Uongozi wa klabu ya Simba SC umevunja mkataba na aliyekuwa kocha mkuu wa kikosi cha ‘wana Msimbazi’ Dylan Kerr kwa baada ya makubaliano ya pande zote mbili na kufikia uamuzi huo.
Makamu Mwenyekiti wa Simba SC Geofrey Ntyange ‘Kaburu’ amesema pande zote mbili (Simba SC na kocha Dylan Kerr) wamekubaliana kuvunja mkataba baada ya kukaa na kujadiliana kwa kirefu.
“Tumevunja mkataba na Kerr kwa makubaliano ya pande mbili baada ya kukaa na kujadiliana hatimaye tukafikia uamuzi huo”, amesema Kaburu ambaye alikuwepo Zanzibar akishuhudia mchezo kati ya Simba dhidi ya Mtibwa Sugar ambao Simba ilitupwa nje ya mashindano ya Mapinduzi katika hatua ya nusu fainali.
Katika hatua nyingine, kocha mpya wa klabu hiyo Jackson Mayanja ambaye amesaini mkataba na klabu hiyo siku chache zilizopita kama kocha msaidizi atachukua mikoba ya Kerr kwa muda wote ambao Simba itakuwa ikifanya mchakato wa kumpata mrithi wa Kerr.
Jana asubuhi Dylan Kerr ali-tweet kwenye account yake ya twitter ujumbe ambao ulikuwa tafsiri nyingi kabla ya kuondoka visiwani Zanzibar kuelekea jijini Dar es Salaam ambapo inasemekana aliitwa kwa ajili ya kikao maalum na viongozi wa klabu ya Simba.
Huu hapa ni ujumbe ambao alipost kocha huyo muda mfupi kabla hajaiacha ardhi ya Zanzibar na kurejea jijini Dar.
REKODI YA DYLAN KERR SIMBA SC;
Jumla ya Mechi; 30
Mechi alizoshinda; 19
Mechi alizofungwa; 5
Mechi alizotoa sare; 6
MATOKEO YA MECHI ZA SIMBA SC CHINI KERR;
Simba SC 2-1 Zanzibar Kombaini (Kirafiki Zanzibar)
Simba SC 4-0 Black Sailor (Kirafiki Zanzibar)
Simba SC 2-0 Polisi (Kirafiki Zanzibar)
Simba SC 3-0 Jang’ombe Boys (Kirafiki Zanzibar)
Simba SC 3-2 KMKM (Kirafiki Zanzibar)
Simba SC 1-0 SC Villa (KIrafiki Simba Day)
Simba SC 2-1 URA (Kirafiki, Dar es Salaam)
Simba SC 0-0 Mwadui FC (Kirafiki, Dar es Salaam)
Simba SC 0-2 JKU (Kirafiki Zanzibar)
Simba SC 3-1 JKU (Kirafiki Zanzibar)
Simba SC 0-0 KVZ (KIrafiki Zanzibar)
Simba SC 1-0 African Sports (Ligi Kuu Mkwakwani)
Simba SC 2-0 JKT Mgambo (Ligi Kuu Tanga)
Simba SC 3-1 Kagera Sugar (Ligi Kuu Taifa)
Simba SC 0-2 Yanga SC (Ligi Kuu Taifa)
Simba SC 1-0 Stand United (Ligi Kuu Taifa)
Simba SC 1-0 Mbeya City (Ligi Kuu Mbeya)
Simba SC 0-1 Prisons (Ligi Kuu Mbeya)
Simba SC 1-0 Coastal Union (Ligi Kuu Mbeya)
Simba SC 6-1 Majimaji FC (Ligi Kuu Taifa)
Simba SC 5-2 Kimbunga FC (Kirafiki Zanzibar)
Simba SC 2-2 Azam FC (Ligi Kuu Taifa)
Simba SC 1-1 Toto Africans (Ligi Kuu Kirumba)
Simba SC 1-3 Geita Gold Mine (Kirafiki Geita)
Simba SC 1-1 Mwadui FC (Ligi Kuu Kambarage)
Simba SC 1-0 Ndanda FC (Ligi Kuu Nangwanda)
Simba SC 2-2 Jamhuri FC (Kombe la Mapinduzi)
Simba SC 1-0 URA FC (Kombe la Mapinduzi)
Simba SC 1-0 JKU FC (Kombe la Mapinduzi)
Simba SC 0-1 Mtibwa Sugar (Nusu Fainali Kombe la Mapinduzi)