Siri ya Ushindi Vita Dhidi ya Ukimwi Katika Mlipuko wa Ebola Yatajwa
TAREHE 1 Desemba kila mwaka watu wote duniani huazimisha Siku ya Ukimwi Duniani, siku ambayo ilianzishwa mnamo mwaka 1987 na ambayo hubeba maudhui mbali mbali ikiwa kwa mwaka huu ikibeba maudhui ya Focus, Partner, Achieve: An AIDS-free Generation yaani Elekeza, Jiunge na Pata: Kizazi kisicho na Ukimwi.
Ujumbe unaokumbusha jamii kuwa ugonjwa wa Ukimwi kuwa bado ni tatizo linalohitaji jitihada endelevu na elekezi hata katika wakati wa milipuko ya magonjwa mengine katika jamii. Siku ambayo huambatana na kuunganisha watu wote katika vita dhidi ya ugonjwa wa Ukimwi wakiwakumbuka wapendwa waliowapoteza kutokana na ugonjwa huo na kuonyesha ushirikiano kwa wagonjwa waishio na virusi vya Ukimwi.
Licha ya kuwa na milipiko kadhaa katika siku za hivi karibuni ya magonjwa kama Ebola huko Afrika ya Magharibi, mlipuko wa homa ya plague nchini Madagascar, homa ya dengi nchini Tanzania na sehemu nyingie duniani, ugonjwa wa Ukimwi bado ni tishio kubwa kwa jamii hususan kwa wakati huu ambapo serikali, mashirika ya afya na utafiti na vyombo husika yanaelekeza jitihada katika kupambana na milipuko ya magonjwa hayo.
Uwezo wa wadau mbali mbali wa kuweza kukabiliana na majanga kadha wa kadha yanayoikumba jamii zetu ni siri kwa mafanikio ya kuyashinda majanga haya. Kwani athari za mlipuko kama Ebola katika sekta ya afya si za kupuuzia kutokana na ukweli kwamba huduma endelevu zinazotolewa kwa wagonjwa waishio na ugonjwa wa Ukimwi zimekuwa zikipuuziwa hivyo kuwafanya wagonjwa hao kuwa katika mazingira hatarishi.
Ni muhimu kwa watu wote hasa mamlaka husika kuzingatia na kuhakikisha kuwa waongonjwa wa Ukimwi hawanyimwi huduma zao muhimu kwa kisingizio cha milipuko ya magonjwa mapya katika jamii. Uhakiki wa upatikanaji wa vidonge vya ARV’s pamoja na njia mbadala za kuendelea kukabiliana na ugnojnwa huo havina budi kuendela kupatiwa kwa wagonjwa na kufuatwa ili kuzuia kuzorota wa kwa afya za wagonjwa wa Ukimwi na kuzuia maambukizi mapya na vifo zaidi (ii).
Hali kadhalika, katika misukosuko hii, mataifa, serikali, mashirika ya umma na yasiyo ya umma yanapaswa kuendelea kuwa thabiti na elekevu ili kukabiliana ipasavyo na kila ugonjwa sugu katika jamii. Mfano unaweza kuigwa kutoka kwa mashikirika ya afya kama Hospitali za Apollo ambayo inawakilisha mashirika yenye mikakati elekezi katika kupambana na magonjwa mbali mbali yanayokabili jamii zetu ikiwemo ugonjwa wa Ukimwi.
Hospitali za Apollo zenye msingi wake nchini India, kwa miongo mingi iliyopita zimekuwa mstari wa mbele kufanya mikakati mbali mbali dhidi ya ugonjwa wa Ukimwi ikiwemo makongamano na semina za usimamizi wa ungonjwa wa Ukimwi iliyofanywa na Hospitali za Apollo, Indraprastha na Hospitali za Apollo, Chennai.
Kupitia idara yake ya utaalamu wa ngozi na magonjwa yaambukizayo kwa zinaa, Hospitali za Apollo, Indraprastha wagonjwa wa Ukimwi waapata huduma. Hospitali imewekeza katika vifaa vya kisasa vya matibabu na huduma za magonjwa hayo (iii).
Miradi ya hospitali hizo inayohusiana na ugonjwa wa Ukimwi ikiwemo kuongeza njia mbadala za kujingika na maambukizi ya VVU, matibabu na huduma ni mfani hai wa mchango unatolewa na hospotali hizo katika kufikia maazimio ya duniania isiyo na maambukizi mapya ya VVU, kuepuka vifo vitokanavyo na ugonjwa huo na kutokuwa na unyanyapaa kwa wangonjwa wa Ukimwi.
