SIMBA SC imebisha hodi Nusu Fainali ya Kombe la Mapinduzi, kufuatia ushindi wa bao 1-0 dhidi ya URA ya Uganda katika mchezo wa Kundi A jana usiku huu Uwanja wa Amaan, Zanzibar.
Ibrahim Hajib Ndiye aliyefunga bao hilo pekee dakika ya
37 kwa shuti lake la umbali wa mita 20, baada ya kupokea pasi ya beki Mrundi, Emery Nimubona.
Simba SC inapanda kileleni mwa Kundi A baada ya kufikisha pointi nne, kutokana na mechi mbili, ikifuatiwa na URA yenye pointi tatu sawa na JKU, wakati Jamhuri wanashika mkia kwa pointi yao moja.
Simba SC, mabingwa watetezi wa Kombe hilo, ilistahili ushindi katika mchezo wa huo, kutokana na kucheza kwa umakini na nidhamu ya hali ya juu, kiasi cha kuwadhibiti kabisa URA.
Michuano hiyo itaendelea leo kwa mechi za Kundi B kuhitimishwa, Azam FC wakimenyana na Mafunzo, wakati Yanga SC watamenyana na Mtibwa Sugar usiku. Simba SC itamaliza na JKU kesho, wakati URA itamaliza na Jamhuri.
Wakati huo huo Timu ya JKU imeisambaratisha timu ya Jamhuri kutoka Pemba kwa magoli 3-0 kwenye mchezo wa Kundi A. JKU wamepata Mabao yao kupitia kwa Emanuel Martin aliyepachika bao la kwanza dakika ya tatu ya mchezo kipindi cha kwanza. Goli la pili la JKU limefungwa na Nassor Matar dakika ya 35 kipindi cha kwanza wakati Mohamed Abdala aliifungia JKU goli la tatu kukamilisha ushindi kwa timu yake.
Makundi, Mtokeo na Ratiba Ya Michuano Hiyo
Kundi A: Simba SC, Jamhuri, JKU, URA
Kundi B: Yanga SC, Mafunzo, Azam FC, Mtibwa Sugar
(Mechi zote zitachezwa Uwanja wa Amaan, Zanzibar)
Jan 3, 2016
Yanga SC 3-0 Mafunzo
Mtibwa Sugar 1-1 Azam FC (Saa 2:15 usiku)
Jan 4, 2016
JKU 1-3 URA (Saa 10:15 jioni)
Simba SC 2-2 Jamhuri Saa 2:15 usiku)
Jan 5, 2016
Mafunzo 0-1 Mtibwa Sugar (Saa 10:15 jioni)
Azam FC 1-1 Yanga SC (Saa 2:15 usiku)
Jan 6, 2016
Jamhuri 0-3 JKU (Saa 10:15 jioni)
URA 0-1 Simba SC (Saa 2:15 usiku)
Jan 7, 2016
Azam Vs Mafunzo (Saa 10:15 jioni)
Mtibwa Sugar Vs Yanga (Saa 2:15 usiku)
Jan 8, 2016
Jamhuri Vs URA (Saa 10:15 jioni)
Simba SC Vs JKU (Saa 2:15 usiku)
NUSU FAINALI
Jan 10, 2016
FAINALI
Jan 13, 2016 (Saa 2:15 usiku)