Sherehe za Mapinduzi Zanzibar zafana

Magari ya msafara wa Rais wa Zanzbar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein yakiingia ndani ya Uwanja wa Amani mjini Zanzibar jana wakati wa sherehe za maadhimisho ya miaka 48 ya Mapinduzi ya Zanzibar. (Picha na Aron Msigwa –MAELEZO)

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi , Dk. Ali Mohamed Shein akikagua gwaride. (Picha na Ikulu Dar es Salaam)

Rais Jakaya Kikwete (kulia) akisalimiana na Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar, Maalim Seif Shariff Hamad. (Picha na Ikulu Dar es Salaam)

Viongozi mbalimbali wakuu wa nchi Zanzibar na Tanzania Bara. (Picha na Ikulu ya Dar es Salaam)

Rais wa Zanzbar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein akipokea heshima kwa kupigiwa mizinga 21 mara baada ya kuwasili katika uwanja wa Amani wakati wa sherehe za maadhimisho ya miaka 48 ya Mapinduzi Zanzibar jana. (Picha na Aron Msigwa –MAELEZO)

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk. Jakaya Kikwete akipokea heshima kwa kupigiwa mizinga 21 mara baada ya kuwasili katika uwanja wa Amani wakati wa sherehe za maadhimisho ya miaka 48 ya Mapinduzi Zanzibar jana. (Picha na Aron Msigwa –MAELEZO)

Makamu wa Kwanza wa Rais Maalim Seif Shariff Hamad na mkewe kushoto, Mke wa Rais Jakaya Kikwete, mama Salma Kikwete na Waziri Mkuu wa Tanzania, Mizengi Pinda (kulia). (Picha na Ikulu Dar es Salaam