
Mzee mwenye umri wa miaka 120 katika Kijiji cha Ngongongare, Kata ya Maji ya Chai, Ibrahim Mbise (kushoto) akimuombea baraka kimila mgombea wa CCM Jimbo la Arumeru Mashariki, Sioi Sumari, katika mkutano wa kampeni za uchaguzi mdogo wa jimbo hilo, uliofanyika katika kijiji hicho, jana. (picha na Bashir Nkoromo).

Kinamama wakimshangilia Sioi baada ya msafara wake wa kampeni kuwasili kijiji cha Ngongongare, Maji ya Chai, jana. (picha na Bashir Nkoromo).

Mfuasi wa CCM akishangilia 'kwa raha zake' kwenye mkutano wa kampeni za CCM katika kijiji cha Ngongongare. Kulia ni mmoja wa polisi ambao huwepo kuimarisha ulinzi kila mikutano ya kampeni ya vyama vinavyoshiriki uchaguzimdogo jimboni humo. (picha na Bashir Nkoromo)