Simba Yabanwa na Mwadui Shinyanga

majabvi-na-awadhi-juma-simba_1vqp59jybdgxh1wdfyp7ql7z1p
Ligi kuu Tanzania bara iliendelea tena jana kwa michezo kadhaa kupigwa kwenye viwanja tofauti na kushuhudia matokeo tofauti katika viwanja hivyo kwa baadhi ya timu kuibuka na pointi tatu huku zingine zikishindwa kabisa kutamba.

Simba imezidi kujiweka kwenye wakati mgumu wa kuwa moja kati ya timu inayopigania ubingwa msimu huu baada ya kulazimishwa sare ya 1-1 na Mwadui FC.

Hiyo ni sare ya tatu mfululizo kwa Simba ambayo tangu kuendelea kwa ligi baada ya kusimama kwa mwezi mmoja haijaonja ladha ya ushindi zaidi ya matokeo ya sare.

Simba ilianza kutoka sare ya 2-2 na Azam FC, uwanja wa taifa na baada ya hapo Jumamosi iliyopita ilipata sare ya 1-1, na Mwadui FC, uwanja wa CCM Kirumba na leo ikapata matokeo kama hayo uwanja wa Kambarage.

Sare hiyo imeifanya timu hiyo inayofundishwa na kocha Muingereza Dylan Kerr, kufikisha pointi 25, katika michezo 12, iliyocheza na matokeo hayo yanaiweka pabaya ajira ya kocha huyo.

Kiungowa zamani wa Yanga na timu ya taifa ya Tanzania Nizar Khalfan alianza kuwaeka mbele wenyeji Mwadui FC, kwa bao safi alilofunga dakika ya 77 na kufufua matumaini ya mashabiki wa timu hiyo kupata ushindi wa tatu mfululizo.

Lakini wachezaji wa Simba waliendelea kupambana kwa kucheza kwa nguvu na zikiwa zimesalia dakika nne mpambano huo kumalizika winga wa kimataifa kutoka Uganda Briani Majwega aliisawazishia timu hiyo bao dakika ya 86 na kufanya hadi mapumziko matokeo kuwa sare ya 1-1.
Matokeo Mengine
Mwadui FC 1-1 Simba
Ndanda FC 1 – 3 JKT Ruvu
Coastal Union 1 – 3 Stand United
Maji Maji FC 0 – 2 Prisons
Yanga 3- 0 Mbea City
Mtibwa Sugar 3-0 Mgambo JKT