TIMU ya Simba SC imeendelea kufanya vizuri katika michezo ya Ligi Kuu Bara na kubaki kileleni baada ya kuibugiza tena Timu ya Kagera Sugar mabao 2-0. Katika mchezo huo uliopigwa kwenye dimba la Uhuru ‘Shamba la Bibi’ magoli ya Mzamiru Yassin na Shiza Kichuya yameikifikishia timu ya Simba jumla ya pointi 23 baada ya kuingia dimbani mara 9.
Mzamiru Yassin alianza kuifungia Simba goli lake la kwanza katika dakika ya 43 kipindi cha kwanda akiunganisha kwa kichwa mpira wa kona uliopigwa na Shiza Kichuya. Simba ikafanikiwa kwenda mapumziko ikiwa mbele kwa bao 1-0 dhidi ya wapinzani wake Kagera Sugar. Kichuiya akapachika bao la pili dakika 75 kwa mkwaju wa penati baada ya Ibrahim Mohamed kuangushwa kwenye eneo la hatari la Kagera Sugar.