
Baadhi ya waumini wa dini ya Kiislamu na wananchi wa Dar es Salaam wakiangalia vijana wa wakisherehekea siku kuu ya Idd kwa kuimba na kucheza mitaa ya soko la Kariakoo.

Baadhi ya waumini wa dini ya Kiislamu wakiwa katika msikiti wa Al-Ghadiir Kigogo jijini Dar es Salaam jana mara baada ya swala ya Iddi.

Alhaji Yusufu Saidi Mfinanga wa Kibaha Njuweni Pamoja na mkewe Mama Mfinanga katika kusherehekea siku kuu ya Iddi wamewaomba Watanzania kudumisha amani na upendo kwa kuondoa tofauti za kidini na kisiasa kwani kufanya hivyo Mungu ataendelea kuijalia amani na baraka nchi. Kupendana kutaleta maendeleo katika nchi hivyo tuswali na kuheshimu mamlaka za Serikali zilizopo.