Skylight Band Ndani ya Usiku Maalumu

Pichani Juu na Chini ni baadhi ya mashabiki kati ya 100 waliobahatika kuonja Shots za Tequila katika usiku maalum ulioandaliwa na SKYLIGHT BAND Ijumaa ya kwanza kwa mwaka 2013 kwa ajili ya kuwashukuru wadau na mashabiki wote wanaotoa Support kwa Band hiyo yenye miezi 4 tu tangu kuzaliwa kwake. (Picha zote na dewjiblog).

Wadau wakishow love kwenye sehemu maalum iliyoandaliwa na SKYLIGHT BAND kwa ajili ya Fans wao kupiga picha za kumbukumbu…Kutoka kushoto ni Justin Ndege, Dr. Sebastian Ndege (wa pili kulia) na Eddie pamoja na wadau wa bendi hiyo.

Ushers waliokuwa wakihudumia wateja wa SKYLIGHT Band wakipozi kupata Ukodak.

Warembo waliobahatika kuwahi siku hiyo walipata T shirts za bure kutoka SKYLIGHT BAND ila kwa wanaume walionunua hizo alizoshika Binti mrembo.

Kipaji kipya kilichotambulishwa rasmi katika usiku huo maalum wa kuwashukuru mashabiki na wadau wa SKYLIGHT BAND si mwingine ni Salma Yusuf binti mwenye kipaji cha kuimba na kupiga gitaa akitoa burudani usiku huo.

Pichani Juu na Chini ni Kikosi kazi cha SKYLIGHT BAND kikishambulia jukwaa kwa furaha isiyo na kifani katika usiku maalum wa kuwashukuru mashabiki na wadau wa Band hiyo.

Hapo Sasa twende kazi…. Sam Mapenzi sambamba na Aneth Kushaba AK47 wakionyesha ufundi wao.

Mmoja wa Fans wa SKYLIGHT BAND akilipanda jukwaani na kuomnyesha umahiri wake wa kucheza moja ya nyimbo za Band hiyo.

Hawakutoka mikono mitupu walizawadiwa Tshirts pamoja na Mvinyo kama inavyoonekana pichani.

Aneth Kushaba AK 47 kazini.

Papaaaa….Justin Ndege akimwaga noti kuwatunza SKYLIGHT BAND.

Salma Yusuf akiwajibika baada ya kutambulishwa rasmi na uongozi wa Band hiyo.

Hapo sasa mduara umekolea….Full kuzungusha nyonga.

Shabiki mwingine huyo hakuweza kuvumilia alipanda Juu ya jukwaa na kucheza ‘Carolina’ moja ya nyimbo za SKYLIGHT BAND zinazobamba mjini.

Hapo sasa….Chezea SKYLIGHT BAND wewe…..balaaaaa…!!!

Haya sasa lote lako ushindwe mwenyewe…..!!!

Sura mpya zilizojitokeza kusheherekea katika usiku maalum wa SKYLIGHT BAND kuwashukuru mashabiki wake.

Couples iliyobamba katika usiku maalum wa Ijumaa ya kwanza kwa mwaka 2013.

Blogger King Kif akiwa na Mwenyekiti wa UVCCM, Beno Malisa.

Wadau wakishow love katika usiku maalum wa kuwashukuru mashabiki wa SKYLIGHT BAND ikiwa ni miezi minne tu tangu kuanzishwa kwa Band hiyo ambayo imeonyesha kukubalika kwa Watanzania na hata raia wa kigeni.

Mkurugenzi wa Perfect Lady Saloon akiwa na Mdau kwenye usiku maalum wa kuwashukuru mashabiki wa SKYLIGHT BAND.

Mdau John Mwansasu akiwa na marafiki.

Mdau Eric Ndalu na mshikaji wake.

Picha Juu na Chini ni Sura mpya za mashabiki wa SKYLIGHT BAND wakishow love mbele ya camera yetu.

Watoto wazuri katika pozi.

Model katika pozi.

Mabloggers wakishow love John Badi (kushoto) na King Kif.