Shirika la USAID wazindua filamu ya TUNU

 

shirika la watu wa marekani USAID limezindua filamu ya TUNU  ambayo ni Kiswahili ikiwan imechezwa na waigizaji wa kitanzania, huku ikiwa na lengo la kuleta ujumbe muhimu na wa kipekee katika vipaumbele vilivyoko nchini Tanzania.

 

Uzinduzi huo umefanyika katika ukumbumbi wa sinema wa suncrest Cineplex Cinema uliopo Quality Center jijini Dar es salaam ambapo kuliudhuriwa na wageni mbalimbali.

vilamu hii ndani yake kuna muigizaji nguli nchini Tanzania Jacob Stephen, Ibrahim Oswald, Martin White(Tin White) na wengineo, filamu hiyo imeandaliwa na taasisi ya Media for development International chini ya director maarufu na mkongwe John Riber ambaye aliongoza filamu kama Neria na Yellow Card.

USAID/Tanzania inasaidia kampeni hii maalumu ya kuhamasisha wanawake na vijana kuona fursa adimu katika kilimo kupitia sanaa. Ni moja wapo ya juhudi kubwa zinazofanywa na serikali ya marekani katika kupunguza uhaba wa chakula duniani na kuwezesha usalama wa chakula kupitia mpango wake wa “Feed the future”

Sekta ya kilimo ya Tanzania ina mashujaa wengi wa kila siku. Wakulima wadogo-wadogo wanaongoza katika orodha hii. Kutoka Morogoro hadi Mbeya, wakulima wadogo-wadogo hupitia mambo mbali-mbali kila siku na wao ndio nguvu ya nyuma inayosukuma sekta ya kilimo nchini. Wakulima wanawake na vijana hasa, ndiyo kitovu cha kilimo cha kuleta faida na cha baadae nchini Tanzania, lakini bado huachwa nyuma katika mlinganisho wa kilimo.

Sekta ya kilimo nchini Tanzania inatoa ajira kwa zaidi ya asilimia 75 ya wananchi, huku nguvu-kazi kubwa ikitoka kwa wanawake na vijana. Vijana wanawakilisha karibia theluthi ya nguvu-kazi katika kilimo.

Ingawa wanawake na vijana wanachangia kwa kiasi kikubwa kutoa nguvu-kazi ya kilimo nchini Tanzania, maamuzi juu ya kilimo mara nyingi hutolewa au kufanywa na wanaume. Taratibu zisizofaa na desturi za kijamii na kitamaduni zenye upendeleo huathiri uzalishaji katika kilimo kwa kuweka vizuizi kwa wanawake kuzifikia rasilimali kama vile mafunzo, mitaji/fedha, vitendea kazi na haki ya kumiliki ardhi. Na ingawa vijana wa leo ndiyo watakaoleta mabadiliko katika usalama wa chakula Tanzania huko mbeleni, kutokana na sababu mbali-mbali, vijana wengi wa Kitanzania hukimbia vijiji vyao na kwenda kutafuta fursa nyingine za kazi mijini.

Kwa kutambua mchango mkubwa unaoletwa na wanawake na vijana katika maendeleo ya kiuchumi ya Tanzania, Shirika la Misaada ya Kimataifa la Marekani (USAID) nchini Tanzania linatoa kipaumbele katika kuwawezesha wanawake na vijana wa Kitanzania katika mpango wake wa miaka mitano. Hii inajumuisha shughuli za uwezeshaji kupitia mpango wa kupatia watu chakula kwa baadae wa Serikali ya Marekani (Feed the Future), ambao unaboresha sekta ya kilimo na kutengeneza fursa kwa wanawake na vijana vijijini.