Shoo ya Usiku wa Mtu Mzima Dawa Mwanza

Mmoja wa wasanii wa muziki wa kizazi kipya atambulikae kwa jina la kisanii Ommy Dimpo akijiachia jukwaani na mmoja wa mashabiki waliyejitokeza kucheza  nae,kwenye shoo ya Usiku wa Mtu mzima Dawa uliofanyika kwenye kiota cha maraha cha Villa park usiku wa kuamkia leo,jijini Mwanza.Aidha katika makamuzi hayo washabiki wapenzi wa muziki wa kizazi kipya walijaa ile mbaya na palikuwa hapatoshi hata kidogo.
Wacheza shoo wa Ommy Dimpoz wakiwajibika jukwaani.
wasanii wa kundi la Wanaume TMK wakiongozwa na Chege na Temba wakilishambulia jukwaa vilivyo,ama kwa hakika ilikuwa ni shangwe tu kwenye makamuzi ya shoo ya Usiku wa Mtu mzima dawa.
Wasanii Chege na Ydash wote kutoka Wanaume TMK wakiwarusha wakazi wa Mwanza ni kibao chao cha Dar mpaka Moro.

Wanaumeeee…eeeeeh..! Wanauuumeeeee…..halafu mashabiki wanaitikia kwa nguvu kabisa eeeehhhh..!

“Sijui nimtawanyee…..aah huwezi wewe mtu mzima dawa.”! Mh Temba akikamua vilivyo na Bibi Cheka jukwaai saafi kabisa huku shangwe zikiwa zinasikika kila kona,kwani Bibi Cheka alionesha uwezo wake mkubwa wa kukamua jukwaa,hata ile mitindo huru nini na niniii yuko swafi mbaya..aaah mbona palinoga Villa Park usiku wa kuamkia leo.
Ommy Dimpoz akikamu mbele ya umati mkubwa ndani ya kiota cha maraha cha Villa Park usiku wa kuamkia leo.

Watu kibao walifurika ndani ya ukumbi wa Villa Park kushuhudia Usiku wa mtu mzima dawa.

Pamoja na kupotea kiaina kwenye gemu ya muziki wa Bongofleva,Ferouz bado nyota yake inaonekana kuwa angavu,alifanya vyema ndani ya ukumbi wa Villa Park,kiasa kwamba shangwe kila wakati zilikuwa za kutosha.
Mkubwaa na wanaweee….na yeyeee yumooo.. ! Mkubwa Fella nae akitafuta kimwana wa kunogesha jukwaa safi kabisa.
Msanii mahiri wa hip hop hapa nchini,Mwana FA akikamua kitu cha laiti na shabiki wake jukwaani kama picha ionekavyo.
Mkali mwingine wa mitindo huru,Mwana FA a.k.a Binadamu akikamua vilivyo ndani ya ukumbi wa Villa Park usiku wa kuamkia leo,kwenye shoo ya usiku wa mkubwa dawa ambao ulifana kwa kiasi kikubwa.Picha zote na  Michuzijr.Blogspot.com