Simba SC Kuvuna Bilioni 20 Leo Kwa Dewji

5
Klabu ya Simba ilikuwa imepewa siku mbili hadi kufikia leo Disemba 31,kuamua mpango wake wa kukubali dau la bilioni 20, kwa ajili ya mfanya biashara mkubwa nchini Mohamed Dewji, kuwekeza na kuiendesha klabu hiyo inayokabiliwa na ukata wa fedha kwa sasa.

Dewji anautaka uongozi wa Simba chini ya Rais Evans Aveva waamue moja kama wako tayari au la na ikipita siku ya Leo kama hawatafanya maamuzi yeye hatoendelea tena na mpango huo na badala yake ataendelea na biashara zake.

Tajiri huyo aliyewahi kuifadhili timu hiyo miaka ya nyuma anataka kuwekeza kiasi hicho cha pesa kwa nia ya kuiendesha kibiashara klabu hiyo kongwe kabisa Afrika.
mohamed-dewji-huyo-mwenye-jezi-nyekundu_1kexgt5hvoxia1jsh7onnces39
“Nilikutana na viongozi wa Simba akiwemo Rais Aveva na Kassim Dewji na Musley Ruhwehi na nimewaeleza dhamira yangu lakini kimwonekano kama hawakuwa tayari kuona klabu hiyo inaendeshwa kibiashara kwasababu wapo kimya hawakuweza kumpa jibu na na ndiyo maana nimetoa muda huo,”amesema Dewji.

Dewji amesema chini ya uwekezaji atakaofanya atajenga Kiwanja cha Bunju na kuwa Kiwanja maalum cha mazoezi ya klabu hiyo na pia kama kituo maalum cha kulea vipaji vya soka kwa vijana ambao baadaye watachezea timu hiyo ya SIMBA.
6
Anasema mipango yote hiyo tayari amewaeleza viongozi wa Simba chini ya Rais Aveva lakini akashangaa mpaka sasa viongozi hao wamekuwa hawanyooshi maneno na badala yake wanasema bado hawajapata barua rasmi kutoka kwake.

Tajiri huyo amesema anataka mpango huo uanze haraka iwezekanavyo ikibidi Januari ili kuanza pia mchakato wa kutuma mascout kusaka wachezaji watakaochezea Simba baada ya kumalizika kwa Ligi hii inayoendelea.