisi nyingine za fedha.
42. Mheshimiwa Spika, Serikali kupitia balozi zetu na Diaspora,
itaimarisha diplomasia ya uchumi katika nchi mbalimbali hasa zile
zilizoendelea pamoja na nchi ambazo uchumi wake unakua kwa kasi,
ikiwemo Jamhuri ya Watu wa China, India, Korea Kusini, Afrika Kusini
na Brazil ili kushawishi wawekezaji kuja kuwekeza Tanzania na hivyo
kufanikisha azma ya Serikali ya kuwa na uchumi wa viwanda. Vilevile,
Serikali itaendelea kuimarisha mazingira ya uwekezaji nchini ambayo
yatahamasisha kampuni za kigeni zilizoko hapa nchini kuwa mabalozi
wetu na kuvutia kampuni nyingine za nje wanakotoka kuja kuwekeza
hapa nchini. Hivyo, kama nilivyoeleza awali, jukumu la kuboresha
mazingira ya uwekezaji litapewa kipaumbele katika Bajeti ya mwaka
2016/17.
HATUA ZA KUTATUA KERO ZA WANANCHI
43. Mheshimiwa Spika; bajeti hii itajikita kutatua kero katika
maeneo yaliyolalamikiwa na wananchi kama nilivyoeleza hapo awali.
36
Baadhi ya hatua za kibajeti na kiutawala zitakazochukuliwa ni kama
ifuatavyo:
Rushwa katika Utoaji wa Huduma
44. Mheshimiwa Spika, katika kukabiliana na suala la rushwa na
ufisadi, Serikali imetenga jumla ya shilingi bilioni 2.5 ili kuwezesha
uanzishwaji wa mahakama ya mafisadi. Aidha, Serikali imetenga jumla
ya shilingi bilioni 72.3 katika bajeti ya mwaka 2016/17 kwa ajili ya
shughuli mbalimbali za Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa
(TAKUKURU) ili kuiwezesha taasisi hii kutekeleza majukumu yake
kikamilifu. Vile vile katika bajeti ya mwaka 2016/17, Serikali imetenga
shilingi bilioni 44.7 kwa ajili ya kuiwezesha Ofisi ya Taifa ya Ukaguzi
kutekeleza majukumu yake ya msingi ya kukagua na kudhibiti
matumizi ya fedha za umma.
Hatua za Kuzuia Upotevu wa Mapato
45. Mheshimiwa Spika, Serikali itadhibiti upotevu wa mapato
kwa kuimarisha ufuatiliaji wa mara kwa mara katika maeneo
mbalimbali ya biashara, bandarini, viwanja vya ndege na mipakani;
37
kuwajengea uwezo watumishi ili waweze kufanya kaguzi za kitaalam
hasa katika sekta za madini, maliasili, ardhi, mafuta na gesi asilia;
kuhimiza matumizi ya mifumo ya kieletroniki katika kukusanya mapato
ya kodi na yasiyo ya kodi, pamoja na kupunguza misamaha ya kodi.
46. Mheshimiwa Spika, Serikali inawapongeza wafanyabiashara
walioitikia matakwa ya Sheria Ya Usimamizi wa Kodi ambayo inamtaka
kila mfanyabiashara isipokuwa wale ambao wametangazwa rasmi na
Kamishna wa Mamlaka ya Mapato kutotumia mashine za EFD kutoa
risiti kila anapouza bidhaa au huduma. Hata hivyo, kuna baadhi ya
wafanyabiashara ambao bado wanakaidi matakwa haya ya kutumia
mashine hizo. Napenda kuwasihi wafanyabiashara hao kuanza mara
moja kutumia mashine hizo vinginevyo watachukuliwa hatua kali za
kisheria ikiwa ni pamoja na kuwanyang’anya leseni zao za biashara na
hawataruhusiwa kufanya biashara hapa nchini kwa kipindi
kisichopungua miaka miwili. Aidha, kwa upande wa Serikali, ili kuwa
na usimamizi mzuri wa fedha za Serikali na kuhakikisha kwamba
zinatumika kama ilivyokusudiwa, kwa mamlaka niliyopewa chini ya
Sheria ya Fedha za Umma pamoja na kanuni zake malipo yote lazima
38
yaambatanishwe na ankara za madai au stakabadhi (tax invoice)
zilizotolewa na mashine za EFD. Kwa sababu hiyo kuanzia tarehe 1
Julai 2016, ni marufuku kwa Wizara, Taasisi, Wakala za Serikali, Mikoa
na Mamlaka za Serikali za Mitaa kufanya biashara na wazabuni na
wafanyabiashara wengine ambao hawatumii mashine za kielektroniki –
EFDs. Aidha, malipo yatakayofanywa bila stakabadhi au Ankara
zisizokuwa za mashine za EFD ni lazima ziambatanishwe na ushahidi
kuwa mfanyabishara husika ametangazwa rasmi na Kamishna wa
Mapato kutotumia mashine za EFD.
Hatua za Kudhibiti Matumizi
47. Mheshimiwa Spika, Serikali itaendelea kuchukua hatua za
kupunguza na kudhibiti matumizi bila kuathiri ubora wa huduma
zinazotolewa na hivyo kuhakikisha uwepo wa ufanisi katika matumizi
ya Serikali. Baadhi ya hatua hizo zimeainishwa katika Mwongozo wa
kutayarisha Mpango na Bajeti ya mwaka 2016/17 niliouwasilisha hapa
Bungeni Februari, 2016. Miongoni mwa hatua hizo ni pamoja na:
39
(i) Kuhakikisha mikutano yote ikiwa ni pamoja na mikutano ya
bodi, mafunzo na semina inatumia kumbi za Serikali na
Taasisi za Umma;
(ii) Kutoa kipaumbele kwa Taasisi za Umma katika kutoa
huduma kwa Serikali kama vile bima, usafirishaji wa barua,
mizigo na vifurushi, matangazo na usafiri;
(iii) Kudhibiti matumizi ya umeme, simu na maji ikiwa ni
pamoja na kufanya ukaguzi wa mara kwa mara;
(iv) Kudhibiti ulipaji wa mishahara kwa watumishi ili kuepuka
malipo yasiyostahili. Aidha, Serikali itaendelea kufanya
sensa ya watumishi wote;
(v) Kudhibiti utoaji wa mikopo ya elimu ya juu ili kuepuka
utoaji wa mikopo kwa wanafunzi wasio stahili;
40
(vi) Kuendelea kufanya ununuzi wa magari kwa pamoja na
bidhaa moja kwa moja kutoka kwa wazalishaji ili kupata
unafuu wa bei;
(vii) Kuendelea kudhibiti gharama za uendeshaji wa magari
ikiwa ni pamoja na matengenezo, mafuta na vilainishi;
(viii) Kupunguza na kuondoa matumizi yasiyo na tija katika
maeneo mbalimbali ikiwemo maadhimisho na sherehe za
kitaifa, matamasha, machapisho na safari za ndani na nje
ya nchi zisizo na tija;
(ix) Kuhimiza matumizi ya nakala laini (soft copy) za
machapisho mbalimbali hususan yanayozidi kurasa 50 ili
kupunguza gharama za uchapishaji na kutunza mazingira;
na
41
(x) Kudhibiti matumizi ya Taasisi na Mashirika ya Umma
yasiyowiana na majukumu yao ya msingi na yasiyo na tija.
Kero katika Sekta ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi
48. Mheshimiwa Spika, azma kuu ya Serikali ni kuimarisha sekta
ya kilimo, mifugo na uvuvi kwa mtazamo wa kibiashara, kukuza
viwanda na kuongeza thamani ya mazao yatokanayo na sekta hii.
Hata hivyo, bado sekta hii inakabiliwa na changamoto kadhaa
zikiwemo kodi na tozo za mazao zisizo na tija, uhaba wa pembejeo,
vifaa duni, masoko, na uhaba wa maafisa ugani.
49. Mheshimiwa Spika, katika kukabiliana na changamoto hizo,
Serikali imetenga jumla ya shilingi trilioni 1.56 sawa na asilimia 4.9 ya
bajeti yote ukiondoa deni la Taifa kwa ajili ya kugharamia shughuli
mbalimbali katika sekta ya kilimo, uvuvi na ufugaji zikiwemo ununuzi
wa pembejeo; kuboresha upatikanaji wa masoko; kuongeza
upatikanaji wa zana bora na za kisasa za kilimo, ufugaji na uvuvi; na
kuongeza maafisa ugani.
42
50. Mheshimiwa Spika, Serikali imedhamiria kupunguza ama
kuondoa kabisa ushuru na kodi mbalimbali za mazao ya kilimo, mifugo
na uvuvi zisizo na tija. Nitaeleza hatua mahsusi muda mfupi ujao.
Aidha, Benki ya Maendeleo ya Kilimo Tanzania itaendelea kutoa
mikopo ya riba nafuu na masharti yanayozingatia hali halisi ya sekta
ya kilimo ili kusaidia kuleta mapinduzi ya kilimo kutoka kilimo cha
kijungujiko (subsistence farming) kwenda kilimo cha kibiashara. Katika
mwaka 2016/17, Benki ya Kilimo itaendelea kutangaza na kupanua
huduma zake kwa wananchi mikoani.
Migogoro ya Ardhi
51. Mheshimiwa Spika, Serikali itaendelea na juhudi za kutatua
migogoro katika Sekta ya ardhi ikiwemo migogoro kati ya wakulima na
wafugaji, vijiji na hifadhi, wananchi na wawekezaji, uvunjaji wa sheria
za ardhi na umiliki wa mashamba pori. Katika kukabiliana na migogoro
hiyo, Serikali imetenga shilingi bilioni bilioni 5.0 kwa ajili ya Mfuko wa
Fidia ya Ardhi; shilingi bilioni 13.0 kwa ajili ya utekelezaji wa mradi wa
umilikishwaji wa ardhi; na shilingi bilioni 8.8 kwa ajili ya ununuzi wa
vifaa vya upimaji wa ardhi. Aidha, Serikali imetenga shilingi bilioni
43
33.4 kwa ajili ya programu ya kuwezesha umilikishaji wa ardhi na
uwekaji wa kumbukumbu utakaotekelezwa kwa kipindi cha miaka
mitatu. Vilevile, Serikali itaendelea kusajili migogoro ya ardhi katika
maeneo mbalimbali nchini na kutafuta ufumbuzi kulingana na
mazingira ya eneo husika ili kupunguza migogoro baina ya watumiaji
mbalimbali wa ardhi.
Huduma zisizoridhisha za Usafiri na Usafirishaji
52. Mheshimiwa Spika, Serikali itaendelea kukabiliana na kero
zinazotokana na uchakavu wa miundombinu ya reli, barabara, bandari
na viwanja vya ndege. Katika mwaka 2016/17, Serikali imetenga
shilingi trilioni 5.47 sawa na asilimia 25.4 ya bajeti yote ukiondoa Deni
la Taifa, kwa ajili ya miradi ya ujenzi na uchukuzi. Baadhi ya maeneo
yanayohusika ni;
(i) Ujenzi wa miundombinu ya barabara – kiasi cha shilingi
trilioni 2.18 kimetengwa kwa ajili ya ujenzi wa barabara
hasa zenye kufungua fursa za kiuchumi na kukarabati
barabara zilizopo.
44
(ii) Uchukuzi – kiasi cha shilingi trilioni 2.49 kimetengwa kwa
ajili ya kuanza kujenga reli ya kati kwa kiwango cha
standard gauge; ununuzi wa ndege mpya tatu za abiria;
ununuzi wa meli mpya ziwa Viktoria; ukarabati wa meli
katika ziwa Viktoria na ziwa Tanganyika; uboreshaji wa
miundombinu ya bandari; na ujenzi na ukarabati wa
viwanja vya ndege. Aidha, Kiasi cha shilingi bilioni 161.4
kimetengwa katika Mfuko wa Reli kwa ajili ya ununuzi wa
mabehewa na vichwa vya treni pamoja na ukarabati wa na
Reli.
Umeme
53. Mheshimiwa Spika, Serikali imetenga jumla ya shilingi trilioni
1.13 sawa na asilimia 5.3 ya bajeti yote bila kujumuisha Deni la Taifa
ili kugharamia upatikanaji wa umeme wa uhakika kwa ajili ya
matumizi ya majumbani na viwandani. Baadhi ya miradi
itakayotekelezwa ni pamoja na: kuongeza kasi ya usambazaji umeme
vijijini kupitia REA na kukamilisha miradi ya umeme inayoendelea
45
ikiwemo kuongeza mitambo mingine yenye uwezo wa kufua MW 185
katika mradi wa Kinyerezi – I na Kinyerezi II. Serikali itahakikisha
kuwa Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) linakuwa na uwezo
kifedha ili lijiendeshe lenyewe na kuwa na ushindani katika uzalishaji
wa umeme kwa kutumia vyanzo nafuu ili kupunguza gharama kwa
wazalishaji na walaji.
Upatikanaji duni wa huduma za afya, maji na elimu.
