Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam
TIMU ya Simba imemua kuweka kambi ya muda huko Loliondo mkoani Arusha ili kusaka tiba ya kuiangamiza timu ya TP Mazembe.
Simba inatarajia kukutana na TP Mazembe mabingwa wa Afrika mara mbili mwishoni mwa mwezi huu huo ukiwa ni mchezo wa awali wa Klabu Bingwa Afrika.
Akizungumza na Mtanzania, Katibu Mkuu wa timu hiyo, Evodius Mtawala alisema bado wanahangaikia utaratibu wa safari ikiwa pamoja na suala nzima la tiketi za wachezaji.
“Bado tupo tupo hapa Arusha kwa ajili ya kukamilisha taratibu mbalimbali na tunatarajia kurejea Dar es Salaam siku ya Alhamisi, kwa sasa hatuwezi kusema ni lini tunawafuata TP Mazembe,” alisema Mtawala.
Kauli hiyo ya Mtawala imekuja pengine kutokana na Watanzania wengi kwa sasa akili na mtazamo wao kuwa huko Loliondo kutokana na Mchungaji
Ambilikile Mwasapile kuendelea kugawa dozi kwa magonjwa sugu.