Shindano la Maisha Plus 2013 Lazinduliwa

Mkuu wa Wilaya ya Mvomero, Anthony Mtaka Akimkabidhi fomu ya Ushiriki wa Maisha plus kwa vijana Bi. Shamimu Ramadhani.

Mkuu wa Wilaya ya Mvomero, Anthony Mtaka Akimkabidhi fomu ya Ushiriki wa Maisha plus kwa vijana Bi. Shamimu Ramadhani.

 
Mkuu wa Wilaya ya Mvomero Mh. Anthony Mtaka, Akizungumza pamoja na wakazi wa eneo la Kingolwira pamoja na wageni mbalimbali waliotoka sehemu mbalimbali Tanzania na kutoa tamko rasmi la  kuzindua  shindano la Maisha Plus/ Mama shujaa wa chakula 2013
Mama Shujaa wa Chakula 2012 Sister Matha Mwasu aliyeshika nafasi ya kwanza , Akizungumza katika uzinduzi rasmi wa Maisha Plus/Mama Shujaa wa Chakula 2013, pia akieleza Jinsi alivyoweza kushinda na kupata mafanikio makubwa kutoka katika shindano la kizalendo la Maisha Plus.
 Mshindi wa Shindano la Maisha Plus Bernick Kimiro akizungumza na wageni wa alikwa pamoja na wenyeji wa eneo la Kingolwira Morogoro, kwa kuwasisitiza vijana wajitokeze kuchukua fomu za ushiriki katika shindano la Maisha Plus/ Mama Shujaa wa Chakula 2013 ambazo sasa zimesha anza kutolewa na kuwaeleza kuwa shindano hilo linatoa Fursa nyingi za kimaendeleo na kilimo kwa ujumla.
Dr. Emmanuel Tumusiime kutoka OXFAM akifanya uzinduzi rasmi wa Ripoti ya ‘Feed the Future Initiative in Tanzania’ ambapo katika ripoti hiyo kuna mambo ya msingi ya kulinda chakula kisije kikaja kuisha na Taifa likaja kukosa kabisa siku za mbeleni.
 
 
Kutoka Kulia ni Mshindi wa Pili wa wa Maisha Plus Venance Mushi akiwa na Mama shujaa wa chakula wa kwanza wa mwaka 2011 Bi. Ester Mtegule pamoja na Aliyekuwa mshiriki wa Maisha Plus/ Mama Shujaa wa chakula 2011 Bi. Dora Myinga
Mgeni Rasmi katika uzinduzi wa Maisha Plus/ Mama shujaa wa Chakula 2013 Mkuu wa Wilaya ya Mvomero Mh. Anthony Mtaka  akifanya uzinduzi wa aina yake wa Maisha Plus/ Mama Shujaa wa Chakula 2012/13 kwa kufukua fomu ambazo zilikuwa zimefukiwa ikiwa ni kielelezo cha kilimo kwanza
  Mkuu wa Wilaya ya Mvomero Mh. AnthonyMtaka  akizionesha fomu hizo baada ya uzinduzi huo.
 
Mgeni Rasmi Mkuu wa Wilaya ya Mvomero Mh. Anthony Mtaka akimkabidhi Fomu ya kwanza ya ushiriki kwa Bi. Nuru Saidi Mbonga kutoka Dakawa ikiwa ni fomu ya Mama shujaa wa Chakula 2013.
 Mmoja ya Vijana wakiume nae akiwa anakabidhiwa fomu ya ushiriki na Mgeni rasmi  Mkuu wa Wilaya ya Mvomero Mh. Anthony Mtaka
Wakiwa wanasoma fomu na kujiandaa kuzijaza 
 
 Burudani za Ngoma zikiendelea
 Burudani za aina yake zikiendelea.
 Mkurugenzi Mtendaji wa Maisha Plus Ali Masoud ‘Kipanya’ akifunga sherehe fupi za uzinduzi wa Maisha Plus 2013