54. Mheshimiwa Spika, kuna changamoto nyingi katika maeneo
haya, ikiwemo kukosekana kwa upatikanaji wa uhakika wa maji safi
na salama kwa ajili ya matumizi ya majumbani na viwandani; na
huduma bora za afya. Aidha, kuna changamoto za ubora wa elimu na
upatikanaji wa mikopo kwa wanafunzi wa elimu ya juu kwa wakati.
Bajeti ya mwaka 2016/17 imejielekeza katika kutatua changamoto
hizo kama ifuatavyo:
Elimu
55. Mheshimiwa Spika, sekta ya elimu imetengewa jumla ya
shilingi trilioni 4.77 sawa na asilimia 22.1 ya bajeti yote bila
46
kujumuisha Deni la Taifa. Fedha hizi zimetengwa kwa ajili ya
kugharamia shughuli mbalimbali za elimu zikiwemo: Elimu Msingi bila
malipo; gharama za uendeshaji wa shule ikiwemo chakula, ununuzi
wa vitabu, na mitihani; mikopo na ruzuku kwa wanafunzi wa elimu ya
juu; na ujenzi na ukarabati wa miundombinu ya elimu katika ngazi
zote
Afya
56. Mheshimiwa Spika, kwa kutambua umuhimu wa huduma
bora za afya kwa wananchi, Serikali imetenga jumla ya shilingi trilioni
1.99 sawa na asilimia 9.2 ya bajeti yote bila kujumuisha Deni la Taifa
kwa ajili ya sekta ya afya. Baadhi ya maeneo yanayohusika ni pamoja
na ununuzi wa dawa, vifaa tiba na vitendanishi (reagents) ambayo
yametengewa shilingi bilioni 180.5; ulipaji wa deni la Bohari Kuu ya
Dawa (MSD) shilingi bilioni 71.0; na uboreshaji wa miundombinu ya
kutolea huduma za afya katika ngazi zote.
Maji
57. Mheshimiwa Spika, Serikali imetenga kiasi cha shilingi
trilioni 1.02 sawa na asilimia 4.8 ya bajeti yote bila kujumuisha Deni la
47
Taifa, kwa ajili ya kuongeza upatikanaji wa maji safi na salama nchini.
Baadhi ya shughuli zitakazotekelezwa ni pamoja na: ujenzi na
ukarabati wa miundombinu ya maji mijini na vijijini; ulipaji wa madeni
ya wakandarasi na utekelezaji wa shughuli za Mfuko wa Maji.
Mazingira Wezeshi kwa Sekta Binafsi
58. Mheshimiwa Spika, kama nilivyoeleza hapo juu, katika bajeti
ya 2016/17 Serikali imedhamiria kuboresha mazingira ya kufanya
biashara, ikiwa ni pamoja na kuwekeza kwenye miundombinu ya reli,
barabara, bandari, maji na kuhakikisha upatikanaji wa umeme wa
uhakika ili kuvutia sekta binafsi kuwekeza katika maeneo mbalimbali.
Aidha, Serikali itaendelea kupitia kodi, tozo na ada mbalimbali ili
kuzipunguza au kuziondoa zile ambazo zinalalamikiwa na wananchi na
wawekezaji wa ndani na nje. Miongoni mwa jitihada zitakazochukuliwa
na Serikali ili kuongeza ushiriki wa sekta binafsi katika uchumi ni
pamoja na kuboresha huduma za upatikanaji wa mikopo kwa sekta
binafsi, kuimarisha soko la mitaji, kukuza utaratibu wa ubia kati ya
sekta ya umma na sekta binafsi – PPP, na kuboresha mazingira ya
kufanya biashara kwa kuboresha miundombinu ya umeme,
48
usafirishaji, maji, usambazaji wa gesi asilia, mfumo wa kodi, kuweka
vivutio mbalimbali, kuondoa urasimu usio wa lazima na kupambana na
rushwa.
Uwezeshaji kiuchumi wa Makundi Maalum
(i) Maendeleo Vijijini
59. Mheshimiwa Spika, Serikali ya Awamu ya Tano imeazimia
kuwezesha wananchi kiuchumi ikiwa ni sehemu ya utekelezaji wa Ilani
ya Uchaguzi ya CCM ya mwaka 2015 ambapo shilingi milioni 50
ziliahidiwa kwa kila kijiji ili kuwawezesha wananchi kuanzisha na
kuendeleza shughuli za uzalishaji kupitia Ushirika wa Kuweka na
Kukopa (SACCOS) na vikundi vingine vya kiuchumi. Katika kutekeleza
ahadi hii, Serikali imetenga shilingi bilioni 59 kwa ajili ya utekelezaji
wa mpango huu kwa awamu. Mpango huu utaanza kutekelezwa chini
ya Ofisi ya Waziri Mkuu mara baada ya kukamilisha utaratibu wa
matumizi ya fedha hizo ili kuhakikisha kuwa fedha hizi zinatumika
ipasavyo.
49
(ii)Vijana, Wazee, Wenye Ulemavu, Wanawake na Watoto
60. Mheshimiwa Spika, Bajeti ya 2016/17 imezingatia mahitaji
ya makundi maalum ya vijana, wazee, wenye ulemavu, wanawake na
watoto wanaoishi katika mazingira hatarishi. Katika mwaka 2016/17
Serikali imetenga shilingi bilioni 2.4 kwa ajili ya uboreshaji wa
miundombinu ya makazi ya wazee na mahabusu za watoto; na
chakula, dawa na mahitaji mengine ya watoto walio katika mazingira
hatarishi. Katika mwaka wa fedha 2016/17, Serikali imetenga asilimia
5.0 ya mapato ya ndani ya kila Halmashauri kwa ajili ya vijana. Aidha,
shilingi bilioni 1.0 zimetengwa chini ya Fungu 65 (Ofisi ya Waziri
Mkuu, Kazi, Ajira, Vijana na wenye Ulemavu, kifungu cha 2032 mradi
namba 4945) kwa ajili ya kuendeleza vijana. Vilevile, shilingi bilioni 5.0
zimetengwa Fungu 65, kifungu cha 2002 mradi namba 6581 kwa ajili
ya kuendeleza ujuzi kwa vijana ambao hawana ajira na walio kwenye
soko la ajira.
61. Mheshimiwa Spika, katika bajeti ya 2016/17, Serikali
imetenga asilimia 5.0 ya mapato ya ndani ya kila Halmashauri kwa ajili
50
ya kuwezesha vikundi vya maendeleo ya wanawake katika
Halmashauri husika. Vilevile, Serikali imetenga shilingi bilioni 1.95 kwa
ajili ya uwezeshaji wa wanawake kiuchumi chini ya Fungu 53 (Wizara
ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, kifungu cha
3001 mradi namba 4950). Kuhusu watu wenye ulemavu, Serikali
itaendelea kuhakikisha kuwa vifaa vilivyotengenezwa mahsusi kwa ajili
yao vinasamehewa kodi ili viweze kupatikana kwa bei nafuu. Aidha,
Serikali itaendelea kuboresha shule maalum za watoto wenye ulemavu
na kugharamia mahitaji yao ili kuwajengea mazingira mazuri zaidi ya
kujifunzia.
(iii) Wasanii, Wabunifu na Wanamichezo
62. Mheshimiwa Spika, katika mwaka 2016/17 Serikali kupitia
Fungu 96 imetenga jumla ya shilingi bilioni 3.0 kwa ajili ya kutekeleza
miradi mbalimbali ya sanaa, ubunifu, utamaduni na michezo ikiwa ni
pamoja na: kuratibu na kusimamia uanzishwaji wa Mfuko wa
Maendeleo ya Sanaa na Ubunifu; kusimamia urasimishaji wa shughuli
za Sanaa; kusimamia na kudhibiti filamu zitakazoingia sokoni bila
kufuata taratibu; na kuratibu uendeshaji wa kazi za sanaa nchini.
51
(iv) Wachimbaji Wadogo wa Madini
63. Mheshimiwa Spika, Serikali ya awamu ya tano imedhamiria
kuwezesha wachimbaji wadogo wa madini ili kuongeza tija na ufanisi
katika shughuli zao na hivyo kuongeza ajira, kukuza kipato cha
wachimbaji na wananchi wanaozunguka maeneo ya uchimbaji madini.
Katika mwaka 2016/17 Serikali inakusudia kutekeleza yafuatayo:
kuwapatia ruzuku; kuwapatia mafunzo; kuwatengea maeneo maalum
ya uchimbaji; kuimarisha soko; pamoja na kuziwezesha taasisi
zinazohusika na ukaguzi wa usalama wa migodi ili kupunguza ajali
zinazoweza kuepukika. Kiasi cha fedha kilichotengwa kwa madhumuni
haya katika bajeti ya 2016/17 ni shilingi milioni 900 kwa ajili ya ruzuku
ya wachimbaji wadogo.
(v)Wafanyakazi
64. Mheshimiwa Spika, ili kuboresha kipato cha wafanyakazi,
siku ya Mei Mosi Mheshimiwa Dkt. John Pombe Joseph Magufuli, Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, aliagiza kiwango cha kodi ya
mapato kwenye mishahara (PAYE) kipunguzwe kutoka asilimia 11 hadi
52
asilimia 9 ili kupunguza makali ya maisha kwa wafanyakazi. Agizo hilo
litaanza kutekelezwa Julai Mosi 2016. Aidha, kuanzia mwaka ujao wa
fedha Serikali itaanza kuwasilisha mchango wa mwajiri wa asilimia 0.5
ya mshahara kwenye Mfuko wa Fidia kwa wafanyakazi ili watumishi
wa umma wapatapo ajali mahali pa kazi waweze kulipwa na Mfuko.
Kadhalika, Serikali itaendelea kuboresha mazingira ya kuwezesha
watumishi wake kujenga ama kununua nyumba kupitia Bodi ya Mfuko
wa Mikopo ya Nyumba kwa Watumishi wa Serikali, pamoja na
Watumishi Housing Company.
(vi) Vyombo vya Ulinzi na Usalama
65. Mheshimiwa Spika, Serikali inavipongeza vyombo vya ulinzi na
usalama kwa kujipambanua kwa nidhamu ya hali ya juu katika kazi zao.
Hata hivyo, Serikali inawaelekeza Maafisa Masuuli wa Mafungu husika
kujipambanua vivyo hivyo kwa nidhamu kama hiyo katika matumizi ya
fedha na mali za umma. Aidha, katika mwaka 2016/17, utaratibu wa
kutoa misamaha ya kodi kwenye maduka ya vyombo vya ulinzi na
usalama utasitishwa na nitaeleza utaratibu mpya baadaye. Kadhalika,
53
Serikali itaendelea kujenga nyumba za makazi kwa askari ili kukabiliana
na uhaba wa makazi kwa askari nchini.
IV. MABORESHO YAMFUMO WA KODI, ADA, TOZO NA HATUA
NYINGINE ZA MAPATO
66. Mheshimiwa Spika, napenda kuwasilisha sasa mapendekezo ya
hatua mpya za kufanya marekebisho ya mfumo wa kodi, ikiwemo
kurekebisha baadhi ya viwango vya kodi, tozo na ada chini ya Sheria
mbalimbali na kuboresha taratibu za ukusanyaji na usimamizi wa mapato
ya Serikali. Aidha, marekebisho haya yanalenga pamoja na mambo
mengine, kuongeza mapato ya Serikali na kuchochea ukuaji wa uchumi
hususan katika sekta ya viwanda, kilimo, usafirishaji na kukuza ajira.
