Na BMG
Benedicto amesema Mradi wa Sauti ya Watoto Wafanyakazi wa nyumbani umelenga kuhamasisha jamii kuondoa aina zote za unyanyasaji na unyonyaji dhidi ya watoto wafanyakazi wa nyumbani ambapo wanajamii watajengewa uelewa juu ya vitendo vyote vya unyanyasaji na unyonyaji vinavyomuathiri mtoto mfanyakazi wa nyumbani ili kushiriki katika kuvitokomeza.
Aidha ameongeza kwamba mradi huo utaongeza ushiriki wa mtoto mfanyakazi wa nyumbani katika kujilinda dhidi ya aina zote za unyanyasaji na unyonyaji ambapo unaambatana na ujumbe usemao “Saidia kutokomeza ukatili, unyanyasaji na unyonyaji dhidi ya watoto wafanyakazi wa nyumbani”.
Katika mradi huo ambao ni wa muda wa miezi sita, wananchi wataweza kutoa taarifa za ukatili na unyanyasi kwa watoto wafanyakazi wa nyumba kwa kupiga simu nambari 0800 71 00 60 bure kabisa.
Wadau waliohudhuria kwenye utambulisho wa mradi huo ni pamoja na Madiwani, Watendaji wa Kata na Mitaa, Wenyeviti wa mitaa, maafisa maendeleo ya jamii, waajiri wa watoto wa nyumbani, watoto waajiriwa wa nyumbani, mawakili, maafisa kazi, maafisa elimu kata, wawakilishi wa dawati la jinsia kutoka vyombo vya ulinzi pamoja na kamati za ulinzi na usalama wa mtoto ambapo wameahidi kutoa ushirikiano wao ipasavyo ili kufikia malengo.
Mwakilishi wa Mkuu wa Wilaya ya Nyamagana, Zubeda Kimaro, akifungua mkutano wa kutambulisha mradi wa “SAUTI YA WATOTO WAFANYAKAZI WA NYUMBANI” utakaofanya kazi kwenye Kata za Igogo, Mkuyuni, Butimba na Nyamagana Jijini Mwanza.
Amelipongeza shirika la WOTESAWA kwa kazi nzuri ya kutetea haki za watoto wafanyakazi wa nyumbani na kuhakikisha kwamba ukatili dhidi yao unatokomezwa kabisa.
Jaqueline Ngalo Mwanasheria kutoka shirika la WOTESAWA akizungumza kwenye mkutano huo.
Baadhi ya washiriki wa mkutano wa kutambulisha mradi wa “SAUTI YA WATOTO WAFANYAKAZI WA NYUMBANI” utakaofanya kazi kwenye Kata za Igogo, Mkuyuni, Butimba na Nyamagana Jijini Mwanza.
Mradi wa Sauti ya Watoto Wafanyakazi wa Nyumbani umefadhiriwa na Taasisi ya The Foundation For Civil Society.
Katika mradi huo ambao ni wa muda wa miezi sita, wananchi wataweza kutoa taarifa za ukatili na unyanyasi kwa watoto wafanyakazi wa nyumba kwa kupiga simu nambari 0800 71 00 60 bure kabisa.