Shuhudia Pambano la Ngumi Kati ya Mabondia wa Kenya na Tanzania

Shuhudia Pambano la Ngumi kimataifa Kati ya Mabondia wa Kenya na Tanzania. Tamasha la kimataifa la ngumi litakalofanyika mkoani Mtwara katika Ukumbi wa Makonde Beach Resolt. Tamasha litasimamiwa na Oganaizeni ya Ngumi za Kulipwa Tanzania (TPBO), na maandalizi ya tamasha yanaendelea vizuri huku bondia Patrick Amote wa Kenya anatarajia kuwasili Tanzania Oktoba 23, 2012 tayari kuanza safari ya kuelekea mkoani Mtwara Oktoba 24, 2012.