Marekebisho hayo yanahusu Sheria zifuatazo:-
a. Sheria ya Kodi ya Ongezeko la Thamani, SURA 148;
b. Sheria ya Ushuru wa Bidhaa, SURA 147;
c. Sheria ya Kodi ya Mapato, SURA 332;
d. Sheria ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi Stadi, SURA 82;
54
e. Sheria ya Magari (Kodi ya Usajili na Uhamisho wa Umiliki),
SURA 124;
f. Sheria ya Mamlaka ya Mapato Tanzania, SURA 399
(sambamba na Sheria ya kodi ya Majengo ya Mamlaka ya
Miji, SURA 289; Sheria ya Fedha za Umma ya Serikali za
Mitaa, SURA 290; Sheria ya Utawala wa Kodi ya mwaka
2015; na Sheria ya Rufani za Kodi, SURA 408);
g. Sheria ya Msajili wa Hazina (Mamlaka na Majukumu), SURA
370;
h. Sheria ya Forodha ya Jumuiya ya Afrika Mashariki, ya
mwaka 200;
i. Marekebisho madogo madogo katika baadhi ya Sheria za
Kodi na Sheria nyingine mbalimbali; na
j. Marekebisho ya Ada na Tozo Mbalimbali zinazotozwa na
Wizara, Mikoa na Idara zinazojitegemea;
a) Sheria ya Kodi ya Ongezeko la Thamani, SURA 148
67. Mheshimiwa Spika, napendekeza kufanya marekebisho
kwenye Sheria ya Kodi ya Ongezeko la Thamani kama ifuatavyo: –
55
(i) Kusamehe Kodi ya Ongezeko la Thamani kwenye maharage
ya soya baada ya kubaini kuwa, mazao haya yalisahaulika
kuingizwa kwenye orodha chini ya kifungu cha 3 cha
jedwali la misamaha linalojumuisha mifugo, mazao ya
kilimo ambayo hayajasindikwa na chakula cha binadamu;
(ii) Kusamehe Kodi ya Ongezeko la Thamani kwenye
mbogamboga zote na mazao ya mifugo yakiwa
hayajasindikwa kama yanavyoonekana kwenye Ushuru wa
Pamoja wa Jumuiya ya Afrika Mashariki, sura ya 2 na 3
(mazao ya mifugo yasiyosindikwa), sura ya 7 (matunda na
karanga), sura ya 8 (nafaka), sura ya 10 (unga wa nafaka)
na sura ya 11 (mbegu za mazao). Hatua hii inakusudia
kutoa msamaha wa kodi ya VAT kwenye mazao ya chakula
ambayo hayajasindikwa ili kuwezesha upatikanaji wa lishe
bora ya msingi kwa gharama nafuu;
(iii) Kuongeza vitamini na virutubishi kwenye orodha ya vifaa
na madawa muhimu yaliyoidhinishwa na Waziri wa Afya,
56
Ustawi wa Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto kwa ajili ya
kupata msamaha wa kodi. Vitamini na virutubishi hivyo
huongezwa kwenye vyakula ili kuboresha lishe kama njia
mojawapo ya kuimarisha afya ya jamii;
(iv) Kuongeza madawa ya kutibu maji yanayotumiwa na
binadamu kwenye orodha ya vifaa na madawa muhimu
yaliyoidhinishwa na Waziri wa Afya, Ustawi wa Jamii, Jinsia,
Wazee na Watoto kwa ajili ya kupata msamaha wa Kodi ya
Ongezeko la Thamani. Madawa haya ni muhimu kwa ajili
ya kulinda afya ya msingi kwa kutumia maji salama. Waziri
wa Maji na Umwagiliaji atatakiwa kuwasilisha orodha ya
madawa hayo kwa Waziri wa Afya, Ustawi wa Jamii, Jinsia,
Wazee na Watoto ili ayajumuishe kwenye orodha hiyo;
(v) Kutoza Kodi ya Ongezeko la Thamani kwenye huduma za
utalii hususan kuongoza watalii, kuendesha watalii, utalii
wa majini, kuangalia wanyama na ndege wa porini,
kutembelea hifadhi na usafirishaji wa watalii ardhini. Hatua
57
hii inachukuliwa kama ilivyokusudiwa wakati wa kutunga
Sheria mpya ya Kodi ya Ongezeko la Thamani, ambayo
ilianza kutumika rasmi Julai 2015, lakini kwa kutambua
mikataba iliyokuwepo wakati huo kati ya watoa huduma za
utalii na watalii waliokuwa wanatarajia kuja nchini,
ilikubalika kusubiri kukamilika kwa makubaliano hayo kwa
mwaka unaomalizika. Huduma hizi pia hutozwa Kodi ya
Ongezeko la Thamani kwenye nchi nyingine kama vile
Kenya, Rwanda na Afrika ya Kusini;
(vi) Bidhaa zinazotengezwa Tanzania Bara na kuuzwa Zanzibar
zitatozwa Kodi ya Ongezeko la Thamani upande wa
Zanzibar, na bidhaa zinazotengezwa Zanzibar na kuuzwa
Tanzania Bara zitatozwa kodi hiyo upande wa Tanzania
Bara. Lengo la hatua hii ni kuondoa utaratibu uliokuwepo
hapo awali wa kufanya marejesho ya Kodi ya Ongezeko la
Thamani kwenda Zanzibar kwa kuwa Sheria ya Kodi hiyo
inayotumika sasa haina kifungu kinachoruhusu marejesho
ya Kodi ya Ongezeko la Thamani kwenda Zanzibar kama
58
ilivyokuwa kwenye sheria iliyofutwa. Kwa kuwa kila upande
wa Muungano una Sheria yake ya Kodi ya Ongezeko la
Thamani, kodi hii itatozwa sehemu ambako bidhaa au
huduma itatumika, yaani “destination principle”. Kwa
msingi huo muhimu katika utozaji Kodi ya Ongezeko la
Thamani, Serikali ya Mapinduzi Zanzibar itakuwa
inakusanya kodi hii kwa bidhaa zinazozalishwa Tanzania
Bara na kupelekwa Zanzibar. Vile vile, Tanzania Bara
itakuwa inakusanya kodi hii kwa bidhaa zinazozalishwa
Zanzibar na kuletwa Tanzania Bara;
(vii) Kufanya marekebisho katika orodha ya misamaha ya
bidhaa za petroli chini ya kifungu cha 15 cha Jedwali la
misamaha la Sheria ya Kodi ya Ongezeko la Thamani ya
mwaka 2014 ili kujumuisha pia bidhaa za lami zenye HS
Code 27.13, 27.14 na 27.15 ambazo hazikujumuishwa
katika Jedwali hilo;
59
(viii) Kusamehe Kodi ya Ongezeko la Thamani kwenye bima ya
vyombo vya usafiri wa anga vinavyotambulika katika HS
Code 88.01 na Hs Code 88.02. Hatua hii inapendekezwa
kwa kuzingatia kuwa sekta ya usafirishaji wa anga bado ni
changa kuweza kuhimili ulipaji wa bima kwa vyombo hivyo
vya usafiri. Hivyo kuna umuhimu wa kuhamasisha ukuaji
wa sekta ya usafiri wa anga na hatimaye kukuza utalii.
Aidha, hatua hii itasaidia wawekezaji katika sekta ya usafiri
wa anga kutumia bima za hapa nchini badala ya nje
kwenye mikataba ya ukodishaji; na
(ix) Kutoza Kodi ya Ongezeko la Thamani kwenye ada za
huduma za kibenki zinazotozwa na benki hizo ili kupanua
wigo wa kodi isipokuwa riba kwenye mikopo.
Hatua hizi za Kodi ya Ongezeko la Thamani kwa ujumla wake
zinatarajiwa kuongeza mapato ya Serikali kwa kiasi cha shilingi
milioni 136,140.3.
60
68. Mheshimiwa Spika, sambamba na marekebisho hayo
kwenye Kodi ya Ongezeko la Thamani, Serikali itachukua hatua
mbalimbali za kiutawala ndani ya Mamlaka ya Mapato ili kuboresha
makusanyo ya Kodi hii, ikiwa ni pamoja na kuanzisha programu
kabambe ya ufuatiliaji wa makusanyo na hivyo kupanua wigo wa kodi.
Ili kutekeleza azma hii, Serikali itatekeleza yafuatayo:
(i) kuhakikisha kuwa daftari la usajili wa walipakodi
linahuishwa kila wakati ili kuwa na taarifa sahihi za walipa
kodi hao;
(ii) kuhakikisha kuwa wafanyabiashara wote wakubwa na wa
kati hapa nchini wanapatiwa mashine za kielektroniki na
zinatumika kikamilifu;
(iii) kuendelea kuimarisha ukaguzi wa hesabu za walipakodi ili
kuwezesha kodi stahiki kulipwa kwa wakati; na
61
(iv) Kuanzisha ofisi mpya za kusimamia mapato kwa ngazi za
wilaya katika mikoa ya kikodi kwenye Jiji la Dar es Salaam
na vituo vipya vya huduma kwa walipakodi katika maeneo
mbalimbali ya majiji na miji mikubwa.
69. Mheshimiwa Spika, Napendekeza pia kufanya mapitio ya
Sheria ya Uwekezaji ili iendane na Sheria ya Kodi ya Ongezeko la
Thamani kwa lengo la kudhibiti na kupunguza misamaha ya kodi isiyo
na tija.
Hatua za kiutawala kwa pamoja zinatarajiwa kuongeza mapato ya
Serikali kwa kiasi cha shilingi milioni 268,607.1.
b) Sheria ya Ushuru wa Bidhaa (Excise Duty), SURA
147
70. Mheshimiwa Spika, napendekeza kufanya marekebisho
kwenye Sheria ya Ushuru wa Bidhaa, Sura 147 kama ifuatavyo: –
62
(i) Kufanya marekebisho ya viwango maalum vya kodi (specific duty
rates) vya bidhaa zisizo za petroli kwa kiwango cha mfumuko wa
bei wa asilimia 5. Marekebisho haya ni kwa mujibu wa Sheria ya
Ushuru wa Bidhaa inayotaka yafanyike marekebisho ya viwango
hivyo vya ushuru kulingana na mfumuko wa bei ili kuendana na
thamani halisi ya fedha. Hata hivyo, marekebisho haya
hayatafanyika kwenye maji ya kunywa yaliyosindikwa kwenye
chupa. Mabadiliko ninayopendekeza ni kama ifuatavyo:
a) Ushuru wa vinywaji baridi, kutoka shilingi 55 kwa lita hadi
shilingi 58 kwa lita;
b) Ushuru wa bidhaa kwenye maji ya matunda (juisi)
iliyotengenezwa kwa matunda yanayozalishwa hapa nchini
kutoka shilingi 10 kwa lita hadi shilingi 11 kwa lita;
c) Ushuru wa bidhaa kwenye maji ya matunda (juisi)
iliyotengenezwa kwa matunda ambayo hayazalishwi hapa
nchini kutoka shilingi 200 kwa lita hadi shilingi 210 kwa lita;
63
d) Ushuru wa bia inayotengenezwa kwa nafaka ya hapa nchini
na ambayo haijaoteshwa (unmalted), mfano kibuku, kutoka
shilingi 409 kwa lita hadi shilingi 430 Kwa lita;
e) Ushuru wa bia nyingine kutoka shilingi 694 kwa lita hadi
shilingi 729 kwa lita;
f) Ushuru wa bia zisizo na kilevi, ikijumuisha vinywaji vya
kuongeza nguvu kutoka shilingi 508 kwa lita hadi shilingi
534 kwa lita;
g) Ushuru wa mvinyo uliotengenezwa kwa zabibu
inayozalishwa ndani ya nchi kwa kiwango kinachozidi
asilimia 75 kutoka shilingi 192 kwa lita hadi shilingi 202 kwa
lita;
h) Ushuru wa mvinyo uliotengenezwa kwa zabibu
inayozalishwa nje ya nchi kwa kiwango kinachozidi asilimia
25 kutoka shilingi 2,130 kwa lita hadi shilingi 2,237 kwa lita;
64
i) Ushuru wa vinywaji vikali kutoka shilingi 3,157 kwa lita hadi
shilingi 3,315 kwa lita;
j) Ushuru wa bidhaa kwenye maji yanayozalishwa viwandani
hautaongezeka;
k) Sigara zisizo na kichungi zinazotengenezwa kutokana na
tumbaku inayozalishwa hapa nchini kwa kiwango cha
angalau asilimia 75, kutoka shilingi 11,289 hadi shilingi
11,854 kwa kila sigara elfu moja;
l) Sigara zenye kichungi zinazotengenezwa kutokana na
tumbaku inayozalishwa hapa nchini kwa kiwango cha
angalau asilimia 75, kutoka shilingi 26,689 hadi shilingi
28,024 kwa kila sigara elfu moja;
65
m) Sigara nyingine zenye sifa tofauti na (k) na (l) hapo juu
kutoka shilingi 48,285 hadi shilingi 50,700 kwa kila sigara
elfu moja;
n) Tumbaku ambayo iko tayari kutengeneza sigara (cut filler)
kutoka shilingi 24,388 hadi shilingi 25,608 kwa kilo;
o) Ushuru wa “cigar” unabaki kuwa asilimia 30;
p) Ushuru wa mafuta ya kulainishia mitambo kutoka shilingi
665.50 kwa lita hadi shilingi 699 kwa lita;
q) Ushuru wa grisi za kulainishia mitambo kutoka senti 75 kwa
kilo hadi senti 79 kwa kilo; na
r) Ushuru wa gesi asilia kutoka senti 43 kwa futi za ujazo hadi
senti 45 kwa futi za ujazo.
66
(ii) Kuongeza ushuru wa bidhaa (excise duty) unaotozwa kwenye
samani zinazoagizwa kutoka nje ya nchi zinazotambulika katika
HS Code 94.01 na HS Code 94.03 kutoka asilimia 15 hadi
asilimia 20 kwa lengo la kuhamasisha matumizi ya samani
zinazotengenezwa kwa kutumia mbao zinazozalishwa hapa
nchini, kuongeza ajira na kuongeza mapato ya Serikali;
(iii) Kutokana na ugumu uliojitokeza katika kudhibiti uchafuzi wa
mazingira unaotokana na mifuko ya plastiki, Serikali imeamua
kupiga marufuku utengenezaji, uuzaji, ununuzi na matumizi ya
mifuko ya plastiki yenye kipimo cha unene chini ya microns 50;
na
(iv) Kutoza ushuru wa bidhaa wa asilimia 10 kwenye ada
zinazotozwa na watoa huduma wa simu katika kutuma na
kupokea fedha badala ya ushuru huo kutozwa tu kwenye
kutuma fedha pekee. Katika utaratibu wa sasa, baadhi ya
kampuni zinazotoa huduma zimetumia mwanya kwa kuhamishia
67
sehemu kubwa ya ada hizo kwenye kupokea fedha na hivyo
kuwa nje ya wigo wa kodi.
