Simba yachwapwa 3-0 na WYDAD

Kikosi cha Simba ya Dar es Salaam

TIMU ya Simba ya Msimbazi jijini Dar es Salaam imeshindwa kuwapa raha mashabiki wake baada na Watanzania kwa ujumla baada ya kukubali kipigo cha mabao 3-0 dhidi ya WYDAD ya Casablanca nchini Morocco.

WYDAD ilianza kuharibu furaha ya mashabiki wa simba katika dakika ya 88 ilipoandika bao la kwanza na 89 bao la pili na kukandamiza bao la tatu tena katika dakika ya 91 kabla ya kumalizika kwa mchezo huo.

Mechi hiyo ambayo ilikuwa ya kuwania kufuzu hatua ya makundi katika Ligi ya Mabingwa Afrika, Simba ilijitahidi kucheza vizuri lakini ilianza kujichanganya katika dakika za mwisho ndipo ilipoanza kuchapwa mabao hayo mfululizo.