Soko la Hisa Laporomoka kwa Asilimia 62.

Mususa
Na Ally Daud –MAELEZO
Dar es Salaam.
Idadi ya mauzo katika soko la hisa la Dar es salaam DSE limeshuka kwa asilimia 62 kutoka shilingi bilioni 6.4 hadi kufikia shilingi bilioni 2.4 ambapo zimeuzwa na kununuliwa katika soko zimeshuka kutoka milioni 4.3 hadi kufikia milioni 2.7.
Akiongea na waandishi wa habari Meneja Miradi na Biashara waDar es salaam Stock Exchange Bw. Pawtrick Mususa alisema kuwa hata hvyo idadi ya mtaji katika soko umekuwa kutoka tilioni 21.9 hadi tilioni 22.3 ikiwa pia na idadi ya mtaji wa makampuni ya ndani imekua tilioni 9.9.
Aidha Bw. Mususa ameitaja benki ya CRDB kuwa ndiyo imeongoza kwa kuuza hisa zake katika soko ikiwa na asilimia 92 ziki fuatiwa na Kampuni ya Swissport yenye asilimia 4 na Twiga Cement ambayo ina asilimia 1.
“Kampuni ambazo zimeongoza kwa ongezeko la bei katika soko la hisa ni Kenya Airways yenye asilimia 9 pamoja na Kampuni ya bia ya East Africa Breweries ambayo ina asilimia 6 pamoja na Kampuni ya uchimbaji wa madini ya Acacia yenye asilimia 3”,alisema Bw.Mususa
Aidha Bw.Mususa aliendelea kusema kuwa viashiria vya soko vimeshuka kwa alama 41 za huduma za kibenki kutokana na kuongezeka bei ya hisa za CRDB kwa alama 3.7 ikifuatiwa na viwanda kwa alama 21 kutokana na ongezeko la bei ya hisa za TBL halikadhalika viashiria vya biashara kuongezeka kwa zaidi ya alama 40 ikiwa imechangiwa na ongezeko la bei ya hisa ya za Kampuni ya Swissport kwa asilimia 0.13,kwa ujumla kiashiria cha soko kimeongezeka kwa asilimia 54.
Mbali na hayo Meneja Mradi huyo alisema wameweza kuongeza wateja kwa kupitia huduma ya kimtandao ya DSE Mobile Trading ambayo inawawezesha kujiunga ,kununua na kuuza hisa kupitia simu ya mkononi kwa kupiga *150*36#.