Hatua hizi za ushuru wa bidhaa kwa pamoja zinatarajiwa kuongeza
mapato ya Serikali kwa kiasi cha shilingi milioni 63,639.4.
c) Sheria ya Kodi ya Mapato, SURA 332;
71. Mheshimiwa Spika, napendekeza kufanya marekebisho
kwenye Sheria ya Kodi ya Mapato, SURA 332 kama ifuatavyo: –
(i) Kuondoa msamaha wa kodi ya mapato kwenye malipo ya kiinua
mgongo kinacholipwa kwa wabunge kila mwisho wa muhula wa
miaka mitano ili kujenga misingi ya usawa na haki katika utozaji
wa kodi kwa kila mtu anayestahili kulipa kodi;
(ii) Kutoza Kodi ya Mapato kwenye mapato yote yatokanayo na hisa
kwenye makampuni. Marekebisho hayo yatafanyika kwa kufuta
aya ya (d) katika kifungu cha 3 cha Sheria ya Kodi ya Mapato,
Sura 332 cha tafsiri ya maneno “Investment Asset” (rasilimali za
68
uwekezaji) iliyokuwa inatoa msamaha wa kodi kwa wenye hisa
chini ya asilimia 25 kwenye makampuni. Hatua hii itaongeza
wigo wa kodi kwa ujumla wake na kupunguza misamaha ya
kodi;
(iii) Kupunguza kiwango cha chini cha kutoza kodi ya mapato
yanayotokana na ajira kutoka asilimia 11 hadi asilimia 9. Hatua
hii inachukuliwa ikiwa ni sehemu ya dhamira ya Serikali ya muda
mrefu ya kuwapunguzia mzigo wa kodi wafanyakazi hatua kwa
hatua hadi kufikia kiwango cha tarakimu moja. Katika kutekeleza
azma hiyo, Serikali imekuwa ikipunguza kiwango cha kodi ya
mapato ya ajira kutoka asilimia 18.5 mwaka 2006/07 hadi kufikia
asilimia 9 inayopendekezwa sasa. Kutokana na mabadiliko hayo,
viwango vya kodi vya sasa na vinavyopendekezwa ni kama
ifuatavyo:
69
Viwango vya sasa
Ngazi Mapato kwa Mwezi Kodi kwa mwezi
1. Mapato ya jumla yasiyozidi Shilingi
170,000/=
Asilimia sifuri (0%)
2. Mapato ya jumla yanayozidi Shilingi
170,000/=lakini hayazidi shilingi
360,000/=
11% ya kiasi
kinachozidi Shilingi
170,000/=
3. Mapato ya jumla yanayozidi Shilingi
360,000/= lakini hayazidi shilingi
540,000/=
Shilingi 20,900/= +
20% ya kiasi
kinachozidi Shilingi
360,000/=
4.
Mapato ya jumla yanayozidi Shilingi
540,000/= lakini hayazidi shilingi
720,000/=
Shilingi 56,900/= +
25% ya kiasi
kinachozidi Shilingi
540,000/=
5. Mapato ya jumla yanayozidi Shilingi
720,000/=
Shilingi 101,900/= +
30% ya kiasi
kinachozidi Shilingi
720,000/=
70
Viwango vinavyopendekezwa
Ngazi Mapato kwa Mwezi Kodi kwa mwezi
1 Mapato ya jumla yasiyozidi Shilingi
170,000/=
Asilimia sifuri (0%)
2 Mapato ya jumla yanayozidi Shilingi
170,000/=lakini hayazidi shilingi
360,000/=
9% ya kiasi
kinachozidi shilingi
170,000/=
3
Mapato ya jumla yanayozidi Shilingi
360,000/= lakini hayazidi shilingi
540,000/=
Shilingi 17,100+
20% ya kiasi
kinachozidi shilingi
360,000/=
4
Mapato ya jumla yanayozidi Shilingi
540,000/= lakini hayazidi shilingi
720,000/=
Shilingi 53,100+
25% ya kiasi
kinachozidi shilingi
540,000/=
5
Mapato ya jumla yanayozidi Shilingi
720,000/=
Shilingi 98,100+
30% ya kiasi
kinachozidi shilingi
720,000/=
71
(iv) Kutoza kodi ya zuio kwenye malipo yanayofanywa kwenye
mifuko ya jamii yanayotokana na mapato ya uwekezaji ili
kuweka misingi ya usawa na haki katika utozaji kodi. Hatua hii
inalenga kuweka wajibu kwa makampuni wa kutoza kodi ya zuio
kwenye malipo yanayofanywa kwenye mifuko ya jamii kutokana
na upangishaji, ukopeshaji, n.k; na
(v) Kumpa Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA)
mamlaka ya kukadiria mapato yanayotokana na pango kwa
kuweka kiwango cha ukomo wa chini wa thamani kulingana na
hali halisi ya soko ili kutoza kodi kwenye mapato hayo (rental
income).
Hatua hizi za Kodi ya Mapato kwa pamoja zinatarajiwa kupunguza
mapato ya Serikali kwa kiasi cha shilingi milioni 71,586.9.
72. Mheshimiwa Spika, sambamba na marekebisho hayo
kwenye Kodi ya Mapato, hatua mbalimbali za kiutawala ndani ya
72
Mamlaka ya Mapato zitachukuliwa ikiwa ni pamoja na kuanzisha
programu kabambe ya ufuatiliaji wa makusanyo na kuanzisha ofisi
mpya za kusimamia mapato katika maeneo mbalimbali kwenye ngazi
za wilaya na vituo vya miji. Hatua hii itajumuisha kusajili walipakodi
wapya, na kuhakikisha kunakuwa na ufuatiliaji wa walipakodi waliopo
ili walipe kodi stahiki.
Hatua hizi za kiutawala kwa pamoja zinatarajiwa kuongeza mapato ya
Serikali kwa kiasi cha shilingi milioni 80,108.18.
d) Sheria ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi Stadi, SURA 82
73. Mheshimiwa Spika, napendekeza kupunguza Tozo ya
kuendeleza ufundi stadi (Skills Development Levy) kutoka kiwango
cha sasa cha asilimia 5 hadi asilimia 4.5 ili kuwapatia nafuu ya mzigo
wa tozo waajiri na kuhamasisha ulipaji wa kodi kwa hiari pasipo
shuruti na hivyo kuongeza mapato ya serikali katika muda wa kati.
Hatua hii itapunguza mapato ya Serikali kwa kiasi cha shilingi milioni
28,403.4
73
e) Sheria ya Magari (Kodi ya Usajili na Uhamisho wa
Umiliki), SURA 124
74. Mheshimiwa Spika, napendekeza kufanya marekebisho
kwenye Sheria ya Magari (Kodi ya Usajili na Uhamisho wa Umiliki),
SURA 124 kama ifuatavyo: –
(i) Kufanya marekebisho ya viwango vya usajili wa magari na
pikipiki kutoka shilingi 150,000 hadi shilingi 250,000 kwa
kila gari; na kutoka shilingi 45,000 hadi shilingi 95,000 kwa
kila pikipiki; na
(ii) Kupandisha ada ya usajili wa namba binafsi za magari
kutoka shilingi 5,000,000 hadi shilingi 10,000,000 kwa kila
baada ya miaka mitatu ili kuhuisha viwango hivyo
kulingana na thamani halisi ya fedha.
Hatua hizi kwa pamoja zitaongeza mapato ya Serikali kwa kiasi cha
shilingi milioni 26,915.9.
74
f) Sheria ya Mamlaka ya Mapato Tanzania, SURA 399;
Sheria ya kodi ya Majengo ya Mamlaka ya Miji, SURA
289; Sheria ya Fedha ya Serikali za Mitaa, SURA 290;
Sheria ya Utawala wa Kodi ya mwaka 2015; na Sheria ya
Rufani za Kodi, SURA 408
75. Mheshimiwa Spika, napendekeza kufanya marekebisho
katika Sheria ya Mamlaka ya Mapato Tanzania, SURA 399, Sheria ya
Kodi ya Majengo ya Mamlaka ya Miji, Sura 289, Sheria ya Fedha ya
Serikali za Mitaa, Sura 290, Sheria ya Utawala wa Kodi ya mwaka
2015 na Sheria ya Rufani za Kodi, Sura 408 ili kuiwezesha Mamlaka ya
Mapato Tanzania kukusanya kodi ya Majengo ambapo hivi sasa kodi
hiyo inakusanywa na Halmashauri. Lengo la marekebisho haya,
pamoja na mambo mengine, ni kama ifuatavyo;
(i) Kuiwezesha Mamlaka ya Mapato kukadiria Kodi ya Majengo
na kufanya uthamini wa majengo husika;
75
(ii) Mamlaka ya Mapato Tanzania kupewa uwezo wa
kukusanya Kodi ya Majengo kwa kutumia utaratibu wake
wa kawaida kupitia sheria za kodi;
(iii) Kuweka utaratibu wa namna ya kuhifadhi na kuwasilisha
Kodi ya Majengo itakayokusanywa na Mamlaka ya Mapato
Tanzania kwenye Halmashauri husika;
(iv) Kuwezesha taratibu za kutatua migogoro itakayotokana na
ukusanyaji wa Kodi ya Majengo kusimamiwa na Sheria
zinazotumika hivi sasa na Mamlaka ya Mapato Tanzania
katika kusimamia migogoro ya kodi; na
(v) Kufanya maboresho katika misamaha ya Kodi ya Majengo
ili majengo mengi zaidi yaingizwe katika mfumo wa
utozwaji kodi hiyo.
76
g) Sheria ya Msajili wa Hazina (Mamlaka na Majukumu),
SURA 370
76. Mheshimiwa Spika, napendekeza kufanya marekebisho
kwenye Sheria ya Msajili wa Hazina (Mamlaka na Majukumu) SURA
370, ili kuzitaka wakala na taasisi zote za usimamizi na udhibiti zilizo
chini ya Msajili wa Hazina kuchangia asilimia 15 ya mapato yake ghafi
katika Mfuko Mkuu wa Serikali. Taasisi hizo zitatangazwa kwenye
Gazeti la Serikali. Aidha, napendekeza kuiondoa katika orodha hiyo
taasisi ya AICC na kuwekwa katika orodha ya taasisi zinazotakiwa
kutoa gawio (dividend) kwa Serikali kwa kuwa ni taasisi inayofanya
biashara.
h) Sheria ya Forodha ya Jumuiya ya Afrika Mashariki, ya
mwaka 2004
77. Mheshimiwa Spika, Mawaziri wa Fedha wa Jumuiya ya
Afrika Mashariki walifanya kikao cha maandalizi ya Bajeti (Pre-Budget
Consultations of EAC Ministers for Finance) jijini Arusha, Tanzania,
kuanzia tarehe 2 hadi 5 Mei, 2016. Katika kikao hicho, walikubaliana
kwa pamoja kufanya marekebisho ya viwango vya ushuru wa pamoja
77
wa forodha (EAC Common External Tariff “CET”) na kurekebisha
Sheria ya Forodha ya Jumuiya ya Afrika Mashariki, (EAC-Customs
Management Act, 2004) kwa mwaka wa fedha 2016/17 kama
ifuatavyo: –
78. Mheshimiwa Spika, marekebisho ya viwango vya ushuru wa
pamoja wa forodha (EAC Common External Tariff “CET”)
yaliyokubaliwa yalizingatia kwa sehemu kubwa katika kuendeleza
uchumi wa viwanda kwenye ukanda wa Jumuiya ya Afrika Mashariki
kama ifuatavyo:-
(i) Tanzania kutoza Ushuru wa Forodha wa asilimia 35 badala
ya asilimia 25 kwenye bidhaa ya saruji inayotambuliwa
katika HS Code 2523.29.00 kwa kipindi cha mwaka mmoja.
