Na Mwandishi Wetu
SIMBA jana imeilaza timu ya Kiyovu ya Rwanda mabao mawili kwa moja (2-1). Timu ya Simba ndio iliyokuwa ya kwanza kufungua kitabu cha magoli katika dakika ya 19 na 32 kupitia kwa mchezaji wake hatari, Felix Sunzu ambaye alipachika mabao yote mawili (2) kipindi cha kwanza cha mchezo huo uliopigwa uwanja wa Taifa Dar es Salaam.
Sunzu alifunga mabao hayo baada ya kupata pasi safi kutoka kwa mchezaji Emmanuel Okwi (Balloteli). Timu ya Kiyovu ya Rwanda ilifanikiwa kupata goli lake la kufutia machozi katika dakika 76 kipindi cha pili.
Wakati Simba ikiendelea na mashindano hayo, wenzao Yanga imeondolewa Ligi ya Mabingwa Afrika baada ya kukubali kichapo cha bila huruma 1-0 katika uwanja wa Chuo cha Kijeshi cha Miri. Yanga sasa inasukumiwa nje katika Ligi ya Mabingwa kwa kukubali kichapo cha jumla ya magoli 2-1 kufuatia mchezo wa awali kutoka sare ya 1-1 uwanja wa taifa jijini Dar es Salaam.