Siku ya Wakunga Duniani Mikono ya Kwanza Kukupokea Duniani

“Takwimu zilizochapishwa na ripoti ya Hali ya Wakunga Ulimwenguni (State of the World’s Midwives) zinaonyesha kuwa Tanzania inahitaji wakunga 9,941 zaidi ili kufikia lengo ifikapo mwaka 2015 la kuwa na asilimia 95% ya wajawazito wanaozalishwa na wahudumu wenye taaluma.”
Akinamama 5,000 na watoto wachanga 32,000
 wangeweza kuokolewa ifikapo 2015

TANZANIA inawahitaji wakunga sasa, kuliko wakati mwingine wowote ule
Akinamama 5,000 na watoto wachanga 32,000 wangeweza kuokolewa ifikapo 2015
Mama Ye! leo, Mei 5, inatoa wito kwa Mh. Dk Hussein Mwinyi (MB), Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii,
kushughulikia kwa haraka upungufu wa idadi ya wakunga wanaohitajika ili kuwasaidia akina mama wa
Tanzania kujifungua salama.
Wakunga wana jukumu kubwa la kuwahudumia wanawake katika kipindi chote cha ujauzito na pia ni
wataalamu wenye ujuzi wa kushughulikia matatizo yanayoweza kujitokeza wakati wa kujifungua.
Wakunga wengi wanatembea umbali mrefu na kufanya kazi masaa mengi ili watoe huduma bora kwa
wanawake katika jamii zao. Wataalamu wa masuala ya afya ya wajawazito na watoto wachanga
wamekadiria kuwa, iwapo wanawake wote wa Tanzania wangepata huduma za wakunga wenye ujuzi,
basi maisha ya akinamama wapatao 5,000 na vichanga 32,000 yangeweza kuokolewa ifikapo 2015.
Akiongea kwa niaba ya kampeni ya Mama Ye! Craig Ferla amesema: “Ni vyema kabisa kuwaenzi
wakunga wetu katika Siku ya Wakunga Duniani. Tunapongeza ahadi za serikali kuitilia mkazo sera ya
huduma za afya ya uzazi kuwa bure, lakini mengi bado yanahitaji kufanyika ili kuongeza idadi ya
wahudumu wa afya.”
Takwimu zilizochapishwa na ripoti ya Hali ya Wakunga Ulimwenguni (State of the World’s Midwives)
zinaonyesha kuwa Tanzania inahitaji wakunga 9,941 zaidi ili kufikia lengo ifikapo mwaka 2015 la kuwa na
asilimia 95% ya wajawazito wanaozalishwa na wahudumu wenye taaluma.
Craig Ferla ameongeza kuwa: “Tunawaalika na kuwahimiza Watanzania kutoa shukrani kwa wakunga –
na kusaidia kuwapa moyo vijana nao waamue kuwa wakunga siku za baadae. Unaweza kufanya hivyo
kwa kutumia ‘Twitter’ ukiwaambia asante kwa kujituma kazini, pia waweza kuweka picha kwenye
ukurasa wetu wa ‘Facebook’ zinzazowaunga mkono wakunga wetu wa Tanzania pamoja na mathalan
kutambua juhudi kubwa za mkunga unayemthamini kwa kazi zake kubwa katika jamii yako.”
Ukitaka kufahamu zaidi kuhusiana na hali ya wakunga nchini Tanzania, tembelea tovuti ya
www.mamaye.or.tz/sw ambapo utapata ushahidi uliowekwa kwa namna rahisi kuelewa, habari kuhusu
mashujaa katika uzazi salama, ahadi zilizowekwa na serikali na hatua mbali mbali unazoweza kuchukua