Hatua hii inalenga katika kuhamasisha na kulinda uzalishaji
wa saruji hapa nchini ambao umekuwa ukiongezeka dhidi
ya ushindani wa bei ya saruji inayoingizwa nchini kutoka
nje;
78
(ii) Kuongeza Ushuru wa Forodha kutoka asilimia 0 hadi
asilimia 10 kwenye bidhaa za chuma (flat rolled products of
iron or non-alloy steel) zinazotambuliwa kwenye HS Codes:
(HS Code 7208.54.00; HS Code 7208.90.00; HS Code
7208.52.00; and, HS Code 7208.53.00). Hatua hii inalenga
katika kulinda uzalishaji wa bidhaa hizi hapa nchini. Utafiti
uliofanywa na Nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki
unaonesha kuwa uzalishaji wa bidhaa za chuma umekuwa
ukiongezeka na uwezo upo wa kukidhi mahitaji. Hata hivyo
kuna ushindani usio wa haki kutoka kwenye bidhaa za
vyuma zinazotoka nje ambazo ni za bei ya chini na zisizo
na kiwango bora;
(iii) Kutoza Ushuru wa Forodha wa asilimia 25 badala ya
asilimia 10 kwenye bidhaa za nondo (bars and rods of iron
and steel) kwa bidhaa zinazotambulika chini ya HS Codes:
(HS Code 7213.10.00; HS Code 7213.20.00; HS Code
7213.99.00; HS Code 7227.10.00; HS Code 7227.20.00; HS
Code 7227.90.00; HS Code 7308.20.00; HS Code
79
7308.40.00; na HS Code 9406.00.90). Lengo la hatua hii ni
kulinda uzalishaji wa bidhaa za chuma zinazozalishwa na
viwanda vya ndani dhidi ya ushindani wa bidhaa zisizo na
ubora na za bei ya chini kutoka nje ya nchi;
(iv) Kuendelea kutoza Ushuru wa Forodha wa asilimia 0 badala
ya asilimia 25 kwenye bidhaa za chuma “iron and steel
products” zinazotambulika chini ya HS Code 7308.10.00
ambazo ni muhimu katika ujenzi wa madaraja (bridge and
bridge sections);
(v) Kuendelea kutoza Ushuru wa Forodha wa asilimia 10 kwa
mwaka mmoja badala ya asilimia 25 kwenye “automotive
bolts and nuts” zinazotambulika kwenye HS Code
7318.15.00. Aidha, ushuru huu unapunguzwa kwa
kuzingatia kwamba malighafi zinazotumika kutengeneza
bidhaa hizi hazizalishwi katika Nchi za Jumuiya ya Afrika
Mashariki;
80
(vi) Kutoa msamaha wa ushuru wa forodha kwa utaratibu wa
duty remission kwa wazalishaji wa “bolts and nuts” kwenye
malighafi zinazotambulika chini ya Hs Code 7228.30.00 na
HS Code 7228.50.00 kwa kutoza kiwango cha asilimia 0
badala ya asilimia 10. Lengo la hatua hii ni kuwawezesha
wazalishaji kupata malighafi hizo kwa gharama nafuu kwa
kuwa hazizalishwi katika ukanda wa Afrika Mashariki;
(vii) Kutoza Ushuru wa Forodha wa asilimia 25 badala ya
kiwango cha sasa cha asilimia 10 kwenye nyavu za samaki
zinazotambulika chini ya HS Code 5608.11.00. Hatua hii
inazingatia kuwa kuna watengenezaji wengi wa nyavu za
aina hii katika Jumuiya ya Afrika Mashariki;
(viii) Kutoza Ushuru wa Forodha wa asilimia 25 badala ya
kiwango cha sasa cha asilimia 10 kwenye bidhaa za “Oil
and Petrol Filters” zinazotambulika kwenye HS Code
8421.23.00, na “intake air filters” zinazotambulika kwenye
81
HS Code 8421.31.00. Lengo la hatua hii ni kulinda
uzalishaji wa bidhaa hizi zinazozalishwa na viwanda vya
ndani dhidi ya ushindani wa bidhaa zisizo na ubora na za
bei rahisi kutoka nje ya nchi;
(ix) Kutoa msamaha wa Ushuru wa Forodha na kutoza asilimia
0 kwa utaratibu wa duty remission kwenye malighafi za
kutengenezea “air filters” za magari kwa wazalishaji wa
hapa nchini;
(x) Kutoa msamaha wa Ushuru wa Forodha na kutoza asilimia
0 kwa utaratibu wa duty remission kwenye malighafi
(splints) za kutengenezea vibiriti zinazotambulika chini ya
HS Code 4421.90.00. Hatua hii imezingatia kwamba
hakuna misitu ya kutosha na yenye mbao za kukomaa
zinazokidhi mahitaji katika Jumuiya ya Afrika Mashariki;
(xi) Nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki kupunguza msamaha
wa Ushuru wa Forodha hatua kwa hatua kwenye Sukari
82
(sugar and sugar confectionery) kutoka kiwango cha sasa
ambapo waagizaji wa sukari ya viwandani hulipa asilimia
10. Kutokana na kupunguza msamaha huo, waagizaji
watalipa ushuru zaidi hatua kwa hatua. Upunguzaji wa
msamaha utakuwa kama ifuatavyo: mwaka 2016/17
kiwango kitakuwa asilimia 15, 2017/18 kiwango kitakuwa
cha asilimia 20, 2018/19 kiwango kitakuwa cha asilimia 25.
Hatua hii inachukuliwa kwa kuwa kiwango cha sasa cha
asilimia 10 kinadidimiza viwanda vyetu vya ndani na pia ni
chachu ya matumizi mabaya ya misamaha husika;
(xii) Kutoza Ushuru wa Forodha wa asilimia 25 badala ya
asilimia 10 za sasa kwa bidhaa zinazotambulika chini ya HS
Code 7612 “Aluminium Milk Cans”. Hizi ni bidhaa
zilizokamilika tayari kwa kutumika hivyo zinatakiwa
kutozwa ushuru wa asilimia 25 unaostahili kwa bidhaa za
namna hiyo. Lengo la hatua hii ni kulinda wazalishaji wa
ndani wenye uwezo wa kuzalisha bidhaa hizi kwenye nchi
za Jumuiya ya Afrika Mashariki;
83
(xiii) Kutoa msamaha wa Ushuru wa Forodha na kutoza asilimia
0 malighafi zinazoagizwa na wazalishaji wa Aluminium cans
zinazotambulika chini ya HS Codes 7606.12.00 na HS
Codes 7606.92.00. Hatua hii inalenga katika kuhamasisha
uzalishaji wa “aluminium cans” katika Nchi za Jumuiya ya
Afrika Mashariki;
(xiv) Kutoza Ushuru wa Forodha wa asilimia 10 badala ya
asilimia 35 kwenye ngano (Wheat grain) inayotambuliwa
chini ya HS Code 1001.99.10 na HS Code 1001.99.90 kwa
mwaka mmoja. Hatua hii imezingatia kwamba nchi za
Jumuiya ya Afrika Mashariki hazina uwezo wa kuzalisha
ngano ya aina hii na kuweza kutosheleza mahitaji. Aidha,
itatoa unafuu kwa wazalishaji wa bidhaa na vyakula
vinavyotumia ngano na kuimarisha utulivu wa bei ya
bidhaa za ngano;
84
(xv) Kuongeza kiwango maalumu cha ushuru kwenye mitumba
ya nguo na viatu kutoka kiwango cha sasa cha dola za
kimarekani 0.2 kwa kilo hadi dola 0.4 kwa kilo. Hatua hii
imechukuliwa ili kudhibiti hatua kwa hatua uingizaji nchini
wa nguo za mitumba ambazo zimeonekana kuwa siyo
salama kwa afya za watu wetu. Aidha, Nchi wanachama wa
Jumuiya ya Afrika Mashariki zimekubaliana kuzuia kabisa
uingizaji wa bidhaa hizi baada ya miaka mitatu kuanzia
sasa. Hata hivyo Nchi hizi zimekubaliana kuweka mikakati
ya kuimarisha na kuhamasisha uzalishaji wa nguo na viatu
ndani ya Jumuiya ya Afrika Mashariki ili kukidhi mahitaji.
Wizara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji tayari imeandaa
mikakati madhubuti ya kuendeleza sekta za ngozi na nguo;
(xvi) Kuendelea kutoza ushuru wa forodha wa asilimia 25 au
kiwango maalum cha dola za kimarekani 200 – kutegemea
kiwango kipi ni kikubwa kwa kila tani moja ya ujazo (metric
ton) kwenye bidhaa za chuma (iron and iron-alloy steel)
85
kwa mwaka mmoja, zinazotambuliwa katika HS Codes: HS
Codes 7210.41.00; HS Codes 7210.49.00; HS Codes
7210.61.00; HS Codes 7210.69.00; HS Codes 7210.70.00;
HS Codes 7210.90.00; HS Codes 7212.30.00; and HS
Codes 7212.40.00. Lengo la hatua hii ni kulinda uzalishaji
wa bidhaa za chuma zinazozalishwa na viwanda vya ndani
dhidi ya ushindani wa bidhaa zisizo na ubora kutoka nje ya
nchi. Utafiti uliofanywa na Nchi za Jumuiya ya Afrika
Mashariki umeonesha kuwa kumekuwa na ongezeko kubwa
la uzalishaji wa bidhaa za vyuma kupita mahitaji ya soko
katika soko la dunia. Hali hiyo imesababisha kushuka sana
kwa bei na hivyo kuathiri viwanda vyetu kutokana na
ushindani wa bidhaa hizo kutoka nje. Hatua hii ya kuweka
viwango maalum vya kodi ni muhimu kulinda viwanda na
bidhaa zetu (anti-dumping measure);
(xvii)Kuendelea kutoza ushuru wa forodha wa asilimia 25 au
kiwango maalum cha dola za kimarekani 200 – kutegemea
kiwango kipi ni kikubwa kwa mwaka mmoja kwa kila tani
86
moja ya ujazo (metric ton) kwenye bidhaa za chuma (Flatrolled
products of bars, rods, sections, angles, shapes, and
related products) zinazotambuliwa katika HS Codes: HS
Codes 7214.10.00; HS Codes 7214.20.00; HS Codes
7214.30.00; HS Codes 7214.91.00; and HS Codes
7214.99.00. Lengo la hatua hii ni kulinda uzalishaji wa
bidhaa za chuma zinazozalishwa na viwanda vya ndani
dhidi ya ushindani wa bidhaa zisizo na ubora kutoka nje ya
nchi;
(xviii) Kuendelea kutoza Ushuru wa Forodha wa asilimia 25
au kiwango maalum cha dola za kimarekani 200 –
kutegemea kiwango kipi ni kikubwa kwa mwaka mmoja
kwa kila tani moja ya ujazo “metric ton’ kwenye bidhaa za
chuma (steel reinforcement bars, angles, sections
zinazotambuliwa chini ya HS Codes: 7216.10.00; HS Codes
7216.21.00; HS Codes 7216.22.00; and HS Codes
7216.50.00.). Lengo la hatua hii ni kulinda uzalishaji wa
bidhaa za chuma zinazozalishwa na viwanda vya ndani
87
dhidi ya ushindani wa bidhaa zisizo na ubora kutoka nje ya
nchi;
(xix) Kutoza Ushuru wa Forodha wa asilimia 10 badala ya
asilimia 0 kwenye mafuta ghafi ya kula (crude edible oil)
yanayotambulika katika HS Code 1511.10.00 kwa mwaka
mmoja. Hatua hii inalenga katika kuhamasisha kilimo cha
mbegu za mafuta hapa nchini na kukuza viwanda vya
kutengeneza mafuta ya kula. Aidha, Wizara ya Viwanda,
Biashara na Uwekezaji imeandaa mkakati maalum wa
kuendeleza viwanda vya kuzalisha mafuta yanayotokana na
mbegu zinazozalishwa hapa nchini na kutumia fursa soko
kubwa lililopo katika Jumuiya ya Afrika Mashariki ambapo
Tanzania inayo nafasi ya kuweza kuongeza uzalishaji wa
mbegu za mafuta;
(xx) Kutoza Ushuru wa Forodha wa asilimia 25 badala ya
asilimia 10 kwa bidhaa za karatasi zinazotambulika kwenye
HS Codes: HS Codes 4804.11.00; HS Codes 4804.19.10;
88
HS Codes 4804.19.90; HS Codes 4804.21.00; HS Codes
4804.29.00; HS Codes 4804.31.00; HS Codes 4804.39.00;
HS Codes 4804.41.00; HS Codes 4805.59.00; HS Codes
4805.11.00; HS Codes 4805.12.00; HS Codes 4805.19.00;
HS Codes 4805.24.00; HS Codes 4805.25.00; HS Codes
4805.30.00; HS Codes 4805.91.00, na HS Codes
4805.92.00. Hatua hii inachukuliwa ili kulinda viwanda vya
hapa nchini vinavyozalisha karatasi za aina hiyo na ajira;
(xxi) Kuendelea kutoza Ushuru wa Forodha wa asilimia 25 au
kiwango maalum cha dola za kimarekani 200 – kutegemea
kiwango kipi ni kikubwa kwa mwaka mmoja kwa kila tani
moja ya ujazo (metric ton) kwenye bidhaa za nondo
zinazotambulika kwenye HS Codes HS Codes 7228.10.00;
HS Codes 7228.20.00; HS Codes 7228.30.00; HS Codes
7228.40.00; HS Codes 7228.50.00; HS Codes 7228.60.00;
HS Codes 7228.70.00; na HS Codes 7228.80.00. Lengo ni
kulinda viwanda vya ndani kutokana na ushindani wa
bidhaa kama hizo zinazoagizwa nje; na
89
(xxii)Kuendelea kutoza Ushuru wa Forodha wa asilimia 25 au
kiwango maalum cha dola za kimarekani 200 – kutegemea
kiwango kipi ni kikubwa kwa mwaka mmoja kwa kila tani
moja ya ujazo (metric ton) kwenye bidhaa za chuma
zinazotambulika kwenye HS Codes 7212.40.00; HS Codes
7215.10.00; HS Codes 7215.50.00; HS Codes 7215.90.00;
HS Codes 7216.61.00; HS Codes 7216.69.00; HS Codes
7216.91.00; na HS Codes 7216.99.00.
