Show ya Jay dee na Kiba Yabamba

Tumefunika mbaya mtu wangu....ndio ishara waliyokuwa wakipeana Ali Kiba na Lady Jay Dee.

Tumefunika mbaya mtu wangu….ndio ishara waliyokuwa wakipeana Ali Kiba na Lady Jay Dee.

DSC_0035

Mwanamuziki Lady Jay Dee akitoa burudani na Machozi Band Ijumaa ya tarehe 27 mwezi huu ndani ya kiota chake cha Mog Bar & Restaurant (Nyumbani Lounge) katika show anazofanya mara moja kwa mwezi kila Ijumaa ya mwisho wa mwezi ambapo Ijumaa hiyo alimualika Msanii machachari wa Bongo Flava Ali Kiba kwa ajili ya kukonga nyoyo za mashabiki wake ndani ya kiota hicho.

DSC_0033

DSC_0058

Vijana watanashati wenye vipaji vya aina yake wa Machozi Band wakipiga Back Vocal kumpa sapoti Lady Jay Dee a.k.a Komando Binti Machozi. Kutoka kushoto ni Faraja, Omirady pamoja na Chiqitita.

DSC_0089

Pichani juu na chini ni mashabiki wa Machozi Band wakimtunza manoti Lady Jay Dee.

DSC_0083

DSC_0078

DSC_0046

Umati wa mashabiki wa Machozi Band wakipata burudani kutoka kwa band hiyo inayoongozwa na Lady Jay Dee.

DSC_0048

DSC_0065

DSC_0066

DSC_0204

Msanii nyota nchini, Ali Kiba akitoa burudani ya aina yake ndani ya kiota cha M.O.G Bar & Restaurant baada ya kutikia mualiko wa msanii mwezake Lady Jay Dee na kufanya Live Music bila kutumia CD na kuwafanya mashabiki kupagawa zaidi.

DSC_0217

Ali Kiba akiendelea kuwaburudisha mashabiki wake Machozi Band.

DSC_0219

Warembo walipagawajem sasa.

DSC_0248

Twende kazi hapo sasa.

DSC_0253

Mrembo akijinafasi kwa Ali Kiba.

DSC_0275

#ChekechaCheketua…….Wadada wakichizika na mauno ya Ali Kiba na style yake mpya.

DSC_0283

Mwanadada hakukubali kabisa na kuamua kupanda jukwaani kulipiza mauno ya Ali Kiba.

DSC_0284

Picha inajieleza jinsi Ali Kiba alivyokonga nyoyo za mashabiki wake.

DSC_0296

Lady Jay Dee: Nimemkuta analia, kajilaza, sababu amechoka…..Mengi amevumilia, yalomkwaza, anataka kuondoka….ana siku ya pili sasa, hajarudi nyumbani kulala,…namuonea huruma sana, haya….mapenzi hayana maana

Lady Jay Dee: who the single girl…..who the single boy, Ali Kiba: i am a single boy…….Ali Kiba: who the single girl, …….Lady Jay Dee: i am a single girl…….Lady Jay Dee: who the single boy, Lady Jay Dee na Ali Kiba:.…mi na we single boy

 

DSC_0281

DSC_0256

DSC_0010

Binti mrembo binti kwenye kipaji Faraja wa Machozi Band akiwapa raha mashabiki wa Band hiyo Ijumaa ya mwisho wa mwezi huu ndani kiota cha Mog Bar & Restaurant (Nyumbani Lounge).

DSC_0142

Mkali wa Reggae na Dance Hall nchini Double D akiwarusha mashabiki wake ndani ya kiota cha M.O.G Bar & Restaurant.

DSC_0158

Mkali wa Reggae na Dance Hall nchini Double D katika hisia kali za kuwapa raha mashabiki wake.

DSC_0144

Vijana wakijiachia vilivyo baada ya Reggae za Double D kuwakolea ndani ya kiota cha M.O.G Bar & Restaurant.

DSC_0170

Omirady wa Machozi Band akitoa burudani kwa mashabiki wa Band hiyo katika show inayopigwa mara moja kwa mwezi na kuwateka mashabiki wengi ndani ya kiota cha M.O.G Bar & Restaurant.

DSC_0015

Msanii Chiqitita wa Machozi Band akitoa burudani kwa mashabiki wa band hiyo (hawapo pichani).

DSC_0059

Mashabiki wa machozi band wakipata Ukodak.

DSC_0193

Sehemu ya umati wa mashabiki wa Live Band uliofurika Ijumaa ya mwisho wa mwezi huu ndani ya M.O.G Bar & Restaurant kushuhudia show ya wakali wa muziki nchini Lady Jay Dee na Ali Kiba.

DSC_0001

Hawa jamaa ndio wanaohakikisha Lady Jay Dee anakuwa salama siku zote.