Dk. Rajib Paul, Mganga Mshauri na mtaalamu wa huduma za vyumba vya wagonjwa mahututi (Intensive Care Unit – ICU) wa kituo cha afya cha Apollo Health City, Jubilee Hills, Hyderabad akitoa maoni jinsi ugonjwa wa Ukimwi unavyoendelea kuwa changamoto kwa sekta za afya duniani, anaonyesha pia ni kwa jinsi gani ugonjwa huo ni kikwazo kikubwa kwa maendeleo hususan kwa nchi zinazoendelea na zenye kipato cha chini.
Dk. Paul alisema pia, “Tunavyoadhimisha siku ya Ukimwi duniani, mataifa yanapaswa kuonyesha uwezo endelevu katika kukabiliana na ugonjwa huo.” Mkazo ambao unaenda sambamba na tamko lililotolewa na shirika la WHO likitaka mkazo utiliwe katika kuimairisha njia madhubuti za kujikinga, kutokomeza maambukizi mapya ya Ukimwi kwa watoto na kuongeza huduma za upimaji wa ya VVU na matibau kwa ujumla ikiwa kama sehemu ya vita dhidi ya ugonjwa wa Ukimwi.
Ugonjwa wa Ukimwi umechukua maisha ya watu zaidi ya milini 39 ikiwa kwa mwaka 2013 peke yake watu milioni 1.5 duniani wamepoteza maisha kutokana na ugonjwa huu. Pia katika mwaka huo huo takwimu zinaonyesha kuwa watu milioni 2.1 wamepata maambukizi mapya ya VVU. Hal kadhalika, watu wengi waishio na VVU wako katika nchi zinazoendela na zenye kipato cha chini. Shirika la WHO lina ripoti kuwa nchi za kusini mwa jangwa ka Sahara linafanya asilimia 70 ya maabukizi mapya ya VVU duniani katika mwaka 20143 (iv).
Akizungumza katika adhimisho ya siku ya Ukimwi duniani liliofanyika mwaka jana, Dk. Luis G. Sambo, Mkurugenzi wa shirika la WHO wa kanda ya Afrika alizungumzia maendelo muhimu yaliyofanyika kaitka vita dhidi ya ugonjwa wa Ukimwi kwenye bara la Afrika. Kumekuwa na upungufu katika vifo vitokanavyo na ugonjwa wa ukimwi kutokana na upatikanaji wa matibabu husika hali kadhalika maabukizi mapya miongoni mwa watu wazima na watoto yamepungua.
Pia wagonjwa wengi zaidi wanapata matibabu ya vidonge vya ARV. Licha ukweli kwamba mafanikio haya yanastahili pongezi lakini bado njia ni ndefu katika kutokomeza kabisa ugonjwa huu. Upatikanaji wa dawa unatakiwa kwenda sambamba na huduma bora za afya.
Mfano unaotolewa na Hospitali za Apollo ni wa kuigwa na mashirika mengine nchini Tanzania, utoaji wa huduma mbadala katika ngazi ya taifa zinazotumia njia za kisasa kabisa ambazo zitapelekea kutokomeza kabisa ugonjwa huo. Haitoshi kwa dawa na mahitaji mengineyo kupatikana tu bali kuhakikisha dawa hizo zipatikana kwa watu wenye mahitaji zaidi hususan wale wanaokuwa mbali na huduma za afya.
Katika kumalizia umuhimu wa siku hiyo, Dk. Rajib Paul anamalizia kwa kusema “Siku ya Ukimwi inatukumbusha ni kwa jinsi gani ugonjwa wa Ukimwi umechimba meno yake katika afya za mamilioni ya watu na uchumi wa familia na mataifa kwa ujumla katika kukabiliana na ugonjwa huo. Kwa hiyo ni budi kwa kila taifa na wadau kuwa na mikakati elekevu katika kukabiliana na majanga yanaoylipuka katika jamii bila kupuuzia jitahada endelevu za kukabiliana na ukimwi. Kutokana na hatua zilizopigwa na mataifa mbali mbali ikiwemo taifa la Tanzania, ni muhimu kutopoteza mwelekeo hat katika hali za dharura”.