79. Mheshimiwa Spika, Mawaziri wa Fedha wa Jumuiya ya
Afrika Mashariki walifanya pia marekebisho kwenye Sheria ya Forodha
ya Jumuiya ya Afrika Mashariki, (EAC-Customs Management Act,
2004) kama ifuatavyo:-
(i) Kufanya marekebisho katika Jedwali la Tano (5) la Sheria
ya Forodha ya Jumuiya ya Afrika Mashariki linalotoa
msamaha wa ushuru wa forodha ili kuongeza vifaa vya
majokofu yanayotumika katika kuhifadhi maiti
90
yanayotambuliwa chini ya HS Code 8418.69.90 kwa
matumizi ya hospitali na mamlaka za miji (city councils);
(ii) Kufanya marekebisho katika Jedwali la Tano (5) la Sheria
ya Forodha ya Jumuiya ya Afrika Mashariki (Chapters 84
and 69) linalotoa msamaha wa ushuru wa forodha ili
kuongeza vifaa vinavyotumika kwenye hospitali kuteketeza
na kuchoma uchafu (incinerator’s equipments and
materials used in hospitals to burn waste);
(iii) Kufanya marekebisho katika Jedwali la Tano (5) la Sheria
ya Forodha ya Jumuiya ya Afrika Mashariki ili kuondoa
msamaha wa ushuru wa forodha unaotolewa kwenye sare
za wafanyakazi wa hospitali. Msamaha huu unaondolewa
kwa kuwa sare hizi zinaweza kuzalishwa katika nchi za
Jumuiya ya Afrika Mashariki;
91
(iv) Kusamehe Ushuru wa Forodha kwa kutumia utaratibu wa
“Duty remission” kwa wazalishaji wa hapa nchini wa
malighafi zinazotumika kutengeneza betri zinazofahamika
kama “deep cycle batteries”. Hatua hii inalenga katika
kuhamasisha uzalishaji wa viwanda vya ndani kwa kuwa
deep cycle batteries zinazoagizwa kutoka nje ya nchi
zimesamehewa ushuru kupitia Jedwali la Tano (5) la Sheria
ya Forodha ya Jumuiya ya Afrika Mashariki;
(v) Kufanya marekebisho katika Jedwali la Tano (5) la Sheria
ya Forodha ya Jumuiya ya Afrika Mashariki linalotoa
msamaha wa ushuru wa forodha ili kujumuisha chupa
zinazotumika kwa ajili ya kukusanya damu kwenye hospitali
(blood collection tubes); na
(vi) Kusamehe Ushuru wa Forodha kwa kutumia utaratibu wa
“Duty remission” kwa malighafi zinazotumika kuzalisha
vifaa vya Nishati ya umeme wa jua (Solar equipments).
92
Hatua zote za Ushuru wa Forodha kwa pamoja zinatarajiwa
kuongeza mapato kwa kiasi cha shilingi milioni 42,850.6.
i) Marekebisho madogo madogo katika baadhi ya Sheria
za Kodi na Sheria nyingine mbalimbali
80. Mheshimiwa Spika, napendekeza kufanya marekebisho
mengine madogo madogo yasiyo ya kisera na ya kiuandishi katika
Sheria mbalimbali za kodi pamoja na sheria nyingine ili ziwe sanjari na
azma ya kurahisisha utekelezaji wake. Marekebisho hayo yataainishwa
katika muswada wa Sheria ya Fedha 2016.
81. Mheshimiwa Spika, ili kurahisisha utekelezaji wa Sheria ya
bajeti ya Mwaka 2015, na kuleta uwajibikaji katika utekelezaji wa
Bajeti ya Mfuko wa Mahakama na Mfuko wa Bunge napendekeza
kufanya marekebisho yafuatayo:-
(i) Kurekebisha kifungu cha 29 kifungu kidogo cha 3 cha
Sheria ya Utawala wa Bunge, SURA 115 (The National
93
Assembly Administration Act, CAP 115) ili kubainisha kuwa
bajeti ya Mfuko wa Bunge itawasilishwa Bungeni na Waziri
mwenye dhamana na masuala ya Bunge. Hivi sasa Sheria
hii imeweka sharti kwa Waziri mwenye dhamana na
masuala ya fedha kuwasilisha Bungeni Bajeti ya Mfuko wa
Bunge; na
(ii) Kurekebisha kifungu cha 59 kifungu kidogo cha 3 cha
Sheria ya Utawala wa Mahakama, SURA 237 (The Judiciary
Administraion Act, CAP 237) ili Bajeti ya Mfuko wa
Mahakama iwasilishwe Bungeni na Waziri mwenye
dhamana na masuala ya mahakama. Kifungu hiki kwa sasa
kimeweka sharti kwa Waziri mwenye dhamana na masuala
ya fedha kuwasilisha Bungeni Bajeti ya Mfuko wa
Mahakama.
94
j) Marekebisho ya Ada na Tozo Mbalimbali zinazotozwa
na Wizara, Mikoa na Idara zinazojitegemea
82. Mheshimiwa Spika, napendekeza kufanya marekebisho ya
viwango vya ada na tozo mbali mbali zinazotozwa na Wizara, Mikoa
na Idara zinazojitegemea ili kuvihuisha kulingana na hali halisi ya
ukuaji wa uchumi. Aidha, napendekeza kufuta baadhi ya Ada na
Tozo ambazo zimeonekana kuwa kero kwa wananchi na kikwazo
katika kuboresha mazingira ya ufanyaji biashara hapa nchini. Tozo
na ada ninazopendekeza kuzifuta ni kama ifuatavyo:
(i) Mamlaka ya Chakula na Dawa (Tanzania Foods and
Drugs Authority – TFDA):
a) Kibali cha kusafirisha chakula nje ya nchi kwa shilingi
50,000;
b) Kushikilia dawa za binadamu na mifugo zinazotengenezwa
na viwanda vya ndani kwa shilingi 100,000;
95
c) Kudurufu cheti cha dawa za binadamu na mifugo
zinazotengenezwa na viwanda vya ndani kwa Dola za
Kimarekani 50;
d) Kudurufu cheti cha dawa za binadamu na mifugo
zinazotengenezwa na viwanda vya nje ya nchi kwa Dola za
Kimarekani 100;
e) Tathimini ya matangazo ya bidhaa zinazotengenezwa nchini
kwa Dola za Kimarekani 50;
f) Matangazo yanayofanyiwa tathimini fupi kwa bidhaa
zinazotengenezwa nchini kwa Dola za Kimarekani 25;
g) Kudurufu cheti cha usafi wa chakula, dawa na vifaa tiba
vinavyotengenezwa nje ya nchi kwa Dola za Kimarekani
100;
h) Kudurufu cheti cha vifaa tiba vinavyotengenezwa ndani ya
nchi kwa Dola za Kimarekani 30;
96
i) Kudurufu cheti cha dawa zinazotengenezwa nchini kwa Dola
za Kimarekani 50;
j) Kushikilia vitendanishi vinavyotengenezwa nje ya nchi katika
rejesta kwa Dola za Kimarekani 150;
k) Kushikilia vipodozi vinavyotengenezwa ndani ya nchi katika
regesta kwa shilingi 30,000;
l) Ukaguzi wa kiwanda cha dawa cha ndani ya nchi kabla ya
kusajiliwa kwa Dola za Kimarekani 250;
m) Wawakilishi wa makampuni ya dawa ya nje ya nchi kwa
Dola za Kimarekani 1,000;
n) Malighafi za vipodozi zinazoingizwa nchini kwa shilingi
50,000,000;
97
o) Malighafi za dawa zinazoingizwa nchini kwa shilingi
100,000,000;
p) Kibali cha hospitali kununua dawa zenye madhara ya
kulevya kutoka bohari kwa Dawa ya shilingi 10,000;
q) Ada ya uingizaji nchini wa dawa zenye madhara ya kulevya
ya shilingi 50,000;
r) Cheti cha kusafirisha bidhaa nje ya nchi kwa shilingi 50,000;
s) Cheti cha utambuzi wa dawa inayosafirishwa nje ya nchi
kwa 50,000;
t) Ukaguzi wa kiwanda kidogo kipya cha kusindika chakula
kwa shilingi 100,000;
u) Cheti cha kuteketeza bidhaa;
98
v) Cheti cha Afya kwa ajili ya kusafirisha bidhaa nje ya nchi
kwa shilingi 50,000; na
w)Kibali cha kufanya maonyesho ya biashara ya bidhaa
inayodhibitiwa kwa shilingi 200,000.
(ii) Bodi ya Pamba:
a) Mchango wa mwenge kwa kila kiwanda cha kuchambua
pamba wa shilingi 450,000; na
b) Ada ya vikao vya Halmashauri za wilaya wanapojadili
maombi mbalimbali ya wafanyabiashara wa pamba ya
shilingi 250,000.
(iii) Bodi ya Chai: Kodi ya moto na uokoaji.
(iv) Bodi ya Kahawa: Ada ya leseni ya kusindika kahawa ya Dola
za Kimarekani 250.
99
(v) Bodi ya Korosho:
a) Ushuru wa chama kikuu cha ushirika wa shilingi 20 kwa kilo;
b) Ushuru wa kusafirisha korosho wa shilingi 50 kwa kilo;
c) Gharama za mtunza ghala kwa shilingi 10 kwa kilo;
d) Kikosi kazi kwa ajili ya ufatiliaji wa masuala mbalimbali kwa
kuchangia shilingi 10 kwa kilo; na
e) Makato ya unyaufu
83. Mheshimiwa Spika, napenda nilifahamishe Bunge lako
Tukufu pamoja na wananchi kwamba, hatua ninazopendekeza za
kufuta tozo na ada nilizozifanya ni za awali tu wakati Serikali
inaendelea kufanya uchambuzi na tathmini ya kina kuhusu tozo na
ada zinazotozwa na mashirika, taasisi na wakala mbalimbali, ikiwa ni
pamoja na Serikali za Mitaa. Hatua hizi ni endelevu katika kuhakikisha
kuwa tunaboresha mazingira ya kufanya biashara ili nchi yetu iweze
kuwa na nafasi nzuri ya kiushindani katika biashara na kuvutia
100
uwekezaji. Aidha, lengo la hatua hizi ni pamoja na kuondoa kero kwa
wananchi na kuwapa unafuu katika uendeshaji wa shughuli za
kiuchumi.
84. Mheshimiwa Spika, napendekeza pia kurekebisha baadhi
viwango vya Ada na Tozo mbalimbali kama zitakavyoainishwa kwenye
Sheria ya Fedha 2016 na nyingine kutangazwa kwenye Gazeti la
Serikali (GNs) na Mawaziri wenye dhamana na Ada na Tozo hizo.
k) Kodi na Tozo Kwenye Bidhaa za Mafuta ya Petroli
85. Mheshimiwa Spika, kwa muda sasa bei ya mafuta (petroli,
dizeli na ya taa) imekuwa ikishuka katika soko la dunia, hali ambayo
imesaidia kuleta unafuu wa gharama katika shughuli za kiuchumi
hususan kwa wananchi masikini maana bei za mafuta haya zinagusa
kila mtu. Hivyo, Serikali imeamua kuwa Ushuru wa Barabara, Ushuru
wa Petroli na Ushuru wa Bidhaa kwenye mafuta ya petroli utabaki
kama ilivyo sasa. Hivyo, Mfuko wa barabara na Mamlaka ya
Usambazaji Umeme Vijijini watumie fedha hizi vizuri.
101
l) Misamaha ya Kodi kwa Majeshi ya Ulinzi na Usalama
86. Mheshimiwa Spika, kwa kipindi kirefu Serikali imekuwa
ikitoa misamaha ya kodi (Ushuru wa Bidhaa, Kodi ya Ongezeko la
Thamani na Ushuru wa Forodha) kwa majeshi ya Ulinzi na Usalama
kupitia kwenye migahawa na maduka maalum ambayo yanauza
bidhaa mbalimbali kwa mahitaji ya askari. Katika kufanya hivyo,
kumekuwa na changamoto ya kuwepo kwa matumizi mabaya ya
misamaha hiyo. Aidha, kutokana na hali hiyo ya upotevu wa mapato,
Nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki zimeondokana na utaratibu huu
isipokuwa Rwanda na Tanzania ambazo zinatoa msamaha wa Ushuru
wa Forodha kwa Majeshi ya Ulinzi na Usalama.
87. Mheshimiwa Spika, katika kikao cha Mawaziri wa Fedha wa
Jumuiya ya Afrika Mashariki cha Maandalizi ya Bajeti kwa mwaka
2015/16, Serikali ya Tanzania ilitakiwa kuangalia njia mbadala ya
kutoa unafuu wa gharama kwa majeshi yake badala ya utaratibu wa
kutoa misamaha. Ili kuendelea kutoa huduma kwa majeshi hayo
pasipo kupoteza mapato ya Serikali, napendekeza kuwapatia posho
majeshi yetu ya Ulinzi na Usalama ili kuwawezesha kununua mahitaji
102
yao wenyewe. Dhamira ya hatua hii ni kusitisha msamaha wa kodi
kwa majeshi ili kuondoa uvujaji mkubwa wa mapato na wakati huo
huo, kuendelea kuwapatia askari wetu mahitaji yao muhimu kwa
utaratibu mzuri zaidi. Aidha, lengo la hatua hii ni kuhakikisha kuwa
motisha unaotolewa unawanufaisha walengwa, yaani askari, badala
ya wajanja wachache kuendelea kunufaika na misamaha hiyo.
Tarehe ya Kuanza Kutekeleza Hatua Mpya za Kodi
88. Mheshimiwa Spika, Hatua hizi za kodi zinazopendekezwa
zitaanza kutekelezwa tarehe 1 Julai, 2016, isipokuwa pale ilipoelezwa
vinginevyo.
V. SURA YA BAJETI KWA MWAKA 2016/17
89. Mheshimiwa Spika, kwa kuzingatia sera za uchumi jumla
pamoja na misingi na sera za bajeti kwa mwaka 2016/17, Sura ya
Bajeti inaonesha kuwa jumla ya shilingi trilioni 29.54 zinatarajiwa
kukusanywa na kutumika katika kipindi hicho. Bajeti ya mwaka
2016/17 inatarajiwa kuwa na ongezeko la jumla ya shilingi trilioni 7.04
103
sawa na asilimia 31.1 ikilinganishwa na Bajeti ya mwaka 2015/16 ya
shilingi trilioni 22.49.
90. Mheshimiwa Spika, Serikali inalenga kukusanya mapato ya
ndani ikijumuisha mapato ya halmashauri ya jumla ya shilingi trilioni
18.46 sawa na asilimia 62.5 ya bajeti yote. Kati ya mapato hayo,
mapato ya kodi ni shilingi trilioni 15.11 sawa na asilimia 13.8 ya Pato
la Taifa. Aidha, mapato yasiyo ya kodi na mapato kutoka vyanzo vya
Halmashauri ni shilingi trilioni 2.69 na shilingi bilioni 665.4 kwa
mtiririko huo. Makisio ya mapato ya kodi na yasiyo ya kodi
yameongezeka kwa kuwa kuna viashiria vingi vinavyoonesha kwamba
TRA kwa kushirikiana na Wizara na Taasisi zinazokusanya maduhuli
wana uwezo wa kukusanya kiasi hiki cha mapato. Hivyo, Serikali
itasimamia kwa karibu na kuziba mianya yote ya uvujaji wa mapato ya
kodi na yasiyo ya kodi ili kuhakikisha kuwa malengo ya ukusanyaji
yanafikiwa.
104
91. Mheshimiwa Spika, Washirika wa Maendeleo wanatarajiwa
kuendelea kutupatia misaada na mikopo ya jumla ya shilingi trilioni
3.60 ambayo ni asilimia 12 ya bajeti yote. Kati ya kiasi hicho, shilingi
trilioni 2.75 ni misaada na mikopo kwa ajili ya miradi ya maendeleo;
shilingi bilioni 372.1 ni misaada na mikopo kwa mifuko ya pamoja ya
kisekta; na shilingi bilioni 483 ni misaada na mikopo ya kibajeti (GBS).
92. Mheshimiwa Spika, ili kuziba nakisi ya bajeti, katika mwaka
2016/17 Serikali inatarajia kukopa jumla ya shilingi trilioni 7.48 kutoka
katika vyanzo vya ndani na nje. Kati ya kiasi hicho, shilingi trilioni 5.37
zinategemewa kukopwa katika soko la ndani kwa ajili ya kulipia
hatifungani na dhamana za Serikali zinazoiva pamoja na mikopo
mipya kwa ajili ya kugharamia miradi ya maendeleo na kulipia
malimbikizo ya madai yaliyohakikiwa. Aidha, ili kuongeza kasi katika
ujenzi wa miundombinu na kuhakikisha inatekeleza Mpango wa Pili wa
Maendeleo kikamilifu, Serikali inatarajia kukopa shilingi trilioni 2.10
kutoka soko la nje kwa masharti ya kibiashara.
105
93. Mheshimiwa Spika, Serikali imefanya jitihada kubwa za
kuongeza ukusanyaji wa mapato ya ndani ili kugharamia, pamoja na
mambo mengine, miradi ya maendeleo. Utekelezaji wa miradi hiyo pia
hutegemea mikopo ya nje ya kibiashara ambayo upatikanaji wake
hutegemea hali ya soko la fedha duniani. Katika mwaka 2016/17,
kuna miradi mikubwa hususan ujenzi wa reli ya kati kwa kiwango cha
standard gauge na uimarishaji wa bandari ambayo matayarisho yake
yanahitaji muda na umakini mkubwa hasa uhakika wa upatikanaji wa
fedha. Hivyo, utekelezaji wa miradi hii unatarajiwa kuanza katika nusu
ya pili ya mwaka wa fedha 2016/17 baada ya kutathmini hali ya
upatikanaji wa fedha zaidi na kukamilisha maandalizi ya msingi ikiwa
ni pamoja na kumpata mkandarasi na kuingia mkataba. Matarajio ya
Serikali ni kuwa mkandarasi atakabidhiwa eneo (site) ndani ya miezi
tisa (9) ya kwanza ya 2016/17.
94. Mheshimiwa Spika, Kwa upande wa matumizi, katika mwaka
2016/17 Serikali inapanga kutumia jumla ya shilingi trilioni 29.54 kwa
matumizi ya kawaida na maendeleo. Kati ya fedha hizo, shilingi trilioni
17.72 zimetengwa kwa ajili ya matumizi ya kawaida na matumizi ya
106
maendeleo yatakuwa shilingi trilioni 11.82 sawa na asilimia 40 ya
bajeti yote ambapo kiasi cha Shilingi trilioni 8.70 ni fedha za ndani na
shilingi trilioni 3.12 ni fedha za nje.
95. Mheshimiwa Spika, Kwa kuzingatia mfumo wa bajeti kama
ulivyoelezwa hapo juu, sura ya bajeti kwa mwaka 2016/17 ni kama
inavyooneshwa katika Jedwali, ukurasa wa 92 wa kitabu cha hotuba
hii.
107
Mfumo wa Bajeti wa Mwaka 2016/17
Shilingi Milioni
Mapato 2016/17
A. Mapato ya Ndani-Serikali Kuu 17,798,118
(i) Mapato ya Kodi (TRA) 15,105,100
(ii) Mapato yasiyo ya kodi 2,693,018
B. Mapato ya Halmashauri 665,415
C. Misaada na Mikopo kutoka nje 3,600,807
(i) Misaada na Mikopo ya masharti nafuu -GBS 483,002
(ii)Misaada na Mikopo ya Miradi 2,745,659
(iii)Misaada na Mikopo ya Kisekta 372,147
D. Mikopo ya Ndani na yenye Masharti ya Kibiashara 7,475,264
(i)Mikopo-Masharti ya Kibiashara 2,100,995
(ii) Mikopo-asilimia 1.5 ya GDP 1,597,157
(iii)Mikopo- Rollover 3,777,112
JUMLA YA MAPATO YOTE (A+B+C+D) 29,539,603
Matumizi
E. Matumizi ya Kawaida 17,719,100
o/w (i) Malipo ya Deni la Taifa 8,000,000
-Malipo ya Riba Ndani 1,089,150
-Malipo ya Mtaji Ndani (Rollova) 3,777,112
– Malipo ya Riba na Mtaji Nje 1,586,640
– Michango ya Serikali kwenye Mifuko ya Hifadhi za Jamii 1,141,144
-Matumizi Mengine ya Mfuko Mkuu 405,954
(ii) Mishahara 6,600,000
(iii)Matumizi Mengineyo (OC)
– Matumizi yanayolindwa (protected expenditure) 2,492,934
– Matumizi ya Halmashauri 266,166
– Matumizi Mengine ya kuendesha ofisi 360,000
F. Matumizi ya Maendeleo 11,820,503
(i) Fedha za Ndani 8,702,697
o/w Matumizi ya Halmashauri 399,249
(ii)Fedha za Nje 3,117,805
JUMLA YA MATUMIZI YOTE (E+F) 29,539,603
NAKISI YA BAJETI 4.5 % YA GDP
108
VI. HITIMISHO
96. Mheshimiwa Spika, wananchi wetu wengi wamechoka na
adha ya umaskini: Watanzania wanataka kipato cha kuweza kukidhi
mahitaji yao ya msingi. Wananchi wanataka huduma bora zaidi
hususan upatikanaji wa maji, elimu, afya, umeme na makazi; akina
mama wamechoka kutembea na ndoo za maji kichwani; watoto wetu
shuleni wamechoka kukaa chini na kugombania matundu machache
ya vyoo; vijana wanataka ajira; kilio cha mauaji ya kikatili ya albino ni
fedheha kwa nchi yetu; wananchi bado wananyimwa haki zao
kutokana na kukithiri kwa rushwa; Watanzania wanataka nchi yenye
neema; Watanzania wanataka Serikali inayofanya kazi kwa ufanisi;
Watanzania wanataka mazingira safi na endelevu; Watanzania
wanataka miundombinu na usafiri wa kisasa na salama; Watanzania
wanataka miji na makazi yaliyopimwa na yaliyopangwa vizuri; na pia
Watanzania wanapenda amani, utulivu, utangamano na furaha. Hata
hivyo, napenda nisisitize kuwa Tanzania mpya ambayo wote
tunaitamani iko mikononi mwetu!!
109
97. Mheshimiwa Spika, katika kuhitimisha hotuba yangu
napenda kuwaambia Watanzania wenzangu siri ya maendeleo. Siri ya
kuifikia Tanzania mpya tunayoitamani! Kwanza, maendeleo hayaji hivi
hivi! Maendeleo yanataka dhamira na utashi, juhudi na maarifa;
maendeleo yanataka vitendo, siyo maneno! Maendeleo yanataka
pawepo dira ya kutuongoza tunakotaka kwenda. Ili kufanikiwa, lazima
kuyafahamu vizuri mazingira tulipo na njia ya kupita, hususan fursa na
hatari zilizo mbele yetu. Maendeleo yanataka mwelekeo (focus),
vipaumbele, malengo na viashiria vya hatua iliyofikiwa; maendeleo
yanahitaji nidhamu ya hali ya juu hususan katika matumizi ya
rasilimali (watu, fedha, muda, vitendea kazi na mali). Maendeleo
yanataka usimamizi makini wa utekelezaji. Hivyo, maendeleo yanataka
hatua kali za kumwajibisha yeyote anayekwamisha na kuhujumu
juhudi zetu kwa kutotimiza wajibu, uzembe, rushwa, ubadhirifu n.k.
Maendeleo yanahitaji kujinyima au kujitoa (sacrifice) na kwa maana
hiyo yafaa Watanzania tujitafakari juu ya kujengeka kwa utamaduni
wa kuchangishana michango mingi ya sherehe za anasa na badala
yake tujielekeze kusaidiana katika masuala ya maendeleo kama ada
za shule, gharama za matibabu n.k. Aidha, maendeleo yanahitaji
110
muendelezo wa hatua stahiki badala ya kurukia mambo mapya kabla
ya kukamilisha yaliyoanza kutekelezwa (consistency of action);
Maendeleo yanapatikana kwa kufanya kazi kwa bidii (hard work).
Hivyo, maendeleo hayatakuja kwa kucheza pool table na kunywa
viroba muda wote; maendeleo yanapatikana kwa kuthubutu
(boldness) na kujiamini (self confidence) na hatimaye kuamua
kujitegemea.
98. Mheshimiwa Spika, niruhusu pia niseme juu ya utegemezi
kwa misaada kutoka kwa wahisani. Tangu Uhuru wafadhili
wameendelea kutupatia misaada ambayo imetoa mchango mkubwa
katika maendeleo ya Taifa letu. Hata hivyo, pamoja na kuwa lengo la
misaada ni kujazia uwezo wa taifa kutekeleza miradi ya maendeleo au
kukabiliana na maafa, ni vizuri watanzania wenzangu tukaelewa kuwa
kwa upande mwingine misaada inaweza kuwa sumu ya maendeleo!
Misaada inaweza kuwa uchochoro wa sera na miradi mibovu,
inapoteza kujiamini na masharti yanayoambatana na misaada
yanapunguza uhuru wa kujiamulia mambo. Misaada pia inaweza
kuchochea rushwa na kuzorotesha jitihada za ndani hususan za
111
ukusanyaji mapato. Mwanazuoni anayeitwa Sebastian Edwards katika
kitabu chake – Toxic Aid: Economic Collapse and Recovery in
Tanzania (2014) amefichua ukweli huo kwa maneno yafuatayo,
nanukuu:-
“After analysing in great depth Tanzania’s history during its first two
decades as an independent nation, it is clear to me that the official aid
community had a major responsibility in one of the most colossal
collapses of a poor country in the history of the modern world. When
one adds and subtracts everything – the misguided policies, the
blunders, the growing corruption, and the socially worthwhile
projects- the balance is hugely negative. The inescapable conclusion
of that exercise is that during 1961-81 aid was worse than ineffective;
it was toxic”! Mwisho wa kunukuu.
Hivyo, ni muhimu sana kama taifa tutambue jambo hili na tufanye kila
linalowezekana kupunguza utegemezi kwa misaada ya wahisani kwa
kulinda utulivu wa uchumi, kujenga uwezo wetu wenyewe hususan
kukuza sekta ya viwanda ili kupanua wigo wa kukusanya zaidi mapato
112
ya ndani na kwa ufanisi zaidi. Ni muhimu sana tuweke msukumo zaidi
wa kukuza na kuvutia uwekezaji wa ndani na nje pamoja na
kuimarisha biashara katika mahusiano yetu na nchi rafiki.
99. Mheshimiwa Spika, jambo la mwisho na muhimu sana ni
kuwa maendeleo endelevu yanapatikana haraka katika mazingira ya
amani na usalama. Hivyo ni lazima tunu ya amani katika nchi yetu
ilindwe kwa nguvu zote.
100. Mheshimiwa Spika, Rai yangu kwa watanzania: Mungu
ametujalia rasilimali nyingi; Mama zetu walizaa na wanaendelea kuzaa
watoto wenye akili timamu, wabunifu na wenye uwezo wa kutatua
changamoto kuu na vikwazo kwa maendeleo ya Tanzania mpya.
Hivyo, tukiongozwa na uzalendo, uchungu wa nchi hii na uthubutu wa
Rais wetu Mhe. Dkt John Pombe Joseph Magufuli, lazima sasa
tudhamirie kuigeuza Tanzania kuwa nguvu kuu ya kiuchumi katika
kanda hii ya Afrika (economic power house) katika kipindi cha miaka
kumi ijayo. Tukiwa na nia moja, inawezekana, na hakika Mungu yuko
upande wetu.
113
101. Mheshimiwa Spika, ningependa pia kuchukua nafasi hii
kuwakumbusha viongozi wenzangu na wananchi kwa ujumla kuhusu
umuhimu wa matumizi ya muda ambao ni rasilimali muhimu katika
maendeleo ya Taifa letu. Watanzania wengi tunatumia muda vibaya
kwa mambo yasiyokuwa na tija na hatuzingatii muda katika kutimiza
majukumu yetu. Kwa upande wa watumishi wa umma, kumekuwa na
mazoea ya kutumia muda mrefu kwenye vikao na mikutano na kuacha
majukumu ya msingi ya kuwahudumia wananchi. Vilevile, wananchi
hasa vijana ambao ndiyo nguvu kazi ya Taifa wamekuwa wakitumia
muda mwingi wa kazi kufanya mambo yasiyokuwa na manufaa kwao
binafsi na Taifa kwa ujumla, hususan; unywaji wa pombe, kucheza
pool, uzururaji, kamari, sinema za mitaani, kukaa vijiweni na kupoteza
muda mwingi kwenye mitandao ya kijamii. Hivyo, natoa rai kwa
watanzania wote kuthamini matumizi mazuri ya muda kwa kufanya
kazi kwa bidii ili kuchochea maendeleo yetu binafsi na Taifa kwa
ujumla.
114
102. Mheshimiwa Spika, Ninapoelekea kumalizia hotuba hii,
napenda kusisitiza mambo yafuatayo ambayo yanalenga kuimarisha
ukusanyaji wa mapato na usimamizi wa matumizi ili kuweza
kutekeleza bajeti kama ilivyopangwa:
Kwanza, Serikali itaongeza msukumo katika matumizi ya mashine za
EFD ili kuhakikisha kila mfanyabiashara anatoa risiti za mashine za
EFD na wanachi wanadai risiti pale wanapofanya manunuzi ya bidhaa
au huduma. Katika kutimiza azma hii Wizara yangu itaunda Kikosi
Maalum cha kufuatilia utekelezaji wa agizo hili katika maeneo
mbalimbali ya nchi yetu ili kuhakikisha wale wote wataokiuka
utaratibu huu wanachukuliwa hatua stahiki za kisheria. Ninapenda
kutoa rai kwa viongozi wote, hususan Waheshimiwa Mawaziri,
Wabunge, Madiwani na Viongozi wa Dini kuwa mfano wa kuigwa kwa
wananchi wetu kwa kuhakikisha kuwa tunadai risiti za EFD pale
tunaponunua bidhaa au huduma. Aidha, viongozi wote mnaombwa
kuhamasisha wananchi kudai risiti za EFD. Kila asiyetoa risiti na
asiyedai risiti ajue anatenda kosa na anasaliti jitihada zetu za
kuijenga Tanzania mpya.
115
Pili, vituo vyote vya kuuzia mafuta ya petroli vinaagizwa kukamilisha
ufungaji wa mashine za EFD kwenye pampu za kuuzia mafuta hayo
ifikapo tarehe 1 Oktoba, 2016 ili kuhakisha kuwa Serikali inakusanya
kodi stahiki. Serikali itafanya ukaguzi kwenye vituo vyote vya mauzo
ya mafuta hapa nchini na kuchuka hatua za kisheria kwa wale
watakaokaidi agizo hili.
Tatu, katika kudhibiti misamaha ya kodi inayotolewa kwa
wafanyabiashara, watumishi wa umma, mashirika ya dini na taasisi
zisizo za kiserikali, kuanzia mwaka ujao wa fedha watalazimika kulipa
kodi kwanza kwa bidhaa watakazoagiza. Kodi hiyo itarejeshwa kwa
wanufaikaji baada ya ukaguzi kufanyika na kujiridhisha kuwa bidhaa
hizo zimetumika kwa malengo yaliyokusudiwa. Aidha, Serikali
itawataka wanufaika kuwasilisha maombi yao Wizara ya Fedha na
Mipango kabla ya kuagiza bidhaa husika ili kupata kibali cha uagizwaji
wa bidhaa hizo.
Nne, Maafisa Maasuuli wote wanaagizwa kutumia vifaa na mifumo ya
kielektroniki katika ukusanyaji wa mapato unaofanywa na Serikali
116
Kuu, Mamlaka za Serikali za Mitaa, na Mashirika na Taasisi za Umma
ili kuongeza ufanisi na kudhibiti upotevu wa mapato. Aidha, kodi na
tozo hizo zitakazokusanywa zipelekwe benki ndani ya masaa 24.
Tano, kuanzia mwaka ujao wa fedha utaratibu wa kubakiza sehemu
ya makusanyo, yaani mfumo wa retention umefutwa. Taasisi zote
zilizokuwa zikitumia mfumo huo zitalazimika kuwasilisha mapato yote
kwenye Mfuko Mkuu wa Serikali. Utoaji wa fedha kutoka Hazina
kwenda kwenye taasisi hizo utazingatia utaratibu wa kawaida
kulingana na bajeti iliyoidhinishwa.
Sita, Maafisa Masuuli wanaelekezwa kuzingatia agizo la Serikali la
kupunguza matumizi yasiyo ya lazima katika maeneo yaliyoainishwa
ikiwa ni pamoja na: safari za nje ya nchi, mafunzo nje ya nchi, posho
za vikao, warsha na makongamano, sherehe na maadhimisho ya
kitaifa, ununuzi wa samani, ununuzi na uendeshaji wa magari, n.k. ili
kupata fedha zaidi na kuzielekeza kwenye miradi ya maendeleo na
kutatua kero za wananchi.
Saba, Waajiri wanatakiwa kuwasilisha kodi ya mapato ya wafanyakazi
– PAYE pamoja na michango kwenye mifuko ya hifadhi ya jamii kwa
117
wakati. Aidha, kwa wale wenye malimbikizo ya PAYE na michango,
wanaagizwa kuwasilisha malipo hayo kabla ya tarehe 31 Desemba,
2016 vinginevyo hatua stahiki zitachukuliwa dhidi yao. Maafisa
Masuuli, Wakuu wa Taasisi, Mashirika na Kampuni Binafsi wanaagizwa
kusimamia utekelezaji wa agizo hili.
Nane, Maafisa Masuuli wanaelekezwa kutumia mfumo wa nakala laini
(soft copy) katika kusambaza nyaraka mbalimbali za Serikali zinazozidi
kurasa 50 isipokuwa kwa mafungu yanayotakiwa kusambaza nakala
ngumu (hard copy) kutokana na matakwa ya kikanuni/kisheria. Hatua
hii inalenga kupunguza matumizi makubwa ya gharama za kuchapisha
na kudurufu nyaraka hizo na kulinda mazingira.
Tisa, katika mwaka wa fedha 2016/17 madai yote yanayohusu
huduma za umeme, maji na simu yatalipwa moja kwa moja (centrally)
na Wizara ya Fedha na Mipango kwa kutumia bajeti za mafungu
husika. Aidha, Maafisa Masuuli wanaagizwa kulipa kwa wakati ankara
za huduma za umeme, maji na simu ili kuepuka malimbikizo ya madai
mapya.
118
Kumi, Maafisa Masuuli wanaagizwa kufanya ununuzi kwa kutumia
Hati za Ununuzi – LPOs zitokanazo na mfumo wa IFMS. Aidha,
wazabuni na watoa huduma wanaelekezwa kuhakikisha wanapatiwa
Hati za Ununuzi – LPOs zitokanazo na mfumo wa IFMS. Hivyo, kuanzia
mwaka 2016/17 Hati za ununuzi zitakazotolewa nje ya utaratibu huu
hazitatambuliwa kama hati halali za ununuzi.
103. Mheshimiwa Spika, mafanikio ya utekelezaji wa bajeti
niliyowasilisha yatategemea ushirikiano wa kila mmoja wetu ili kufikia
malengo yanayokusudiwa. Kama nilivyoeleza hapo awali, bajeti ya
mwaka 2016/17 itategemea zaidi mapato ya ndani katika utekelezaji
wake, hivyo kila taasisi ya Serikali inahimizwa kutekeleza wajibu wake
wa kusimamia ukusanyaji wa mapato ili kufikia lengo la mapato
linalokusudiwa na hatimaye kutoa huduma bora kwa wananchi wetu.
Ninaomba sote tushirikiane kwa pamoja na kila mmoja awajibike
katika nafasi yake ili tuijenge Tanzania ya viwanda.
119
104. Mheshimiwa Spika, kwa kumalizia, niwashukuru kwa dhati
wananchi wa Tanzania, hususan wakulima, wafugaji na wavuvi,
wafanyabiashara, watumishi wa umma na walioko sekta binafsi, na
Diaspora ambao wanafanya kazi kwa bidii kuchangia maendeleo ya
uchumi wa Taifa. Ninyi ndiyo nguzo/muhimili wa Taifa
linalojitegemea. Serikali inawathamini sana. Ninawashukuru pia vijana,
Taifa la kesho. Wale waliopo shuleni na vyuoni someni kwa bidii
mpate maarifa na ujuzi wa kuijenga nchi yenu. Na wale wengine
tumieni nguvu zenu na ubunifu wenu katika kilimo cha mazao ya
thamani kubwa, ufugaji, na huduma ikiwa pamoja na tasnia za
ubunifu, muziki, filamu, komedi, mitindo ambako bado kuna fursa tele
za kujipatia kipato halali ili kukidhi mahitaji ya maisha.
105. Mheshimiwa Spika, mwisho kabisa naomba kuwatambua na
kuwashukuru Washirika wetu wa Maendeleo wanaotarajia kuchangia
Bajeti ya Serikali kwa mwaka 2016/17 kama ifuatavyo: nchi za
Canada, Jamhuri ya watu wa China, Denmark, Finland, Hispania,
India, Ireland, Italia, Japani, Korea ya Kusini, Marekani, Norway,
120
Poland, Sweden, Ubelgiji, Ufaransa, Uholanzi, Uingereza, Ujerumani,
na Uswisi, pia taasisi mbalimbali za kimataifa ikiwemo Arab Bank for
Economic Development in Africa (BADEA), Benki ya Maendeleo ya
Afrika, Benki ya Dunia, Global Fund, Mashirika ya Umoja wa Mataifa,
Organisation of the Petroleum Exporting Countries (OPEC Fund),
Saudi Fund, Kuwait Fund, na Umoja wa Ulaya. Aidha, napenda
kutambua uhusiano mzuri tulionao na Shirika la Fedha la Kimataifa
(IMF) chini ya Mpango wa Ushauri wa Kisera unaojulikana kama Policy
Support Instrument (PSI). Rai yangu kwa marafiki zetu ni kuwa:
Endeleeni kutuunga mkono hususan katika jitihada zetu za kujenga
uchumi wa viwanda kwa kuwavutia wawekezaji kutoka katika nchi
zenu na kututafutia fursa za masoko ya bidhaa zetu. Mtimize ahadi
zenu kwa wakati nasi tunawaahidi kutumia michango yenu kwa ufanisi
na uwazi.
HAPA KAZI TU! MUNGU IBARIKI TANZANIA!